Huyu naye kapata passport kaanza kuona wasio na passport ni maskini, achana na passport kuna watu wana passport tangu 2005 - 2010 huko na wapo US, UK, Canada etc, na nauli tu ya kurudi bongo kusalimia ni mtihani unawaweka kundi gani!?,na kuna vijana chini ya miaka 35 wapo Simanjiro, Sengerema, Namtumbo, Simiyu, etc,wana maduka ya spare za pikipiki,magari, wengine wana mbuzi na ng'ombe zaidi ya 200 na hawana habari na mambo ya passport Wala kusafiri na wanaingiza ela chafu kila siku unawaweka kundi gani!??, nimegundua watu wengi wanaojionaga wajanja sana huwa ndo wajinga. Nahisi umepata passport leo au wiki iliyopita, na nina uhakika huna exposure ya aina yoyote. Nyie ndio watu ukisafiri kidogo miezi 6 tu, ukirudi unaona ambao hawajawahi kusafiri wote wajinga umewazidi kila kitu.