Kama wewe mtoto wa kiume, dada zako wakiolewa furahi sana, shukuru Mungu

Kwenye familia yetu tumezaliwa wavulana 6 wasichana 2, dada yetu mkubwa aliolewa mapema sana. Huyu mwingine wakati anaolewa mama alilia sana maana alimzoea sana na ndo alikua msaidizi wake mkubwa sana, "ajabu baba alifurahi sana" sikumwelewa baba alimaanisha nini mpaka baada ya miaka 6 alikuja kuniamba "KUOLEWA KWA DADA ZENU NDO SALAMA YA NDOA ZENU"

Leo baba amefariki nakuja kuyaona haya kwenye nyumba ya baba yangu mkubwa. Baada ya watoto wake wawili kuoa nyumba imejawa na vurugu dada(mawifi) wameanzisha vita ya hatari.

Maneno kila kukicha japo ya kila mtu kuishi kwake bado hawajaridhika. Bado wanaona wana haki na kaka zao wanaona mawifi wanafaidi nafasi yao yaani vurumai tupu.

Wangekua wameolewa haya mambo yangeoungua au yasiwepo kabisa.

Kijana kama dada zako wanataka kuolewa furahi sana kama unaweza suport fanya. Usije ukaweka kikwazo as long wamekubliana waache waoane. Hata ukiweka kikwazo kamwe huwezi kumtafutia mwanaume wa kumuoa.

Kuolewa wao ndo salama ya ndoa yako.
issue sio kuolewa, issue ni anaolewa kipindi gani.
 
Sasa unaogopa dini? au unogopa wanadamu??
Mwenye dini anamwona anachokifanya,yeye anaogopa wanadamu...Kati ya majibu nayaona ya kipuzi na kinafiki ni "Dini linakataa" lakini kuwa na mchepuko dini linakubali ?,kabla ya dini watu walioa kimila Bora uoe kuliko kuwa na mchepuko.
 
Unaanzaje kumwambia dadako atafute bwana? Kauli ngumu sana hiyo ataona unamfukuza..akipata shukuru sana
Kinachonikera wanao mdeti mkuu ndio kero angekuwa na mmoja angalau unamjua huyu Shem, Sasa yeye ni wa kubadilishabadilisha.
 
Ni kweli dada zako wakiolewa ni heshma kubwa kwa familia. Mimi niko pekee yangu wa kiume dada zangu wote walisha olewa tulifurahi sana aisee hamna aibu hata moja!
Aibu kivipi jmn[emoji25]
 
Kwenye familia yetu tumezaliwa wavulana 6 wasichana 2, dada yetu mkubwa aliolewa mapema sana. Huyu mwingine wakati anaolewa mama alilia sana maana alimzoea sana na ndo alikua msaidizi wake mkubwa sana, "ajabu baba alifurahi sana" sikumwelewa baba alimaanisha nini mpaka baada ya miaka 6 alikuja kuniamba "KUOLEWA KWA DADA ZENU NDO SALAMA YA NDOA ZENU"

Leo baba amefariki nakuja kuyaona haya kwenye nyumba ya baba yangu mkubwa. Baada ya watoto wake wawili kuoa nyumba imejawa na vurugu dada(mawifi) wameanzisha vita ya hatari.

Maneno kila kukicha japo ya kila mtu kuishi kwake bado hawajaridhika. Bado wanaona wana haki na kaka zao wanaona mawifi wanafaidi nafasi yao yaani vurumai tupu.

Wangekua wameolewa haya mambo yangeoungua au yasiwepo kabisa.

Kijana kama dada zako wanataka kuolewa furahi sana kama unaweza suport fanya. Usije ukaweka kikwazo as long wamekubliana waache waoane. Hata ukiweka kikwazo kamwe huwezi kumtafutia mwanaume wa kumuoa.

Kuolewa wao ndo salama ya ndoa yako.
Chanzo nii malezi mabovu ya kuwalea hao watoto wa kike na wala msiseme kuwa nature ya mawifi wakorofi huu ni uongo.

Kama mzee wako hakuwapa msingi wa kuwalea watoto wa kike katika maadili mema na adabu na heshima kwa wengine basi unaweza kuwa sahihi.

Lakini solution bi kurekebisha tabia tokea mwanzo,sio kukimbia jambo hili,kila siku mtalalamika humu
 
Back
Top Bottom