Kama unaingiza faida ya Tsh. 30,000 na kuendelea kwa siku pita hapa

150,000/= Mimi ninayo mawili ilinitoka laki tatu mana mm yangu nime weka matairi ya pikipiki yaliyo tumika ambapo fremu pekee nili tengeneza kwa 60,000/= hayo matairi mawili nilinunua 90,000/=

Return yake ikoje hii mkuu.....
 

Hongera sana nimeipenda 🤝
 
Wow huu ushauri ni mzuri mkuu, thank you itabidi nifanye hivo maana saving kwa hiari ni ngumu😐
Kuwa na account ambayo hauwezi kuiaccess muda wote, mie nna jr account.... Unajaza ile huduma ya kukatwa kiasi flani katika mshahara then inaingia huko, inategemea na kipato chako sasa ukikatwa laki mbili miezi mitano tu una 1m umepata mtaji wa kutosha kabisa kuanzia.
 
Mkuu... Huyu mwamba anazungumzia faida ya 30K kwa siku. Boda ya 2.5m inakupa 10K kwa siku. Inakupasa uwe na boda 3 ili kupata 30K kwa siku... Hapo mtaji ni 7.5m

Kuna vibiashara vinaonekana vya kizembe lakini kwa hiyo 2.5m unakika 30K kiroho safi kabisa.

Hivi kwa mfano unajua kreti moja ya bia inakupa faida ya 5K? Kreti 6 tu unalamba 30K.

Ka grocery tu ambako unaweka na kajiko ka chipsi na mishikaki... Ukauza hata vikreti vitatu vya bia + Visoda + Vi-K Vant, nyagi, smart gin, maji na vitakataka vingine unaikunja 30K korahisi tu. Mtaji waweza usifike 4m.

Tatizo hivi vidigrii vinafanya wengi wabague kazi za kufanya...

Kuna kagrocery kanakunja faida mpaka nashangaa. Afu kuna mjasiriamali aliomba aweke shoeshine and repair pembeni na kuuza juice. Jamaa yule pia anaosha magari ya wateja kiaina anatengeneza mkwanja mpaka namwonea wivu natamani nimtoe pale lakini Roho wa Mungu ananikataza
 
Mbinguni utaenda kulala chooni
 

Hapa kuna lesson ya mtaji, kuna watu hukimbilia kusingizia hatuna mitaji kumbe mitaji tunayo afu hatujui 😁

Hongera sana mkuu 👍👍 ahsante kwa mchango wako
 
Hongera hapa kuna funzo kwamba ukipata mke sahihi ni rahis kufanikiwa.
 
Mkuu ulichosema ni sahihi mimi mara ya kwanza naona huu uzi mwaka 2021 nilipata wazo la biashara nikalifanyia kazi huku mkoani nilipo huwez amini mtaji hauzidi laki 2 lakini nakunja elfu 40 mpaka 50 kama faida kwa siku, nikikosa sana naambulia 25k mpaka 30k.... Hapa nataka nikitulia niweke goli kabsa maana pamechangamka!
 
Ahsante sana ngoja nifanye hivyo pia, maana saving imekua shida pesa haikai
 
Biashara gani hiyo si muwe mnasema na biashara mnayofanya kwa faida ya wengi maana ndo dhumuni la huu uzi! Ukisema tu unakunja kiasi fulani kwa siku haimsaidii msomaji!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…