Kama utani vile mwalimu Paulo anaweza kuja kuwa mkuu wa shule

Nje ya mada. Kuna mwalimu mmoja wa kike mama hivi, ana jina kama la yule mchungaji wa kawe. Huwa akiingia darasani mimi huwa nafurahi sana.
 
Nje ya mada. Kuna mwalimu mmoja wa kike mama hivi, ana jina kama la yule mchungaji wa kawe. Huwa akiingia darasani mimi huwa nafurahi sana.

Ni member wa jf yule mwalimu

Anaupiga mwingi sana japo wanamtupa kwenye idara ambazo hazina madhara kwa wafadhili
 
Mbona kwenye michezo alikataa jezi za umitashumta?
 
Tanzania ni sehemu ambayo hautakiwi kusema kitu flani hakiwezekani.Hii nchi hasa kwenye siasa kila kitu kinawezekana.

Ni nchi hii hii kuna mtu alituhumiwa ufisadi akajiuzulu uwaziri mkuu kisha akakaribia kushinda urais kwa chama kile kile kilichomtuhumu fisadi,akaaminiwa na watu zaidi ya mil 6 TZ hiyo.

Ni nchi hii katibu mkuu wa chama cha upinzani aliyekuwa anaiponda ccm akawaita majina mabaya aliyekuwa mstari wa mbele kuitoa ccm,mwisho wa siku akawakimbia wenzake dakika za mwisho akapewa ubalozi na aliokuwa anawaponda akatulia tuli.

Bado mkuu wa nchi hii kwa awamu inayofata anaweza kutoka ccm,swali ni je huyo anayetajwa ana tofauti gani kubwa na hao wenzake wengine? bado ni ndogo tu

Kama upo Tanzania na unabisha huyo Paul kuwa mkuu basi kuna namna una matumaini na hii nchi.na kuwa hivyo unahitaji kuwa na roho ngumu.
 
Wanafunzi wengi tunampenda yule mwalimu wa kujitolea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…