Kama unaingiza faida ya Tsh. 30,000 na kuendelea kwa siku pita hapa

Duh hongera ..kwa faida hii nadhan ni dar mikoani kupati faida km hyo kbs!haipogo
una chembe chembe za ubishi wa kutaka kuamini unachotaka

mkoani hamna hiyo faida una uhakika?

umeshafanya hiyo biashara mikoa mingapi??

kwanini watu mnaamini dar ndio kuna biashara kuliko mikoani?

iko hivii

hiyo faida inaweza kupatikana DAR na mikoani ikapatikana vile vile
 
Popcorn asee.

Tafuta mashine ya popcorn, hukosi 30 kila siku.
ataenunua hii mashine namshauri biashara akafanyie wenye mlango wa Drasa la Tatu B

ili wanafunzi wakienda chooni wanamuona,wakienda break wanamuona,wakiwa darasani wanamuona

ilaaa

tofauti na hapo aseee mtu kapoteza hela yake plus Muda Juu bora angeuza ice cream
 
Hii biashara kuna jamaa alindokezea majuzi, kuna mwamba ana hivyo vyuma sokoni anakunja 90-100k deile
one of the hidden idea watu wasio ijua

wanasema ukienda shamba ukiona kila mtu anawaza nilime zao gani

we nenda kawauzie Majembe (usilime)

maana vyovyote vile hawatolimia mikono lazima waje kufata majembe ndio walime.
 
Umenishawishi sana kiongozi ila hujataja bei ya kila nguo!
 
asilimia kubwa ya wanaofeli dar, kinachowaponza zaidi ni kukataa kukubali kua kuna mikoa mingine unaeza ukapiga sana pesa kuliko hata dar.. wanabaki wanasema wanakomaa na jiji kuna ishu wanaisikilizia [emoji23]
 
huwa siogopi kumshirikisha mtanzania mawazo yangu maaana najua wengi ni waskilizaji sio watendaji

so nafungukaga tu hata siogopi maana najua wanajua kuitikia wameelewa ila hawataki kuingia ktk utendaji

wengi ni waoga na wachagua fursa.
Haa haaahaaa haa sijawahi cheka hivi[emoji23][emoji23][emoji23]

Ila mkuu uko vizuri mwaya[emoji108][emoji108]
 
Acha ukuda we mzee. Pale Makumbusho kuna mashine ngapi za popcorn....pale ni shuleni?
Mbagala Rangi 3 stand kuna wauza popcorn wangapi? Pale ni shuleni?

Pale mwenge ukivuka tu mataa upande huu wenye sheli ya Puma kuna jamaa anachoma popcorn, na yule mimi ndio aliniambia anaingiza mpaka elfu 50 wakati mtaji wake kwa siku ni chini ya shilingi 20,000.

Una fact?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…