Kama unaingiza faida ya Tsh. 30,000 na kuendelea kwa siku pita hapa

Hii ulikua unaifanyaje?
 
Nimesoma kuanzia post ya mtoa mada mpaka comment ya mwisho wakati huu nimetype.

Huu uzi udumu milele kwamaana madini yake yanasaidia Sana.

Muhimu naenda kwenye utendaji moja kwa moja.
Mitaji kwa fursa nyingi zilizotolewa humu ni ya kawaida sana.
 
Biashara ya kusaga na kuuza Chupa za plastiki zilizotumika za maji na juisi ... hii biashara ina pesa sana ila watu bado hawajaishtukia

Unanunua Chupa kutoka kwa hawa waokota Chupa mitaani... tena hata huwaiti, wakiona tu umefungua dago wanajileta wenyewe.
 
Ongezea nyama kidogo mkuu

Mashine ya kuzisaga ni zipi? Na baada ya kuzisaga soko liko wapi?
 
Ukisaga unaenda kumuuzia nani boss
 
Biashara ya kuuza utumbo unaweza kunja elfu 30 kabis kwa siku na biashara unafunga saa nane.

Kwa mtaji usiozidi milioni moja unafanikisha zoezi.

Mahitaji..
mzani mmoja wa laki na nusu..
Banda linatengezwa kwa laki na nusu..
kodi ya eneo unalipa miezi sita, assume 180k...

manunuzi;
utumbo unagharimu maximum laki 1, lakin bei ni elfu 60-80.

Hela ya kula fanya elfu 3.

Nauli kwenda home fanya 1500

Biashara inafanyikia pembeni ya bucha, kilo ya utumbo ni elfu 4-5.


usafiri ni assume elfu 5.

JUMLA KUU: kwa haraka haraka ni LAKI 6.

MAUZO NA FAIDA

Kilo 1 ya utumbo ni Tshs elfu 4 mpaka elfu 5.

kama umebeba mzigo wa kilo 30 na ukauza wote it means

35kg of utumbo×4000Tsh @kg=140,000Tshs. Gross profit.

TUNAONDOA GHARAMA TUPATE KINACHOBAKI.

140,000-100,000=40,000/=

Nauli 5000
Kula 3000
nauli tena 1500
Jumla 9500

Tunatoa tena;
40,000-9500=30,500

Mia 5 natoa naweka kwenye kibubu kila siku

inabaki hio 30,000 cash.

Hii biashara nimeifanyia utafiti kuanzia machinjio ya ng'ombe kule mazizini gogolamboto na nimeongea na wauza utumbo maeneo ya tabata na buguruni, wengi wanasema faida ya elfu 20 mpaka 40 ni kawaida kabisa na biashara huwa hot kipindi cha sikukuu.

CHA MUHIMU UPATE ENEO ZURI.

wakuu mimi sina mtaji ila ningependa kuifanya hii kazi.

atakaependa kunisaidia, karibu. Nipo Dar es salaam
 
Namba zinatamaisha hizo
 
Boss mabegi ya mtumba unapata wapi
 
Mabelo ya nguo grade one unachukulia wapi je hawachakachui
 
Sio rahisi kihivyo mama ntilie hawa wanapenda kukopakopa
 
jangala, sometyme hawa mama ntilie wanapika kilo 5 za mchele na wali unalala, je kwny stuation kama hz utadai hyo buku jero?
na je kama kilo 5 tu znalala ni nan akubali kupokea laki yako akat anaona kabisa hata msosi wa 50k unasumbua kuisha
Ndio hapo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…