Kama wewe si mshirikina na huendekezi imani hizo, jipongeze sana!

Kuna kitu huwa nakiwaza sana unakuta viongozi wanaapa kwa biblia na vitabu vya dini , ila wanaiba na kukiuka kiapo, ebu fikiria wangekua wanaapa viapo vya asili kama kulambishwa asili , au kiapo cha damu ingekuaje🤔
Hakuna ambae angefanya ujinga... wote wangenyooka maana ukienda kinyume ni kifo shwaaaa😆😆😆😆
 
Wafuata mila na desturi za mataifa sasa... pure African hatuachi kufanya matambiko it's our culture as long as hatuui wala kuvunja sheria za kinchi then we are good.
Hakika mkuu, mambo ya kufuata imani za watawala wa zamani kwenye bara letu na kuziita ni dini takatifu huo ni utumwa kifikra na kiimani, wacha tuishi kivyetu piga tambiko mkuu, hayo ndiyo mambo yetu waafrika.
 
Wanaojionesha kwa watu kuwa ni watakatifu na hawafanyi ushirikina hao ndiyo wazee wa kazi 😂😂😂
 
Hakika mkuu, mambo ya kufuata imani za watawala wa zamani kwenye bara letu na kuziita ni dini takatifu huo ni utumwa kifikra na kiimani, wacha tuishi kivyetu piga tambiko mkuu, hayo ndiyo mambo yetu waafrika.
Waache waendelee kubaki utumwani ila mimi sitawahi acha mila na desturi zilizoachwa na mababu zetu.
 
Kuna watu huwaambii kitu kuhusu uchawi na ukisema nyumbani hatuamini ujinga huu hakubali kabisa
Naona mpaka baadhi ya watu wanaoheshimika katika society wana chale vifuani
Wanahangaika sana na kutwa wanatusumbua kwa kutuomba hela
Si wakaombe kwa hao waganga njaa
 
Kwanini mtu mwenye chale akimbiwe na sio kuombewa akatoka kwenye hilo giza?
Naona umemalizia vibaya
Kuombewa na kutoka huko ni utashi wa mtu mwenyewe huwezi mlazimisha, watumishi wa Mungu kila siku wanawaalika watu kwenye ibada za kufunguliwa.
 
Imani za mababu zetu unaita uchawi? tuombe radhi tafadhali
 
Hamna mwenye kufuata Dini ya RC asie mshirikina kimawazo na kivitendo. .. beliefs zao nyingi ni Dogma hazina logic/mantiki au reasoning.
Nonsense!!
 
Hamna mwenye kufuata Dini ya RC asie mshirikina kimawazo na kivitendo. .. beliefs zao nyingi ni Dogma hazina logic/mantiki au reasoning.
yaani ushasema belief halafu unataka iwe logic, upo sawa kweli wewe!?
 
Chale ni Sawa na Hizo Ndui(Modified Chale)
 
Hamna mwenye kufuata Dini ya RC asie mshirikina kimawazo na kivitendo. .. beliefs zao nyingi ni Dogma hazina logic/mantiki au reasoning.
Mimi nataka niingie huko.Nipe mifano ya hizo imani potofu nipige rivazi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…