Uchaguzi 2020 Kama wewe sio dhaifu kwanini utafute kupendelewa?

Uchaguzi 2020 Kama wewe sio dhaifu kwanini utafute kupendelewa?

MTU DHAIFU HUTAFUTA UPENDELEO; JE LISU ANAPAMBANA NA MTU DHAIFU?

Na, Robert Heriel
Watu Dhaifu hutafuta kupendelewa. Lakini wanajijua wazi kabisa uwezo ni mdogo bila hila, njama na figisu figisu.

1. Kwa Mara ya kwanza wakati Magufuli anagombea ubunge (miaka ya 1990s), alikula mweleka mbaya uliomfanya apoteze pambano. Kabla ya awamu nyingine ya uchaguzi kufika, serikali iliamua kuligawanya jimbo hilo ili kumpa ahueni Magufuli. Kwa hiyo, Magufuli aliikuja kuibuka baada ya kumegewa jimbo kutoka lile la mpinzani wake (Mbeleko ilitumika = hulka ya uanamke).
2. Mwaka 2015, CCM walikuja na njama za kumletea figisu ili Tundu Lissu ashindwe uchaguzi, lakini mwanaume alipambana na kisha kuibuka kidedea dhidi ya mabedui "CCM" (Ushujaa wa mapambano = uanaume).
 
Mbona dhaifu yuko wazi kwenye uzi anajipendelea yeye tuu
 
Yule ambaye akiguswa anakimbilia polisi ndo dhaifu
Je nan huyo?
 
Mtu dhaifu baada ya kupendelewa ni lazima aanze maisha ya Uongo, ulaghai na utapeli. Watu wote waliopendelewa huwa ndio mwanzo wa kutapeli na kulaghai watu ili kuwafanya waone ni kweli anastahili ushindi.
Mtu dhaifu hapendi ushindani, hata ndani ya chama.
Kumbuka figisu walizofanyiwa makatibu wakuu wastaafu, ikiwa njia ya kuondoa kupingwa.
Uteuzi wa mgombea urais ndani ya chama...

Mtu dhaifu hupenda kujionyesha yeye ni jasiri kwa vitendo anavyofanya kulaghai watu.
Rejea misemo ya 'Mabeberu' ilitokea wapi wakati huu. Mabeberu tulishawatwisha vilago nyakati za Mwalimu

Mtu dhaifu hupenda sana kujifananisha na watu jasiri, huku akijua hana sifa hata chembe za kuwasogelea watu hao.
Mfano - 'Wanyonge' imelazimu waibuliwe wakati huu ili watumike kama kinga ya kutafuta sifa hizo, hata kama wanyonge wenyewe hawajulikani ni akina nani.

Mtu dhaifu anapowekwa kwenye madaraka makubwa hutumia vyombo vya taifa alivyokabidhiwa na kuvihodhi kana kwamba ni vyake.
Anavitumia kukandamiza wote majasiri wanaokata uonevu wake.

Mtu dhaifu hukandamiza haki za wengine na hujifanyia mambo yake bila kufuata taratibu au sheria zilizopo kwa sababu anajua kwa udhaifu alionao hawezi kushawishi watu jasiri wakubali mambo anayotaka kuyafanya.

Naunga mkono mada.

Mtu dhaifu hununua haki. Atajifanya mchukia rushwa huku yeye ndie mtoa rushwa mkubwa. Mtu anatembea na vitita vya manoti kwenye magari na kuwagawia watu bila mpangilio wowote.

Mtu dhaifu, angalia tu misururu ya ulinzi anaopewa. Mwalimu alitaifisha mali za 'mabeberu', lakini hakulazimika kuweka ulinzi wa mitutu ya bunduki ikimtangulia mbele.

Mtu dhaifu hapendi kabisa ushindani, ndio maana juhudi kubwa zilifanyika kuua upinzani, ikiwa ni pamoja na kununua mamluki. Mtu shupavu hupambana, haogopi kukabiri ushindani
 
MTU DHAIFU HUTAFUTA UPENDELEO; JE LISU ANAPAMBANA NA MTU DHAIFU?

Na, Robert Heriel

Kikawaida watu dhaifu hutafuta kupendelewa, hutafuta dezo kwa watu. Pia kikawaida watu dhaifu ndio hupewa upendeleo na huukubali huo upendeleo kwa kuwa wanajua hawastahili.

Hii ni tofauti na mtu hodari. Mtu hodari hapendi kupendelewa, hapendi dezo, na wala hatafuti upendeleo kwani anajiamini kuwa yeye ni hodari, anauwezo, na ni mahiri katika jambo fulani hivyo anastahili.

Tulipokuwa wadogo ndani ya familia, hasa yenye watoto kuanzia wawili wanaokaribiana. Ni kawaida kuona yule mdogo(dhaifu) akiwa mchokozi, na hata ikitokea wakipigana mdogo anajua wazi kabisa wazazi(hasa Mama) atamtetea yeye. Hata kwenye chakula au zawaid ni kawaida mdogo(dhaifu) kupewa upendeleo maalumu na wazazi. Hiii ni kumfanya mtoto aliyemdogo kujisikia vyema.

Mfano wa pili;
Wale tuliosoma tutakubaliana kuwa, wanafunzi wengi wanaotafuta kuvujishiwa mitihani na waalimu ni wale wanafunzi dhaifu. Hata mwalimu anapovujisha mtihani hufanya hivyo kwa kujua wazi kuwa wanafunzi wake ni vilaza, dhaifu, hawajajiandaa vyakutoha. Hivyo huwapa upendeleo wa kuwaonyesha mtihani kabla ya muda wa mtihani kufika.

Kwa asilimia 90% Upendeleo huvunja haki. Watu wote waliopendelewa walivunja haki za wengine. Kupendelewa ni matokeo ya kutokujiamini, kudharauliwa, kutokustahili.

Hata Makazini wale wote wanaotafuta upendeleo wengi wao hawastahili, sio mahiri, hawajiamini, na wengi ni wapenda Rushwa. Hii huwafanya kujipendekeza kwa Boss ili kupewa upendeleo maalumu.

Watu hodari na mahiri huwa hawatafuti kupendelewa. Wanajua yakuwa wao ni bora. Wanajua kuwa wao wanajua kupambana katika mazingira yoyote yale bila kujali. Hawana muda wa kutumia uhalifu, uovu, hila au njama kujitangaza au kuhitaji kukubalika.

Kwenye michezo, hasa mpira, ni kawaida timu dhaifu kuomba upendeleo kwa Refa. Hii husababisha kumnunua Refa na wale Kamisaa. Timu inayojiamini,bora na mahiri haiwezi kutafuta upendeleo kwa refa.

Mtu bora hujisikia aibu pale anapopendelewa. Mtu hodari hujisikia kaabishwa pale anapohisi anapendelewa yaani hashindi kihalali, yaani hana uwezo wa kushinda kulingana na sheria za mchezo, bali hila, njama, figisu figisu ndizo zitamfanya ashinde.

Lakini Mtu dhaifu huchekelea pale anapopendelewa, anaona ni kawaida kufanya hila au njama, au figisu figisu ili kutimiza ushindi bandia.

Mtu dhaifu baada ya kupendelewa ni lazima aanze maisha ya Uongo, ulaghai na utapeli. Watu wote waliopendelewa huwa ndio mwanzo wa kutapeli na kulaghai watu ili kuwafanya waone ni kweli anastahili ushindi.

Tundu Lisu ni Hodari, hahitaji upendeleo(Hila, njama, Figisu Figisu) Ili ashinde. Watu kama Tundu Lisu nilishasemaga ni heavy Weight katika mapambano. Ni shujaa kama Goliath, anauzoefu wa vita, sio kama Daudi ambaye alipewa upendeleo na Mungu kwenye pambano lake na Goliath.

Watu hodari, mashujaa ndio hufanyiwa hila, njama, figisu Figisu ili washindwe. Huwezi mfanyia Figisu Figisu mtu dhaifu wakati unajua hana uwezo wa kukushinda. Na huwezi mpendelea mtu ambaye unauhakika kabisa anauwezo wa kushinda.

Washindi hawapewagi upendeleo, bali huwekewa hila, njama, Figisu Figisu ili wasishinde.

Sisemi kuwa Lisu hana madhaifu mengine, Hasha! Lisu ni mwanadamu kama wanadamu wengine. Lakini itoshe kusema kuwa anapambana na Mtu dhaifu wakati yeye ni shujaa.

Kama wangekuwa wanalingana uzani. Basi mmoja asingependelewa. Na kama mpambanaji anayepambana na Lisu angekuwa anajiamini angesema kwa ushujaa kabisa hivi: , nataka nipigane naye kavu kavu, huyu hanishindi kwa vyovyote. Lakini udhaifu ndio hupelekea mtu kutumia silaha.

Hujawahi ona hata kwenye vita wanapokutana wababe, basi utaona wote wanatupa silaha, wanasema tupigana kavu kavu kama unajiamini. Na kweli wote wanatupa silaha na ngumi zinaanza kuchapwa. Mpaka kidume apatikane.

Hivi ni kweli Tundu Lisu ni hodari kiasi hiki mpaka apatiwe nafasi ya kuonyesha uwezo wake na ushujaa wake?
Unajua Lisu anapambana Kavu Kavu na mtu anayetumia silaha(Hila, njama, Figisu Figisu) ambapo ni kinyume na mchezo wa mapambano.

Ni sawa na shuleni, mwanafunzi kipanga ambaye hajavujishiwa mtihani afanye mtihani na mwanafunzi aliyevujishiwa mtihani. Hata kama mwanafunzi aliyevujishiwa mtihani atafaulu lakini bado atakuwa ni kilaza tuu na yeye mwenyewe anajua hivyo.

Watu Dhaifu hutafuta kupendelewa. Lakini wanajijua wazi kabisa uwezo ni mdogo bila hila, njama na figisu figisu.

Makala hii inaweza kutumika katika nyanja zote za maisha. Nafahamu hata hapo ulipo huenda unapambana na mtu unayemuweza kabisa lakini anapendelewa, iwe ni ofisini, kwenye biashara, shuleni, chuoni, mpirani, masumbwi n.k

KUMBUKA: Tundu Lisu ametumika kama kiwakilishi cha watu majasiri, hodari, shujaa na mahiri. Huenda ni wewe au mtu mwingine.

Mtu dhaifu ametumika kama kiwakilishi cha watu wote mnaopenda kupendelewa kutokana na udhaifu wenu wa kuwa na uwezo mdogo.

Swali Muhimu:
Kama wewe sio dhaifu kwani utafute kupendelewa?

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300

ukitaka kujua mtu ni dhaifu unatakiwa kumshinda sio kuongea! tatizo mnaongea sana ni kama mmamsaidia kupiga kampeni uyo mdada wenu sjui, mshindeni na tactics zake zote mmshinde, izi kelele waachie wanataka kudanga
 
Mtu dhaifu hapendi ushindani, hata ndani ya chama.
Kumbuka figisu walizofanyiwa makatibu wakuu wastaafu, ikiwa njia ya kuondoa kupingwa.
Uteuzi wa mgombea urais ndani ya chama...

Mtu dhaifu hupenda kujionyesha yeye ni jasiri kwa vitendo anavyofanya kulaghai watu.
Rejea misemo ya 'Mabeberu' ilitokea wapi wakati huu. Mabeberu tulishawatwisha vilago nyakati za Mwalimu

Mtu dhaifu hupenda sana kujifananisha na watu jasiri, huku akijua hana sifa hata chembe za kuwasogelea watu hao.
Mfano - 'Wanyonge' imelazimu waibuliwe wakati huu ili watumike kama kinga ya kutafuta sifa hizo, hata kama wanyonge wenyewe hawajulikani ni akina nani.

Mtu dhaifu anapowekwa kwenye madaraka makubwa hutumia vyombo vya taifa alivyokabidhiwa na kuvihodhi kana kwamba ni vyake.
Anavitumia kukandamiza wote majasiri wanaokata uonevu wake.

Mtu dhaifu hukandamiza haki za wengine na hujifanyia mambo yake bila kufuata taratibu au sheria zilizopo kwa sababu anajua kwa udhaifu alionao hawezi kushawishi watu jasiri wakubali mambo anayotaka kuyafanya.

Naunga mkono mada.

Mtu dhaifu hununua haki. Atajifanya mchukia rushwa huku yeye ndie mtoa rushwa mkubwa. Mtu anatembea na vitita vya manoti kwenye magari na kuwagawia watu bila mpangilio wowote.

Mtu dhaifu, angalia tu misururu ya ulinzi anaopewa. Mwalimu alitaifisha mali za 'mabeberu', lakini hakulazimika kuweka ulinzi wa mitutu ya bunduki ikimtangulia mbele.

Mtu dhaifu hapendi kabisa ushindani, ndio maana juhudi kubwa zilifanyika kuua upinzani, ikiwa ni pamoja na kununua mamluki. Mtu shupavu hupambana, haogopi kukabiri ushindani

Je mbowe anataka changamoto kwenye uenyekiti wake? je ni dhaifu?
 
Back
Top Bottom