Kama Wanakwaya wanavaa hivi basi si ajabu Wengine kuvaa pia!

Kama Wanakwaya wanavaa hivi basi si ajabu Wengine kuvaa pia!

Wacha kunisema vibaya nimeshaomba msamaha tayari nikasema nimekosea mimi hapa ni mgeni. Kwa hiyo nimejibu mada sio zangu.
Tupo p1 usijali! Karibu! Ila ile offer ya UK nasikitika nimeikosa nili fit vigezo ila ndio hivyo sipo uk[emoji1][emoji1][emoji1]
 
Bwanawee! Nawasikiaga tu! Nasikia wana adabu na heshima, pia lafudhi ya maongezi yao huniacha hoi kabisa[emoji2958]
Kweli mkuu Wana lafudhi tamu Sana na lugha ya mwambao hata kama mfukoni salio limepelea wala haujali hahaha
 
Around saa mbili na ushee asubuhi ya Leo, Nimeshuka zangu Chanika kituo kinaitwa Kwa Ngwale.

Natembea zangu mdogo mdogo naelekea eneo husika. Kwa mbali nasikia sauti za ibada hasa ulichukulia Leo ni siku ya ibada Kwa ndugu zetu Wakristo.

Mara paap nakaribia katika kanisa moja na huko ndani ibada zinaendelea, kama unavyojua macho hayana pazia, upande wa kushoto nafika usawa WA geti la Kanisa na geti lipo wazi, nashawishika kuangalia ndani ya Kanisa kwakuwa geti lipo wazi, kuna kondoo wengine wa bwana wapo ndani ya Kanisa na wengine wapo nje, huenda walikuwa wanasubiri misa ya pili.

Mara nawaona vijana wa kiume wamevaa Sare nzuri za bluu Kwa mwonekano wao ni rahisi kuwatambua kuwa hawa ni Wanakwaya, wamependeza Sana kwakweli, sasa mara upande mwingine nawaona mabinti nao wamevaa Sare za bluu vile vile, lakini jinsi zilivyoshonwa ndio zikanifanya nitahayari Kwa mwonekano wao.

Karibia wote Sare zao zimewabana na kuchora maumbile Yao ya kike, yaani hata Yule ambaye ana kalio dogo nalo limebanwa linaonekana, na hapo ndipo nilipopata mshangao.

Ni dhahir kabisa zilishonwa Kwa maelekezo maalumu, kwasababu isingekuwa hivyo basi huenda ingetookea Kwa mmoja au wawili Tu.

Je Uongozi WA Kanisa Una bariki hivi?

Je kiongozi wa kwaya anabariki hivi?

Je waumini wanaridhika na hili?

Unapata jawabu moja Tu,kuwa Hilo Jambo linachukuliwa kawaida na ndio maana hata waumini wanaenda na vimini makanisani!

Ni hayo Tu!
Mm ni mpiga vyombo kanisani, kuna mwana kwaya mmoja yani ananiponza sana na nguo zake
 
Kuna manzi mmoja niliwahi kumuuliza kua hivi kwanini wale mnaowaita masister na maaskofu hua wanajisitiri sana mda wote lakini ninyi waumini hasa wakike hua mnavaa vimini hadi kwenye ibada, hakuwahi nipatia jibu hadi leo hii. Ila all in all wao wana dini yao na sisi tuna dini yetu
 
Back
Top Bottom