Kama unakasirika sababu ya jambo moja kati ya haya fahamu wewe ni Mpumbavu kabisa

Usiseme natukana watu, soma mpaka mwisho utajua kwanini kichwa cha uzi kimeandikwa hivyo.

Katika mijadala na malumbano ya hoja hapa JF, kuna watu wengi waliojaa hasira vifuani mwao. Wanakasirishwa na maneno au vitendo vidogo vinavyoweza kuepukika.

Yafuatayo ni baadhi ya mambo madogo ambayo mara nyingi humfanya mtu aliyejaa hasira akasirike:
  • Akiulizwa maswali magumu – Wakati wa mijadala, mtu anaweza kuulizwa maswali yanayohitaji ufafanuzi wa kina au uthibitisho wa madai yake. Badala ya kuchukulia maswali hayo kama fursa ya kueleza hoja yake vizuri, mtu aliyejaa hasira anaweza kuhisi kama anashambuliwa au anawekewa mtego wa kumfanya ashindwe kujibu. Anaweza kuona kama anaonewa, anadharauliwa au kulazimishwa kukiri kuwa uzi wake hauna mashiko
  • Akikosolewa uandishi wake – Akikosea kuandika na watu wakalenga tu kuonyesha makosa hayo badala ya hoja yake, anachukia na kukasirika.
  • Akitajwa jina au akiona emoji ya kejeli – Emoji kama 😂, 🤦‍♂️, au 😏 zinaweza kumuudhi sana. Na akitajwa jina lake, anaweza kuona kama vile anapigwa vita moja kwa moja na kwa sababu hiyo anajaa hasira.
  • Akipachikwa jina la dharau – Akiitwa majina kama "mjinga," "chawa” au "hater," anapandwa na hasira haraka.
  • Akiambiwa akapime afya ya akili – Anaweza kuona kama amedharauliwa au kutiliwa shaka akili yake.
  • Akishutumiwa kwa lengo ambalo hana – Mfano, akionekana kama ana ajenda fulani ya siri, anaweza kujihami kwa hasira.
  • Ajibiwa tu kwa "OK" au "Sawa" badala ya maelezo marefu – Anaweza kuona kama amepuuzwa au hajaheshimiwa na hivyo anajaa hasira.
  • Akishambuliwa na kundi kubwa – Akiona watu kadhaa wanamshambulia kwa mpigo, anaweza kulipuka kwa jazba.
  • Akijibiwa kwa “meme” badala ya hoja – Picha za utani zinapotumika kujibu hoja yake anayoiona ya maana, anachukia na kukasirika.
  • Akiambiwa "huna pointi" au “hujui unachosema,” – Anakasirika na kuona kama amedhalilishwa.
  • Akiambiwa "acha kuandika kwa kukurupuka" – Anakasirika akifikiri wanamaanisha hajui kitu chochote alichoandika.
  • Akipewa "reaction" ya kicheko😂 kwenye hoja yake “serious” – Anakasirika kwa kuhisi amefanyiwa mzaha.
  • Mada anayoitetea ikipuuzwa – huku nyingine anazoona hazina uzito zikipewa kipaumbele, anakasirika na kuona kama kuna upendeleo.
  • “Moderator” au "Content Manager" akiunganisha au kuuhamishia panapostahili uzi wake – Anakasirika na kuhisi kama ananyamazishwa kwa makusudi.
  • Akiambiwa amewekwa kwenye “ignore list” – Anakasirika sana na kumchukia huyo aliyemwambia hivyo.
Mambo ni mengi, ongezea na wewe...

Kama umegundua mojawapo ya mambo hayo yanakukasirisha, basi fahamu kuwa mbele za Mungu unahesabika “mpumbavu.” Biblia inasema: "Usifanye haraka kukasirika rohoni mwako, maana hasira hukaa kifuani mwa wapumbavu."(Mhubiri 7:9).
Well said
 
Kuna watu wanapenda ligi, yaani hata uki reack kwa ku dislike Anakasirika anaku quote ili akutukane,

Sent from My iPhone 16 Pro max, Nimeinunua jana pale karume karibu na duka la mapajama.
Umeona eeh?
 
Kabisa. Biblia naijua vizuri na pia najua hasira hukaa kifuani mwa wapumbavu.
Kukasirika ni moja wapo ya sifa za ubinadamu na kiumbe yeyote hai, hasa pale unapo chokoza hisia zake, huwezi kukosa hasira alafu ujiite binadamu. Hata Mungu huwa ana kasirika mtu anapo kengeuka mafundisho yake na ndo maana atatoa adhabu kali kwa wasio mtii.
 
Sikai kimya na wala sikasiriki badala yake nakuombea:
"Ee Mungu mkumbuke SweetyCandy kwenye ufalme wako. Msaidie kuudhibiti ulimi wake usinene matusi. Maana watukanao hawataurithi ufalme wako. In Jesus' name, I pray, Amen."
Utapata wa kufanana naye heri wale wanahukumu wengine maana wataingia ufalme wao sio wa Mungu humjaji mtu mie sijakutukana nimekupa facts .
Jingine mke mwema hajufichi kwenye ngozi ya kondoo bali hukubali kukosea
 
Kukasirika ni moja wapo ya sifa za ubinadamu na kiumbe yeyote hai, hasa pale unapo chokoza hisia zake, huwezi kukosa hasira alafu ujiite binadamu. Hata Mungu huwa ana kasirika mtu anapo kengeuka mafundisho yake na ndo maana atatoa adhabu kali kwa wasio mtii.
Mwenzako kaja na gia zake
 
Hasira ya mwanadamu haitendi haki ya Mungu(Yak 1:20)
 
Utapata wa kufanana naye heri wale wanahukumu wengine maana wataingia ufalme wao sio wa Mungu humjaji mtu mie sijakutukana nimekupa facts .
Jingine mke mwema hajufichi kwenye ngozi ya kondoo bali hukubali kukosea
Umenichekesha: "wataingia ufalme wao ila sio wa Mungu..."

Usikasirike, SweetyCandy sijakuhukumu na wala sina uwezo huo. Mimi pia nimekupa facts kwamba nikitukanwa sikai kimya ila badala ya kukasirika na kujibu tusi kwa tusi namwombea aliyenitukana.
 
Juzi kati niliweka bandiko kuomba msaada account yangu ya whatspp business imefutwa na meta aissee Kuna member mmoja aliweka comment ya dhihaka ilahali hajui maumivu niliyonayo moyoni kuhusu iyo situation aisee mpaka Leo nikipitia machapisho yake namuona kama Nini vile. Any way ya hum unayaachia hum huwezi muwekea kisiriri mtu Ambae hata humjui ila ukweli roho/ utu mtu unapimwa kwa machapisho anayoyaweka, Kuna watu hum Wana roho mbaya sana harafu unakuta ni mwanamke mpaka unajiuliza haka kadem mbona kana roho ngum hivi?
 
Usiseme natukana watu, soma mpaka mwisho utajua kwanini kichwa cha uzi kimeandikwa hivyo.

Katika mijadala na malumbano ya hoja hapa JF, kuna watu wengi waliojaa hasira vifuani mwao. Wanakasirishwa na maneno au vitendo vidogo vinavyoweza kuepukika.

Yafuatayo ni baadhi ya mambo madogo ambayo mara nyingi humfanya mtu aliyejaa hasira akasirike:
  • Akiulizwa maswali magumu – Wakati wa mijadala, mtu anaweza kuulizwa maswali yanayohitaji ufafanuzi wa kina au uthibitisho wa madai yake. Badala ya kuchukulia maswali hayo kama fursa ya kueleza hoja yake vizuri, mtu aliyejaa hasira anaweza kuhisi kama anashambuliwa au anawekewa mtego wa kumfanya ashindwe kujibu. Anaweza kuona kama anaonewa, anadharauliwa au kulazimishwa kukiri kuwa uzi wake hauna mashiko
  • Akikosolewa uandishi wake – Akikosea kuandika na watu wakalenga tu kuonyesha makosa hayo badala ya hoja yake, anachukia na kukasirika.
  • Akitajwa jina au akiona emoji ya kejeli – Emoji kama 😂, 🤦‍♂️, au 😏 zinaweza kumuudhi sana. Na akitajwa jina lake, anaweza kuona kama vile anapigwa vita moja kwa moja na kwa sababu hiyo anajaa hasira.
  • Akipachikwa jina la dharau – Akiitwa majina kama "mjinga," "chawa” au "hater," anapandwa na hasira haraka.
  • Akiambiwa akapime afya ya akili – Anaweza kuona kama amedharauliwa au kutiliwa shaka akili yake.
  • Akishutumiwa kwa lengo ambalo hana – Mfano, akionekana kama ana ajenda fulani ya siri, anaweza kujihami kwa hasira.
  • Ajibiwa tu kwa "OK" au "Sawa" badala ya maelezo marefu – Anaweza kuona kama amepuuzwa au hajaheshimiwa na hivyo anajaa hasira.
  • Akishambuliwa na kundi kubwa – Akiona watu kadhaa wanamshambulia kwa mpigo, anaweza kulipuka kwa jazba.
  • Akijibiwa kwa “meme” badala ya hoja – Picha za utani zinapotumika kujibu hoja yake anayoiona ya maana, anachukia na kukasirika.
  • Akiambiwa "huna pointi" au “hujui unachosema,” – Anakasirika na kuona kama amedhalilishwa.
  • Akiambiwa "acha kuandika kwa kukurupuka" – Anakasirika akifikiri wanamaanisha hajui kitu chochote alichoandika.
  • Akipewa "reaction" ya kicheko😂 kwenye hoja yake “serious” – Anakasirika kwa kuhisi amefanyiwa mzaha.
  • Mada anayoitetea ikipuuzwa – huku nyingine anazoona hazina uzito zikipewa kipaumbele, anakasirika na kuona kama kuna upendeleo.
  • “Moderator” au "Content Manager" akiunganisha au kuuhamishia panapostahili uzi wake – Anakasirika na kuhisi kama ananyamazishwa kwa makusudi.
  • Akiambiwa amewekwa kwenye “ignore list” – Anakasirika sana na kumchukia huyo aliyemwambia hivyo.
Mambo ni mengi, ongezea na wewe...

Kama umegundua mojawapo ya mambo hayo yanakukasirisha, basi fahamu kuwa mbele za Mungu unahesabika “mpumbavu.” Biblia inasema: "Usifanye haraka kukasirika rohoni mwako, maana hasira hukaa kifuani mwa wapumbavu."(Mhubiri 7:9).
Una shida kichwani
 
Juzi kati niliweka bandiko kuomba msaada account yangu ya whatspp business imefutwa na meta aissee Kuna member mmoja aliweka comment ya dhihaka ilahali hajui maumivu niliyonayo moyoni kuhusu iyo situation aisee mpaka Leo nikipitia machapisho yake namuona kama Nini vile. Any way ya hum unayaachia hum huwezi muwekea kisiriri mtu Ambae hata humjui ila ukweli roho/ utu mtu unapimwa kwa machapisho anayoyaweka, Kuna watu hum Wana roho mbaya sana harafu unakuta ni mwanamke mpaka unajiuliza haka kadem mbona kana roho ngum hivi?
Pole, issac77, msamehe bure
 
Kuna button ya ignore list hapo juu kwenye profile yako.
Mtu akikukera bonyeza hapo hutamuona tena.
 
Back
Top Bottom