Kama wewe sio Freemason basi hujui chochote kuhusu Mungu wala ulimwengu

sahizi mkuu una wafuasi wengi sana(atheist)

#sijui kama unalijua hilo?
Atheism ilikuwapo kabla sijazaliwa.
Hivyo mtu kuwa atheist si kuwa mfuasi wangu, kwa sababu sikuianzisha mimi, labda ni watu ambao tuna maoni sawa.

Kadiri watu wanavyozidi kuelimika, wanazidi kujua ukweli. Wanazidi kuhoji uongo wa wazi ulio katika dini.

Ndiyo maana kuna mrandano kati ya nchi za watu wenye elimu kubwa na atheism (northern Europe is an example) na nchi zenye elimu ndogo zina amini dini zaidi (Africa for example)

Sasa hata kwetu Africa watu wanavyozidi kusoma, wanapanua mawazo, wanakuwa freethinkers/ atheists.

Ni jambo rahisi sana kuliona.
 
Atheism ilikuwapo kabla sijazaliwa.
Hivyo mtu kuwa atheist si kuwa mfuasi wangu, labda ni watu ambao tuna maoni sawa.

Kadiri watu wanavyozidi kuelimika, wanazidi kujua ukweli.

Ndiyo maana kuna mrandano kati ya nchi za watu wenye elimu kubwa na atheism (northern Europe is an example) na nchi zenye elimu ndogo zina amini dini zaidi (Africa for example)

Sasa hata kwetu Aafrica watu wanavyozidi kusoma, wanapanua mawazo, wanakuwa freethinkers/ atheists.

Ni jambo rahisi sana kuliona.
Sijakataa ni kweli atheist walikuwepo enzi na enzi lakini kws wana JF ninao kutana nao huku mtaani na kuwauliza kuhusu swala lao la imani, wengi hujibu kwa sasa hawajihusishi na imani yeyote na chanzo cha wao kufumbuliwa macho ni wewe, mimi yule na wale (member wa hapa jukwaani umetu- inspire kwa kiasi kikubwa sana.

#long live Kiranga
 
Asante. Nashukuru sana kusikia hivyo.

Moja ya mambo niliyoyaona yaliyofanya atheism kuonekana ni kitu cha ajabu sana ni wengi wetu kukosa kujua vizuri lugha za watu wa nje, hususan Kiingereza.

Kwa kweli nimetafuta maandishi ya atheism katika Kiswahili, sijayapata. Kwa hiyo, kwa mtu ambaye hajasafiri nje ya Tanzania au hajajikita sana katika kusoma vitabu vya Kiingereza, hususan vitabu vya falsafa, kujua atheism kutoka maisha ya kila siku ya Kibongobongo ni nadra sana, labda baba awe profesa wa chuo anayefundisha mambo haya au msomi wa aina hiyo, na watu hawa ni wachache.

Hivyo, kwa kupitia JF na posts zangu za muda mrefu hapa, inawezekana kabisa nikawa ni mtu ambaye nimeandika kuhusu atheism kwa kirefu zaidi katika Kiswahili kuliko mwingine yeyote.

Ila, napenda kuonya jambo moja. Kukataa dini na kuwa atheist si tiketi ya kuishi bila moral compass, kwa kweli, mimi nimekataa dini kwa sababu nimeona dini ina a very low bar, na mimi kukataa dini naweza kujiwekea a higher bar kwenye kuishi in a moral way.

Kwa hivyo nisingependa kuona kuwa nachochea watu waache dini kuwa atheists halafu wakaacha kuishi kwa kusaidiana, kuelimishana, kuwa na huruma kwa wengine etc, within a reasonable limit.
 
Atheism ilikuwapo kabla sijazaliwa.
Hivyo mtu kuwa atheist si kuwa mfuasi wangu, kwa sababu sikuianzisha mimi, labda ni watu ambao tuna maoni sawa.

Kadiri watu wanavyozidi kuelimika, wanazidi kujua ukweli. Wanazidi kuhoji uongo wa wazi ulio katika dini.

Ndiyo maana kuna mrandano kati ya nchi za watu wenye elimu kubwa na atheism (northern Europe is an example) na nchi zenye elimu ndogo zina amini dini zaidi (Africa for example)

Sasa hata kwetu Africa watu wanavyozidi kusoma, wanapanua mawazo, wanakuwa freethinkers/ atheists.

Ni jambo rahisi sana kuliona.
Mkuu Kiranga naomba unipe tofauti kati ya atheism na luciferianism,kuna sehem nimesoma hawa luciferian hawaimani katika uwepo wa mungu wala miungu lakini wanaamini kwamba knowledge ni kitu pekee kitakachomukomboa binadamu ,the same as atheist
 
Ukiongea habari za Lucifer, ushaingia katika mkondo wa habari za hadithi za Mungu. Kwa sababu Lucifer katika narrative traditional ya Mungu, alikuwa malaika wa Mungu aliyeasi.

Luciferianism ni imani inayomtetea Lucifer, wanasema kwamba, Mungu alikuwa mchoyo wa elimu ndiyo maana alimkataza Adam kula tunda la ujuzi wa mema na mabaya.

Wanamuona Lucifer kama mkombozi aliyepingana na Mungu, kwa kutaka kumfungua macho Adam, ili Adam apate elimu ya kujua mema na mabaya awe kama Mungu.

Luciferianism si atheism, ni dini inayoamini Mungu tofauti tu, kama Waislamu wanavyoamini Allah na Wakristo wanavyoamini Jehovah, hawa wanaamini Lucifer ndiye Mungu, kwa hiyo si atheism.

Tatizo langu na habari hizi ni kwamba, zinarudi kule kule nilikokukataa kwenye hadithi za Biblia za Mungu na Adam.

Mimi sikubali Mungu yupo, sikubali Lucifer (ambaye ametoka kwa Mungu) yupo. Ile story ya Adam kuwa mtu wa kwanza ni hadithi , habari za Biblia nyingi zimeandikwa na kuwa edited na watu mara kibao.

Kwa hiyo, Luciferianism si atheism, atheism ni kusema Mungu hayupo, Luciferians wana Mungu wao, Mungu wao ni Lucifer, hivyo hao si atheists.
 
Mkuu unadhani dini zina umuhimu kwa kiasi chake au ni za kupuuza tu..? (Hasa hizi zinazofundisha habari za Mungu)
 
Shukurani,nimeelewa

Kwa nani? Kwa kiwango gani? Kwa lengo gani?

Ukiuliza "Mkuu, unadhani kujifunza kuhesabu 1,2,3 kuna umuhimu wake au ni jambo la kupuuza tu" swali lako linaweza kuwa na majibu tofauti kwa watu tofauti.

Kwa mtoto wa miaka mitano, kujifunza kuhesabu ni muhimu sana.

Lakini kwa Profesa wa hisabati, huyo kashapita kujifunza kuhesabu 1,2,3, anashughulika na mengine makubwa zaidi.

Dini zina umuhimu kujifunza. Usipojua dini hutajua misingi mikubwa ya historia, uchumi, tamaduni, sheria na kadhalika.

Mimi mpaka leo najifunza dini, pamoja na mengine. Hapa pembeni yangu nina vitabu kadhaa vya dini. Nasoma dini kama falsafa na historia.

Pembeni nina "How To Read The Bible: A Guide To Scriptures Then And Now" cha James L Kugel. Nina "The Reason For God: Belief In An Age of Skepticism" cha Mchungaji Timothy Keller. Nina "The Meaning Of The Holy Quran" cha Abdullah Yusuf Ali, ni Quran nzima na muongozo wa kuisoma na kuielewa. Nina The Dhammapada (Buddhism) The Bhagavad Gita (Hinduism) The Uppanishads (Hinduism).

Kusoma dini kunatajirisha "cultural intelligence" yako. Huwezi kwenda sehemu ya waumini wa dini unayoijua ukashangaa sana.

Na hata kama hukubaliani na dini, huwezi kuipinga kama huielewi. Hutakiwi kuipinga kabla ya kuisoma na kuielewa.

Unatakiwa kuisoma, kuielewa halafu kama hukubaliani nayo, baada ya kuisoma na kuielewa, ndiyo unaipinga.

Sasa, mimi naona kusoma dini ni muhimu, kama vile kusoma Shakespeare na Shaaban Robert kulivyo muhimu.
 
Asante. Nashukuru sana kusikia hivyo.

Moja ya mambo niliyoyaona yaliyofanya atheism kuonekana ni kitu cha ajabu sana ni wengi wetu kukosa kujua vizuri lugha za watu wa nje, hususan Kiingereza.

Kwa kweli nimetafuta maandishi ya atheism katika Kiswahili, sijayapata. Kwa hiyo, kwa mtu ambaye hajasafiri nje ya Tanzania au hajajikita sana katika kusoma vitabu vya Kiingereza, hususan vitabu vya falsafa, kujua atheism kutoka maisha ya kila siku ya Kibongobongo ni nadra sana, labda baba awe profesa wa chuo anayefundisha mambo haya au msomi wa aina hiyo, na watu hawa ni wachache.

Hivyo, kwa kupitia JF na posts zangu za muda mrefu hapa, inawezekana kabisa nikawa ni mtu ambaye nimeandika kuhusu atheism kwa kirefu zaidi katika Kiswahili kuliko mwingine yeyote.

Ila, napenda kuonya jambo moja. Kukataa dini na kuwa atheist si tiketi ya kuishi bila moral compass, kwa kweli, mimi nimekataa dini kwa sababu nimeona dini ina a very low bar, na mimi kukataa dini naweza kujiwekea a higher bar kwenye kuishi in a moral way.

Kwa hivyo nisingependa kuona kuwa nachochea watu waache dini kuwa atheists halafu wakaacha kuishi kwa kusaidiana, kuelimishana, kuwa na huruma kwa wengine etc, within a reasonable limit.
Perfect[emoji119]
 
Huyo Mungu anayehitaji watu kumtangaza ili wengine wamuelewe ni wa maboksi.

Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo na upendo wote angekuwepo, asingehitaji mtu kumtangaza ili aeleweke.
.
20190605_175324.gif
 
Alchemically ndio .Hata ukitaka God awe proved kwako " Anatomically" inawezekana pia..Anyways kuhusu uchawi " Go and tell ur biological father that I Likud of Jamii Forums has said that tomorrow he will die and on the day of his barrier there will be the heaviest rainfall ever" Fanya hivyo halafu uone kama baba ako mzazi ataishi zaidi ya hiyo kesho.
Mrejesho wa hii
 
Huyo Mungu anayehitaji watu kumtangaza ili wengine wamuelewe ni wa maboksi.

Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo na upendo wote angekuwepo, asingehitaji mtu kumtangaza ili aeleweke.
Na kuja kwa yesu je alikuja kumtangaza nani na kwa agizo LA nan?
 
Maandiko ya Yesu yamemtangaza Mungu ambaye hayupo. Kwa kutumia akili zake na mapokeo ya utamaduni wa jamii yake.

Kumtangaza Mungu si lazima awepo.

Gazeti la SANI limewatangaza Kipepe, Madenge, Lodi Lofa, Ndumilakuwili.

Wote hawapo hao. Ni fictional characters.

Aristablus Elvis Musiba alimtangaza Willy Gamba, kachero jasusi wa Kitanzania. Wa kutungwa, hayupo.

Kumtangaza fictional character hakumfanyi huyo fictional character awepo.

Mungu ni character katika hadithi ya kutungwa, hayupo.

Ndiyo maana mpaka leo nauliza wanaosema Mungu yupo wathibitishe yupo, wanashindwa.
 
Yesu alkuja kwa maagizo ya nan hujajibu mkuu
 
Back
Top Bottom