Setfree
JF-Expert Member
- Dec 25, 2024
- 1,679
- 2,123
Usiseme natukana watu, soma mpaka mwisho utajua kwanini kichwa cha uzi kimeandikwa hivyo.
Katika mijadala na malumbano ya hoja hapa JF, kuna watu wengi waliojaa hasira vifuani mwao. Wanakasirishwa na maneno au vitendo vidogo vinavyoweza kuepukika.
Yafuatayo ni baadhi ya mambo madogo ambayo mara nyingi humfanya mtu aliyejaa hasira akasirike:
Kama umegundua mojawapo ya mambo hayo yanakukasirisha, basi fahamu kuwa mbele za Mungu unahesabika “mpumbavu.” Biblia inasema: "Usifanye haraka kukasirika rohoni mwako, maana hasira hukaa kifuani mwa wapumbavu."(Mhubiri 7:9).
Katika mijadala na malumbano ya hoja hapa JF, kuna watu wengi waliojaa hasira vifuani mwao. Wanakasirishwa na maneno au vitendo vidogo vinavyoweza kuepukika.
Yafuatayo ni baadhi ya mambo madogo ambayo mara nyingi humfanya mtu aliyejaa hasira akasirike:
- Akiulizwa maswali magumu – Wakati wa mijadala, mtu anaweza kuulizwa maswali yanayohitaji ufafanuzi wa kina au uthibitisho wa madai yake. Badala ya kuchukulia maswali hayo kama fursa ya kueleza hoja yake vizuri, mtu aliyejaa hasira anaweza kuhisi kama anashambuliwa au anawekewa mtego wa kumfanya ashindwe kujibu. Anaweza kuona kama anaonewa, anadharauliwa au kulazimishwa kukiri kuwa uzi wake hauna mashiko
- Akikosolewa uandishi wake – Akikosea kuandika na watu wakalenga tu kuonyesha makosa hayo badala ya hoja yake, anachukia na kukasirika.
- Akitajwa jina au akiona emoji ya kejeli – Emoji kama 😂, 🤦♂️, au 😏 zinaweza kumuudhi sana. Na akitajwa jina lake, anaweza kuona kama vile anapigwa vita moja kwa moja na kwa sababu hiyo anajaa hasira.
- Akipachikwa jina la dharau – Akiitwa majina kama "mjinga," "chawa” au "hater," anapandwa na hasira haraka.
- Akiambiwa akapime afya ya akili – Anaweza kuona kama amedharauliwa au kutiliwa shaka akili yake.
- Akishutumiwa kwa lengo ambalo hana – Mfano, akionekana kama ana ajenda fulani ya siri, anaweza kujihami kwa hasira.
- Akijibiwa tu kwa "OK" au "Sawa" badala ya maelezo marefu – Anaweza kuona kama amepuuzwa au hajaheshimiwa na hivyo anajaa hasira.
- Akishambuliwa na kundi kubwa – Akiona watu kadhaa wanamshambulia kwa mpigo, anaweza kulipuka kwa jazba.
- Akijibiwa kwa “meme” badala ya hoja – Picha za utani zinapotumika kujibu hoja yake anayoiona ya maana, anachukia na kukasirika.
- Akiambiwa "huna pointi" au “hujui unachosema,” – Anakasirika na kuona kama amedhalilishwa.
- Akiambiwa "acha kuandika kwa kukurupuka" – Anakasirika akifikiri wanamaanisha hajui kitu chochote alichoandika.
- Akipewa "reaction" ya kicheko😂 kwenye hoja yake “serious” – Anakasirika kwa kuhisi amefanyiwa mzaha.
- Mada anayoitetea ikipuuzwa – huku nyingine anazoona hazina uzito zikipewa kipaumbele, anakasirika na kuona kama kuna upendeleo.
- “Moderator” au "Content Manager" akiunganisha au kuuhamishia panapostahili uzi wake – Anakasirika na kuhisi kama ananyamazishwa kwa makusudi.
- Akiambiwa amewekwa kwenye “ignore list” – Anakasirika sana na kumchukia huyo aliyemwambia hivyo.
Kama umegundua mojawapo ya mambo hayo yanakukasirisha, basi fahamu kuwa mbele za Mungu unahesabika “mpumbavu.” Biblia inasema: "Usifanye haraka kukasirika rohoni mwako, maana hasira hukaa kifuani mwa wapumbavu."(Mhubiri 7:9).