Kama unaswali kuhusu pombe niulize?

Kuna hizi pombe mbili;

1.Hii ya Kwanza ni gongo ya marapurapu,unaambiwa kila unachokiona mbele yako,kuanzia viatu,nguo chafu,betri mbovu..Hahahah😅 unaweka kwenye pipa kisha unatoa gongo

2.kuna pombe kabla hujakunywa unafungwa kamba kwenye magoti(miguu) km tahadhari ukiachia haja kubwa ubaki Nayo mwilini mwako,usiwaharibie wengine burudani😀..inaitwa Pingu hiyo pombe!!

Hizi pombe mbili umeshawahi kuzijaribu? Vipi vibe lake likoje?
 
Kama mtu amekuwa addicted na pombe kiasi ambacho asipokunywa anatetemeka........nawezaje kumsaidia akaacha kabisa pombe
Yap. Inawezekana. Lakini chini ya uangalizi maalumu. Mtu kama huyo withdrawal inaweza hata kumuua. Kwanza anapewa dawa za kuzuia madhara ya kuacha pombe(withdrawal). Kisha anapewa za kuacha pombe. Huyo ndugu yako hata akilazwa na kukosa pombe anaweza pata madhara makubwa.
 
Hapana. Hizo sijawahi kujaribu.
 
Dawa za kuzuia madhara ya kuacha pombe ni zipi hizo? Na dawa za kuacha pombe ni zipi? Naomba uende deep nahitaji kufahamu zaid
 
Dawa za kuzuia madhara ya kuacha pombe ni zipi hizo? Na dawa za kuacha pombe ni zipi? Naomba uende deep nahitaji kufahamu zaid
Dawa ya kuzuia madhara ya kuacha pombe ni kama valium(Diazepam). Hii hufanya kazi kama pombe hivyo mtu huepuka witdrawal syndrome. Dawa za kusaidia kuacha ni kama disulfiram. Hii mtu akitumia inakuwa kama yamini, akigusa pombe anapata madhara yatayomfanya asitamani kabisa pombe.

Lakini madhara yatokanayo na kuacha pombe huwakuta wanywaji masugu tu.
 
Kuna siku hizo dawa nazo utaweza kuziacha?
 
Disulfiram inapatikana kirahisi maduka ya madawa kama inavyopatikana kirahisi diazepam? Je kuna sehem special anaweza patiwa hii huduma mpaka akaacha kabisa?
 
Kuna siku hizo dawa nazo utaweza kuziacha?
Yap, baada ya muda unaziacha
Kwa mfano, mnywaji wa safari, ukimpa kilimanjaro hawezi.. na mwingine hataki kabisaa...! achana na wale wa jiko la shamba halichagui kuni
Mapemdezi tu ya ladha. Haina sababu ya kitaalamu. Ni kama mwingine hawezi kunywa bia chungu(stout) kama Guiness. Au tamtamu(Ale) kama Redds.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…