Wakristo waafrika wameshiba imani tangu kale hakuna cha kuwabadilisha mioyo yao warudi kwenye upagani. Kuhusu wazungu kupingana huko ni kukua kwa kanisa katika nyakati mbalimbali. Yapo madhehebu mengi tu ya kikristo yaliyoanzishwa na waafrika, hata Tanzania yapo, anza na PEFA, EAGT, KLPT, CAG, FPCT, ACT, Kanisa la ufufuo na uzima, ngurumo ya upako, arise and shine, mana, Efatha, FGBF, hayo ni kwa uchache tu yapo mengi ya kitanzania. Ukienda Kenya, uganda, south africa, nigeria, ghana, zimbabwe, zambia, malawi waafrika wanahudumia makanisa yao. Mind kwamba miaka hii wamisionari wazungu wameacha kuanzisha makanisa afrika wala hawasaidii labda mzungu mmoja mmoja ajitolee kusaidia ujenzi wa kanisa fulani kama sadaka au mchango wake lakini waafrika ndio wanaosimamia na kuendesha makanisa yao. ROMA/VATICAN ina kanisa lake dunia nzima na kiongozi mkuu wake ni papa na makao makuu ya kanisa hilo yapo vatican huko italia
Ujinga wako ni unapochanganya dini,madhebu na makanisa.
Tafuta maana ya dini,madhehebu na makanisa ndipo utajua hakuna dini au dhehebu lililoanzishwa na mwafrika bali "makanisa" ,unielewe!!
Dini kwa kizungu ni "religious";madhehebu ni "denomination, sect, custom";ma makanisa ni "churches".
Dini zilizopo Afrika nimekuwekea hapo juu Tradition/Panafricanism,ukiristo na uislam.
Madhehebu ya kikristo ni Adventism, Anabaptism, Anglicanism, Baptists, Lutheranism, Methodism, Moravianism, Quakerism, Pentecostalism, Plymouth Brethren, Reformed Christianity, na Waldensianism. na madhehebu ya kiislam ni Sunni, Shia, Whabbi, Salafi, Berelvi, Sufi na Deobandi (Madhehebu Saba) yoooote kwa uchache tu.
Wafia dini wengi hasa wanyakyusa ndiyo wameanzisha makanisa kwa wingi baada ya kigundua kuna wajinga wengi Afrika na ni ulaji.
Dini ya Panafricanism/Traditionalism/Africanism(Religion in Africa is multifaceted and has a major influence on art, culture and philosophy" ina madhehebu yake ambayo ni MAKABILA kulingana na MILA ZAO,hivyo naweza kusema dini za Waafrika ni makabila yao.
Maana halisi:-
DINI:-Dini (kutoka Kiarabu اﻟدﻴن, tamka: ad-din) inamaanisha jumla ya imani ya binadamu kadhaa pamoja na mafundisho wanayotoa kuhusu yale ambayo wanayazingatia ama kuyasadiki, yaani mambo ya roho, kama vile kuhusiana na Mungu, maisha na uumbaji.
DHEHEBU:-Madhehebu (kutoka Kiarabu مذهب madhhab) ni mafundisho, maadili na matendo ya ibada yaliyo ya msingi katika dini fulani.
KANISA:-ni jengo wanapokutanikia watu wenye imani moja kwaajili ya kuabudu(elewa ni kwa mtazamo wa Kiafrika na kiswahili na siyo wakizungu)