Mtaji kuanzia laki moja na kuendelea ndo itakuwa fresh, lakini mimi nilianza na tsh 30k saiv naona faida hata ya 25k, had 50k siku nyingine kama faida.
Hapa parcel moja nauza tsh 2000 ..nikiwa na parcel 50 tu nikipita ofisi tano zinaisha zote..
Hili hii biz ..pia ongezea na value kidogo, yani kuwa mchangamfu, mchekeshaji hehehe hukosi wateja..
Wanaotafuta Ajira achezi kupoteza Muda hakuna ajira kwa sasa ila kazi zipo za kufanya. Ondoa aibu, mimi nakutana na wenzangu niliomaliza nao chuo, wapo tu eti wamejishkiza, kimshara chenyewe 3k,4k,5k, ukiotea sehemu nzuri ndo 10k hapo ujala, nauli, hujui ni lini utapata kazi ya kueleweka..
Nimegundua Kwamba watu ambao "hawajasoma" wanaingiza pesa nzuri sana kwa sababu hawana cha kupoteza. Wenzangu na mie wenye vi Degree vyetu tunachagua kazi za kufanya..
Mithali 10:4