Kama unaogopa hasara, baki na hela zako

Kama unaogopa hasara, baki na hela zako

Mzee Mengi alikuwa na gazeti linaitwa ALASIRI. Halikuleta faida. Gazeti la Dar Leo vile vile. Ushindani wa magazeti mengine ulikuwa mkali. Wasomaji wakabadilika. Internet zikaingia nk.

Akaachana nayo. Afu wewe eti unataka ufundishwe biashara ambayo hutaki kupoteza hela. Kaa na hela zako tu kwa kweli.
Hivi unadhani Novida imeenda wapi. Kama Coca Cola wanakosa soko la bidhaa yao wewe je? Lakini CocaCola wamefilisika? Mengi amefilisika? No.

Okay, tufanye hivi, ule ukumbi wa Sinema pale Mwenge ITV ulikufa kifo cha fasta. Competition. Century Cinemax ilileta upinzani. Wenye mradi wakajifunza. Kuna matajiri wengi tu walipoteza sana pesa. Mabasi ya Scandinavia yapo tena? Kuna maduka mengi tu Kariakoo yamefungwa kipindi hiki.

Ni kawaida kwenye ulimwengu wa biashara. Si uliona Landmark Hotel Ubungo ilibadilishwa ikawa hostel. Umeona jinsi ambavyo tayari amerejea na kuwa hoteli ya kisasa zaidi. Alishajifunza. Sijui unaelewa?

Dar Village hapo Rose Garden Kijitonyama haijajengwa hadi leo. Mradi wa mabilioni uliingia mdudu miaka zaidi ya 8 sasa. Wewe unataka utakachoanza nacho kisife. Hela zako hutaki zipotee. Aisee you're not an entrepreneur. Kaa tu na hela zako. Bora ukazinywee soda tu au kula nyama choma kama unataka. Umekuwa mtu wa kutaka mafanikio yasiyo na changamoto yoyote. Ndo maana unasubiri ukiambiwa aisee biashara ya Matikiti inalipa hatari huyo umo. Ukiambiwa mayai ya kware yanalipa huyo. Hutaki kutulia kwanza ujifunze.
Hakuna biashara isiyolipa. Ila kuna akili zisizo za kibiashara ambazo lazima kuzibadili zijue biashara faida na hasara ni kawaida kabisa. Wanasema SOMETIMES YOU WIN AND SOMETIMES YOU LEARN.

Sasa wewe hutaki kulearn utafikaje kwenye mafanikio kibiashara?
Trump mwenyewe alifilisika kabisa. NIL. Zero. Rock bottom. Licha ya kuanza kwa mtaji mkubwa. Kama haupo tayari kukosekana pesa basi kazinunulie nguo mpya sikukuu zikifika uvae.
Na hiyo ndo maana kuna matajiri wachache. Wenye moyo wa UTHUBUTU katika jamii huwa ni wachache tu.
If you're afraid to lose money NEVER INVEST. Baki na hela zako.

Nikutakie moyo wa kuthubutu pale utakapoichungulia fursa yoyote.
 
Nachoona mimi huyu ndugu hataki wenzie wafanikiwe kwa vile yeye kaliwa anataka na wengine waliwe ndio maana naona utolewe tu.
Hapana ndugu utakuwa umemuelewa vibaya.....iwe yeye kafanikiwa au kapata hasara ila tu mzizi wa uzi wake ni kuwa watu wasiwe na matarajio makubwa ya kupata faida muda wote kwenye biashara bali wakati mwingine na hasara huwepo ingawa sio matarajio ya anayefanya biashara.....

Hivyo kuwa na matarajio makubwa ya faida upelekea mshttuko wa moyo pindi upatapo hasara!!!!....

Ndio maana akasema kama wewe unaogopa hasara basi usifanye kabisa biashara baki na hela zako!!!
 
Hapana ndugu utakuwa umemuelewa vibaya.....iwe yeye kafanikiwa au kapata hasara ila tu mzizi wa uzi wake ni kuwa watu wasiwe na matarajio makubwa ya kupata faida muda wote kwenye biashara bali wakati mwingine na hasara huwepo ingawa sio matarajio ya anayefanya biashara.....

Hivyo kuwa na matarajio makubwa ya faida upelekea mshttuko wa moyo pindi upatapo hasara!!!!....

Ndio maana akasema kama wewe unaogopa hasara basi usifanye kabisa biashara baki na hela zako!!!
Angetoa tuu kama onyo sio kwa hasira namna hiyo.
 
Ndio maana sisi tunaamini katika FX kwamba hasara hazikwepeki but profit izimeze loss

Risk takers knows this
 
Ebana mtoa UZI kwanza kula Senksi kadhaa toka kwangu....Asomae na aelewe... hili kwangu ni bonge la somo aisee... you made my day
 
Back
Top Bottom