Kama Wakenya wameweza, sisi tunashindwa kwenda kujifunza kwao?

Chai hii! Walikuja lini SUA kujifunza kilimo cha kisasa? Acha uongo sema walikuja kutuelekeza namna ya kufundisha kilimo.
Ndio shida ya watanzania wao wanafanya kilimo cha kisasa ila mafunzo na mbegu walikuja kuyapata SUA mbona tunapenda kujidharau hivyo waafrika mbona Vladimir Putin alikuja udsm ina maana vyuo huko duniani viliisha marais wengi wa east Africa wamesoma udsm hivi watanzania nani alituroga fuatilia kitu kabla hujabisha au kukoment itakusaidi yaani ukikuta kitu kama hujui Google kwanza usibishe usitumie hyo device kuangalia pornography tu nonsense.
 
Noted🙏
 
Ongezea maelezo kidogo hapo kwa Putin! Ilikuwaje?
 
Hii nchi mpaka inaumiza. Kuwa tu na bandari hii nchi ilifaa kuwa miongoni mwa nchi tajiri duniani. Lakini haijabahatika kupata watu sahihi.
 
Ongezea maelezo kidogo hapo kwa Putin! Ilikuwaje?
Sikia kwanza fanya mpango tuandae events ya wadau wanaosoma vitabu nimeona mijitu ni mijinga sana humu kazi yao kubisha tu kila wanatumia device kuangalia videos za gigi na uwoya hebu fanya jambo tuokoe kizazi kijacho maana hichi kilichopo tushakipoteza tayari.
 
Mkuu kuna Mbunge wa Uganda amesema itungwe sheria masikini wachapwe ili wajielewe wawe na maisha bora, unajiuliza yeye familia yake wote matajiri au amewapa hizo hela alizoiba za miradi

Hakuna watu wanafiki kama wanasiasa
Kavimbiwa Kodi za wananchi
 
Tuna mlolongo wa export permit kibao na ndio zinazokwamisha wakulima wa Kati wasipeleke mazao nje ya nchi.

Wakulima na wafanyabiashara hata kama mitaji ni midogo serikali kupitia Export Promotion Zone na Benki ya kilimo wangeruhusu Watu Wawezeshe kutumia Letter of Credit kuwasaidia wafanye export ya bidhaa zao
 
Equity na KCB Bank kitambo wanatoa Letter of Credit na collateral management. Mtu akiwa na mzigo wake umeandaliwa vizuri anaenda bank mzigo unakuwa Chini ya Collateral akitaka ku export anafanya process zote za export huku Bank ikihudumia ila mwisho wa siku original documents kama Bill of Lading, Packing List,Quality Certificate,Certificate of Origin,Export permit zinakabidhiwa Benki na wanawekeana condition au mkataba baada ya siku 60 ukilipa pesa documents zote utakabidhiwa na mzigo unakuwa umefika nchi husika na unauzwa.
 
Umeongea la maana sana na ukweli mtupu, tunasema ooh kwani wana akili kutushinda hapana bali mtu lazima uwe na mtaji wa kutosha na ujue biashara vizuri na pia wanaanzia mbali sana mpaka kuja kufika hapo

Waswahili tunalawama sana na kutaka short cut tu
Kaiba hela za umma anataka afanye kitu maisha yake hana hata idea nacho,
Mwingine kapata hela kidogo anadanganywa na bank manager aombe mkopo ataupitisha ale 10% yake jamaa anaingia mkenge na kuchukua mkopo say 200m
Anashusha mjengo wilayani au mkoani nyingine biashara asiyoijua mradi kamuona Juma amefanya

Wakenya wamejifunza na kuingia field miaka namjua mama mmoja analeta biadhaa tz na nchi za jirani
Anashusha Mombasa port containers mpaka 20 ni tajiri sana mama huyo na very honest ana msaada sana
Sasa sisi humu unamkuta mtengeneza nywele tu
 
✅🙏
 

Mwambie hata VietNam walikuja Mtwara wakajifunza kilimo cha Korosho, wakabeba na miche pamoja na mbegu. Sasa hivi wao ndiyo wanatoa korosho bora kabisa duniani hata hizi za Mtwara sasa haziuziki!!
 
Wale watu wako vizuri. Na wamejipanga vizuri.
 
Hizo bank za Kenya ziko vizuri mno. Hasa hiyo equity bank. Wamenyooka hawana konakona. Kila kitu kipo kwenye website yao.
Mfano
 
Bado tuna safari ndefu. Sisi tuko bize na uchawa na maV8
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…