Wakuu salamu,
Leo naomba tujiambie ukweli mchungu ambao wengi watauchukia, lakini ndio ukweli halisi. Kama wewe ni mwanaume au mwanamke unayeendekeza uzinzi na ngono zembe, sahau kabisa habari ya kufanikiwa kimaisha kwa njia halali ya jasho lako.
Ukiona mtu ni mzinzi wa kutupwa na bado ana ukwasi mkubwa, chunguza vizuri mfumo wa maisha yake. Utakuta aidha anasafiri na ndagu za waganga wa kienyeji, anajihusisha na utapeli (scams), au anafanya biashara haramu. Mafanikio ya halali na uzinzi hazitangamani.
Hizi hapa ni sababu kuu kwanini uzinzi utakuacha maskini:
1. Unapoteza Kibali na Baraka: Kiimani, uzinzi unakuondolea neema na mikosi inakuandama.
2. Mabadilishano ya Nuksi: Kila unayezini naye hubadilishana naye mifumo ya nishati; unabeba laana na mikosi yake.
3. Ufujaji wa Mtaji: Hakuna uzinzi wa bure. Pesa za guest, mizinga, na usafiri zinamaliza akiba yako.
4. Kupoteza Focus: Akili inayowaza ngono kila saa haiwezi kubuni mawazo mapya ya biashara au uwekezaji.
Kama unataka utajiri unaodumu na wenye amani ya moyo, fanya toba, tulia na mwenzi mmoja, na uweke nguvu kwenye kazi.
Nawasilisha wakuu. Je, unaamini kuna mtu anazini sana na anafanikiwa kwa njia halali kabisa?