Kama wewe sio Freemason basi hujui chochote kuhusu Mungu wala ulimwengu

Hizi mambo huwa zipo deep sana.
Ngoja nisikilize nondo za wakuu
 
Biblia inasema Mungu ni Roho na imewapasa kumuabudu katika Roho na kweli. Yohana 4 mstari 24.Sasa swala la wewe kutaka kujua Mungu kama yupo kuna kanuni zake za kufuata than utamuona. Ntafute ntakusadia bure na hakika utamuona
 
Kwa nini unauliza maagizo ya nani? Kwa nini swali liwe nani na siyo nini?

Huoni kwamba kwa kuuliza swali la nani tayari ushalenga kwenye jibu lako ulilo nalo mfukoni?

Unaweza kuthibitisha Yesu alikuja kwa maagizo ya yeyote?
Basi ni seme kwa nn alikuja
 
Weka kitabu cha Moral and Dogma humu halafu uanze kueleza ugunduzi wako. Kwa kusema mungu wa Kabili wanaojua uongo wa secret society unamaani Jahbullon. Au Sataniel mungu wa giza na si Jehova. Acha stori za utafiti hewa thibitisha kuwa freemason ni wazuri kwa kuweka maandiko yao
 
Alikuja kufany nn mkuu na kwa sababu gani alikuja?
Watu wote wanakuja duniani kuishi.

Kwa sababu baba na mama zao walikutana kimwili na kufanya mimba itungwe.

Na Yesu naye, kama aliishi. Ni hivyo hivyo.

Mengine mbwembwe tu za kujiongeza.

Nimeuliza kuthibitishiwa Mungu yupo hapa miaka na miaka, napewa hadithi tu, hakuna aliyethibitisha.
 
Basi ni seme kwa nn alikuja
Watu wote wanakuja duniani kuishi.

Kwa sababu baba na mama zao walikutana kimwili na kufanya mimba itungwe.

Na Yesu naye, kama aliishi. Ni hivyo hivyo.

Mengine mbwembwe tu za kujiongeza.

Nimeuliza kuthibitishiwa Mungu yupo hapa miaka na miaka, napewa hadithi tu, hakuna aliyethibitisha.
 
Biblia inasema Mungu ni Roho na imewapasa kumuabudu katika Roho na kweli. Yohana 4 mstari 24.Sasa swala la wewe kutaka kujua Mungu kama yupo kuna kanuni zake za kufuata than utamuona. Ntafute ntakusadia bure na hakika utamuona
Una hakika gani kwamba wewe ndiye utanisaidia mimi na si mimi ndiye nitakusaidia wewe?

Unaweza kuthibitoisha kwamba wewe ndiye utanisaidia mimi na si mimi ndiye nitakusaidia wewe?
 
Salama sana mkuu.

Natumaini na wewe salama.
Kwanini unatumaini..?
Unamtumainia nani...? MUNGU AU SHETANI
Nini kinachokufanya uwe na matumaini kwamba jamaa yupo salama...?
Huoni kama hili tumaini lako linamtumainia Mwenye Mamlaka na asieonekana..?
Kupitia hii sentensi yako, nimepata picha kwamba moyoni mwako unafahamu dhahiri kuna Mamlaka ya Mwenye Mamlaka.
 
Kwanza kabisa, kabla ya kwenda mbali sana, mtu anaposema "natumaini" unaelewa nini?

Unaweza ku define neno "tumaini"?

Swali hili ni muhimu, kwa sababu ili nikujibu swali lako vizuri, ni muhimu tukubaliane maana ya tumaini ni nini.

Vinginevyo, unaweza kuuliza kitu na mimi nikakujibu ambacho hujauliza. Jambo ambalo nakumbana nalo sana hapa JF.

Maana ya tumaini ni nini?
 
"Tumaini ni hali ya kutegemea jambo fulani liwe au litokee"

"Tumaini ni hali ya kuwa na tamaa au matarijio ya kitu fulani" kwa mujibu wa oxford dictionaries

Sasa hapa huoni kwamba unatumani kitu kutoka kwenye nguvu zisizo onekana ambazo ndizo sisi tunaziita nguvu za kiMungu??
 
Definition yako sina matatizo nayo sana.

But.

Your conclusion is a logical non sequitur.

Unaelewa logical non sequitur ni nini?
 
Definition yako sina matatizo nayo sana.

But.

Your conclusion is a logical non sequitur.

Unaelewa logical non sequitur ni nini?
Okay tuseme conclusion yangu ni invalid na haifati protocal za logic

Tuje kwako, kwann haukutumia logic kutambua kwamba jamaa atakuwa salama instead umetumia "tumaini"

Kipi kilichokufanya uwe na "tumaini" kuhusu Afya au hali ya jamaa
 
Kwanza hujanijibu kama umeelewa logical non sequitur ni nini. Sijui kama umejifunza ulipokosea katika logic ya assumption zako za mwanzo.

Nani kakwambia tumaini haliwezi kuwa katika msingi wa logic?
 
Logic ina pande mbili tu, TRUE au FALLACY/FALSE otherwise that is not logic
Kama ulikuwa unategemea logic kutambua hali ya jamaa usitetanguliza neno "natumaini" hili neno limetengua nadharia nzima ya logic

Ukitumani maana yake huna uhakika kama ni True au Fallacy/False bali una wish jamaa atakuwa kama ulivyotumani

Swali langu ni, nn chanzo cha tumaini lako??
Tumaini lako limeegemea kwenye kitu ganii?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…