jmushi1
Platinum Member
- Nov 2, 2007
- 26,540
- 25,834
1.Freemasons wanafundishwa kuhusu Mungu aliye uumba ulimwengu na namna ya kuishi hapa duniani katika namna impendezayo yeye.Watu wa dini zote wangefundishwa kuhusu Mungu katika namna wanayo fundishwa Freemasons basi dunia ingekuwa sehemu nzuri sana ya kuishi.Mafundisho ya Freemasons kuhusu Mungu yanamchambua Mungu vizuri sana..
Hapa kuna utata...
Moja, Freemason hawawezi kukubali ujiunge nao hadi uwe unaamini uwepo wa higher power...Mungu yoyote tu uwe unaamini.
Mbili, wanaoingia humo ni mchanganyiko wa dini za tofauti. Mfano wakristo, waislam, budha, baniani nk. Na wote hao hawaamini Mungu mmoja, yet unasema “wanamchambua Mungu na kumwelezea vizuri, ni Mungu yupi huyo wanaomchambua? Wa waislam au wa baniani? Au ni Mungu wa Miungu wa dini zote? Huyo “Grand architecture”?
Mwishoni, siyo kweli kusema hawakubali uchawi. Lodges huwa zinashirikisha tamaduni nyingine za maeneo husika.