Kama unaingiza faida ya Tsh. 30,000 na kuendelea kwa siku pita hapa

Kweli mkuu, hata mimi ninao sita, ila walio SMART ni wawili tu na ndio ninaowalipa vizuri, wengine wana changamoto mara uvivu, dharula zisizo na msingi...

Ila pia kazi hii inachosha, maana mimi wanaingia saa kumi na mbili asubuhi kutoka saa 4 usiku kwa siku 6 ktk wiki. Ila mchana wateja wakipungua huwa wana shift ya kupumzika
 
Mimi nimeajiriwa na Serikali na hapohapo nafanya biashara ya Mtumba. ninaagiza beli/robota la nguo za mtumba hii inategemea wateja wangu kwa wakati huo wanahitaji nini, naweza kuagiza skert/mashati ya kiume/blause/gauni au nguo za watoto beli moja tu ambalo naweza kununua kwa laki 450-1,000,0000 inategemea ni mzigo gani nimeagiza.

Tuamshum nimeagiza nguo za watoto beli 1 Grade one (1) inaweza kuwa 600,000 pamoja na usafiri na hela ya kutolea ninayemtumia hela inafika 650,000. Kwanza ifahamike mimi sina frame, ninachokifanya mzigo ukifika naenda kuupokea nafungulia home, muda huo nakuwa nimeshawasiliana na wateja wangu kwenye magroup ya whattsapp ya Kazini na mengineyo kwahiyo nikifungua wateja tayari wapo wanachagua.

Zinazobaki nawasiliana na watu wa Ofisi nyingine nampa Boda 1000 najaza nguo kwenye begi mbili ambapo nakuwa nimezihesabu ananipeleka Ofisi flani wanachagua then wananiandikia majina na idadi ya nguo walizochuku. Baada ya hapo akirudi nacheki nguo namjazia tena nampa nauli yake naongea na mtu wa Ofisi nyingine ananipelekea tena huko.

Najikuta nauza nguo zote kwa muda mfupi sana ndani ya wiki nakuwa nimeshauza nguo zote ama zimebaki chache ambapo kwa beli la laki 600,000 nikiuza napata 1,300,000 au zaidi japokuwa biashara yangu niya kukopesha kwa mwezi. Hivyo ikifika karibia na mwisho wa mwezi naanza kuwakumbusha kwa sms. Inanilipa kwakweli namshukuru Mungu sitegemei mshahara, na kwa mwezi naweza leta mzigo mara mbili.
 
Balo zako waagiza kutoka wapi mkuu?
 


Duh hongera ..kwa faida hii nadhan ni dar mikoani kupati faida km hyo kbs!haipogo
 
Mkuu una idea nzuri sana afu unazitoa bila choyo safi sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…