Kama uzinzi huleta umasikini, mbona kuna watu ni wazinzi wana maisha mazuri kiuchumi?

Kama uzinzi huleta umasikini, mbona kuna watu ni wazinzi wana maisha mazuri kiuchumi?

Balqior

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2021
Posts
2,406
Reaction score
8,039
Wanasema ukiwa mtu wa kutembea na kila mwanamke unajiletea mabalaa/mikosi wakimaanisha unakaribisha umaskini kwenye maisha yako, mbona kuna watu nawafahamu ni wanabadilisha wanawake kila kukicha, miaka nenda rudi, ila bado kipesa wako vizuri, na navowafahamu pesa zao si za kishirikina.

Hio stereotype imetoka wapi
 
Kitu chochote kikisemwa sana jua kinaukweli, jambo lolote lina kanuni ya muda kuleta matokeo hivyo hao unaowajua wanafanya uzinzi na Bado wapo vizuri kiuchumi wape muda utapata majibu baada ya kuanza kushuka kiuchumi.
 
Wanasema ukiwa mtu wa kutembea na kila mwanamke unajiletea mabalaa/mikosi wakimaanisha unakaribisha umaskini kwenye maisha yako, mbona kuna watu nawafahamu ni wanabadilisha wanawake kila kukicha, miaka nenda rudi, ila bado kipesa wako vizuri, na navowafahamu pesa zao si za kishirikina..

Hio stereotype imetoka wapi
Mkuu kwani unataka kufanyaje ?
 
Kitu chochote kikisemwa sana jua kinaukweli, jambo lolote lina kanuni ya muda kuleta matokeo hivyo hao unaowajua wanafanya uzinzi na Bado wapo vizuri kiuchumi wape muda utapata majibu baada ya kuanza kushuka kiuchumi.

nakubaliana na wewe mkuu

Sex is overrated,zinaa sio nzur mbali na kupoteza fedha na muda…inavutia majanga pia kwenye maisha na kizazi chako…moja kat ya kaz kubwa tunapaswa kuifanya binadamu n kujizuia,kujitawala,kujithibiti na kujiweza….
 
Wanasema ukiwa mtu wa kutembea na kila mwanamke unajiletea mabalaa/mikosi wakimaanisha unakaribisha umaskini kwenye maisha yako, mbona kuna watu nawafahamu ni wanabadilisha wanawake kila kukicha, miaka nenda rudi, ila bado kipesa wako vizuri, na navowafahamu pesa zao si za kishirikina..

Hio stereotype imetoka wapi
Labda chief tukuulize ww ulietuletea Uzi huu 😂
 
Huu ndio uonez wenyewe.Kizazi changu kimekosa nini wakat uzinzi nafanya kwa habar zangu binafsi? Halaf watu wakianzaga kupinga scripture kwa mambo kama haya mnaanza kuwaona sio.

Kizaz changu kinahusika vipi.
Ni mfumo wa nature wa uumbaji umeruhusu hivyo, hasa pale hicho kizazi kitakapoyashabikia Yale mabaya yaliyotendwa na wazazi wao, pona Yao nikuyaona kama yalikuwa chukizo basi wasiyashabukie.
 
Huwezi kuwa mzinzi alafu ukawa na Maisha mazuri.

Lakini unaweza ukawa na Maisha mazuri alafu ukawa mzinzi alafu baadaye ukafilisika.

Uzinzi unahitaji Pesa. Kwa kijana mtafutaji uzinzi haumfai Kwa sababu kidogo akipatacho kinatolewa macho na pisikali. Hivyo atakosa Pesa ya kuwekeza na kufanya Maendeleo.
Ukiwa na demu utahitaji kumtunza, kumlipia bills zake ikiwa ni pamoja na kulipia Kodi nyumba anayoishi.

Lakini unaweza ukawa sio mzinzi, ukapata Maisha mazuri ndipo uwe mzinzi.
Hivyo ukiona MTU amefanikiwa na hapohapo ni mzinzi basi jua ameanza uzinzi Baada ya mafanikio.

Huwezi ukatoka familia Maskini alafu ukawa mzinzi kisha uje kuwa na Maisha mazuri
 
Back
Top Bottom