Uchaguzi 2020 Kama wewe sio dhaifu kwanini utafute kupendelewa?

MTU DHAIFU HUTAFUTA UPENDELEO; JE LISU ANAPAMBANA NA MTU DHAIFU?

Na, Robert Heriel
Watu Dhaifu hutafuta kupendelewa. Lakini wanajijua wazi kabisa uwezo ni mdogo bila hila, njama na figisu figisu.

1. Kwa Mara ya kwanza wakati Magufuli anagombea ubunge (miaka ya 1990s), alikula mweleka mbaya uliomfanya apoteze pambano. Kabla ya awamu nyingine ya uchaguzi kufika, serikali iliamua kuligawanya jimbo hilo ili kumpa ahueni Magufuli. Kwa hiyo, Magufuli aliikuja kuibuka baada ya kumegewa jimbo kutoka lile la mpinzani wake (Mbeleko ilitumika = hulka ya uanamke).
2. Mwaka 2015, CCM walikuja na njama za kumletea figisu ili Tundu Lissu ashindwe uchaguzi, lakini mwanaume alipambana na kisha kuibuka kidedea dhidi ya mabedui "CCM" (Ushujaa wa mapambano = uanaume).
 
Mbona dhaifu yuko wazi kwenye uzi anajipendelea yeye tuu
 
Yule ambaye akiguswa anakimbilia polisi ndo dhaifu
Je nan huyo?
 
Dhaifu ni yule Msaliti Nchi kutoka ubeligiji
 
Mtu dhaifu baada ya kupendelewa ni lazima aanze maisha ya Uongo, ulaghai na utapeli. Watu wote waliopendelewa huwa ndio mwanzo wa kutapeli na kulaghai watu ili kuwafanya waone ni kweli anastahili ushindi.
Mtu dhaifu hapendi ushindani, hata ndani ya chama.
Kumbuka figisu walizofanyiwa makatibu wakuu wastaafu, ikiwa njia ya kuondoa kupingwa.
Uteuzi wa mgombea urais ndani ya chama...

Mtu dhaifu hupenda kujionyesha yeye ni jasiri kwa vitendo anavyofanya kulaghai watu.
Rejea misemo ya 'Mabeberu' ilitokea wapi wakati huu. Mabeberu tulishawatwisha vilago nyakati za Mwalimu

Mtu dhaifu hupenda sana kujifananisha na watu jasiri, huku akijua hana sifa hata chembe za kuwasogelea watu hao.
Mfano - 'Wanyonge' imelazimu waibuliwe wakati huu ili watumike kama kinga ya kutafuta sifa hizo, hata kama wanyonge wenyewe hawajulikani ni akina nani.

Mtu dhaifu anapowekwa kwenye madaraka makubwa hutumia vyombo vya taifa alivyokabidhiwa na kuvihodhi kana kwamba ni vyake.
Anavitumia kukandamiza wote majasiri wanaokata uonevu wake.

Mtu dhaifu hukandamiza haki za wengine na hujifanyia mambo yake bila kufuata taratibu au sheria zilizopo kwa sababu anajua kwa udhaifu alionao hawezi kushawishi watu jasiri wakubali mambo anayotaka kuyafanya.

Naunga mkono mada.

Mtu dhaifu hununua haki. Atajifanya mchukia rushwa huku yeye ndie mtoa rushwa mkubwa. Mtu anatembea na vitita vya manoti kwenye magari na kuwagawia watu bila mpangilio wowote.

Mtu dhaifu, angalia tu misururu ya ulinzi anaopewa. Mwalimu alitaifisha mali za 'mabeberu', lakini hakulazimika kuweka ulinzi wa mitutu ya bunduki ikimtangulia mbele.

Mtu dhaifu hapendi kabisa ushindani, ndio maana juhudi kubwa zilifanyika kuua upinzani, ikiwa ni pamoja na kununua mamluki. Mtu shupavu hupambana, haogopi kukabiri ushindani
 

ukitaka kujua mtu ni dhaifu unatakiwa kumshinda sio kuongea! tatizo mnaongea sana ni kama mmamsaidia kupiga kampeni uyo mdada wenu sjui, mshindeni na tactics zake zote mmshinde, izi kelele waachie wanataka kudanga
 

Je mbowe anataka changamoto kwenye uenyekiti wake? je ni dhaifu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…