Naam,
Hili niswali ambalo nishalijibu mara nyingi sana. Labda wewe tu hujanifuatilia.
Umeuliza hivi.
Mkuu Kiranga,nakuuliza swali hivi ukienda msituni ukaona nyumba imejengwa vizuri sana ina mfumo wa maji mzuri,mfumo wa umeme mzuri,kuna cctv camera na kuna mfumo wa choo mzuri tu halafu ukaambiwa hii nyumba haikujengwa ila imetokea tu,utakubali au utakataa?.ukijibu vyema tutaendelea
Hebu tulijadili hili swali kwa utafiti wa ndani kabisa, kinyume na ugoigoi wa mawazo ambao watu wanatumia kila siku.
Nataka tuende ngazi kwa ngazi.
Hoja ya msingi hapa ni ipi? Hoja ya msingini ni kwamba complex order haiwezi kutokea tu? Lazima itakuwana muumbaji?
Ukikubali hoja hii, utaona ili kuumba complex order,inatakiwa iwepo complex order iliyoumba, kwa hivyo na hiyo complex order nayo itahitaji muumbaji. Kwa mfano wako hapo, hiyo nyumba haiwezi kujiweka yenyewe, atakuwepo mtu kwa mfano aliyeiweka, na huyo mtu hawezi kuwa katokea mwenyewe (mtu ni complex order ya hali ya juu zaidi ya nyumba, tunaona complexity inaongezeka, na hivyo ulazima kwa kwamba mtu kaumbwa unaongezeka).
Tukirudi, kwa wanaosema mtu kaumbwa na Mungu, basi Mungu naye ni complex order, na hivyo, kwa ile kanuni yetu kwamba complex order haiwezi kutokea tu, lazima itakuwa imewekwa, tunaona na Mungu naye hawezi kutokea tu, lazima atakuwa kaumbwa, na yeye ana muumba wake, na muumba wake ana muumba wake, na muumba wake ana muumba wake.
Ad infinitum, ad nauseum.
Unaona kwamba, kamaulitaka kuuliza hiloswali kwania ya kuonesha lazima Mungu mjuziwa yote, mwenye uwezo wote, mwenye upendo wote, muumba ulimwengu na watu, yupo, hoja yakoinaonesha jibu tofauti.
Inaonesha Mungu huyo hayupo.