Kama unaingiza faida ya Tsh. 30,000 na kuendelea kwa siku pita hapa

dar panalemaza kama hamna kinachokuingizia

Unalemewaje hata km luku inakusumbua?? Mm nnachafuka balaa ukiniona huwez jua ni mm..lakini nna amani moyoni najua napata nn...hii ni njia tu ya kuelekea ninapotaka...!ss kila siku unashinda saloon...ina maana gani ss..wanao unawatengenzea fyucha gan?umewah jiuliza ukifa wanao watasurvive vip!mm nikikumbuka hapo napata wazimu wa kuzitafta!
 
safi sana mkuu, mimi pia nmewaambia hao mchawi ni location ,na huduma bora pia kauli nzuri kwa wateja
 
Mkuu kuna chuo kinafundisha ufundi simu
 
Mkuu kuna chuo kinafundisha ufundi simu
Mkuu mimi siajafundishwa na mtu, ni internet, youtube tutorial za kutosha na kukosea
mpaka na master simu nishazizima simu kama kumi za watu kwa kuflash wrong ROM.

Kama unataka chuo basi nakushauri nenda veta Soma Eletronics Hata Miez Sita Au Mwaka Vilivyobakia Tafuta Moderm Pitia Mwenyewe Lazima Utafanikiwa Tu.
Pitia Thread Hii Chini Utajifunza Kidogo

 
Nauza askirimu hizi za Mia Mia friza mbili! Moja nilikununua jipya 850,000 ni deep friza na lingine nilinunua used 400,000, baiskeli zakuzungushia 110,000, deli za kuuzia 100,000!
Faida ipoje?
 
Hongera chief..Mtaji wako utakuwa around 30ml..Mleta mada anaonyesha Bado Yuko kwenye starting point mean capital yake Itakuwa less milion..Sasa Nafikiri ushauri mzuri kwake atafute biashara hizi za kutembeza,. Yaani asiwe na operating expenses kubwa..Kuna mama 1 Anauza matunda Mtaji wake Ni Kama laki 2..Ni mdau wangu Aliwahi niambia kwa siku anaweka elfu 20..Kama faida..Pia Kuna madogo wanalenga viatu, trousers, nk..Awa awkosi 20 Mpaka 30..Per day na huu ndo msimu..wa biashara.So mleta mada jichanganye kwa uzoefu wangu Akuna mbongo atakueleza exactly faida ya biashara anayofanya..Atakwambia Ni hasara tu Cha kushangaa yeye afungi iyo biashara inayompa hasara na anazidi kufanya maendeleo..
 
ANGALIZO
Biashara pia inategemea vitu viwili muhim, kama kuna mchungaji unaemwamin sali Sana. Kama unamganga unaemwamin roga sana, usiwe vuguvugu

huu ni ukweli mchungu ambao wengi wataupinga
Upo sahihi wengi watakuambia biadshara wanazofanya na faida yake lakini hawasemi kama wamenda kwa KALIMANZILA ila ukweli biashara bila kupata Tiba ya Mvuto utasota sana.
 
Hahah frem za laki 2 hapo bado na w/holding tax ya 10% ya serikali itakuhusu.
Hii w/holding tax serikali inabidi iitoe tu maana ni wizi, unamkata mtu kodi unamwambia mwenye nyumba atairudisha, anairudishaje? na wengi hawarudishi maana wanakuwa wamelipa kodi ya jengo hivyo kurudisha hiyo kodi kwa mpangaji ni kumuumiza zaidi, huu mpango JPM inabidi aingilie kati.
 
npe huo mchongo mm niuendeleze nna shda na pesa hapa nlipo ni balaaa ziiitoooo yna2
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…