Kama yaliyoandikwa kwenye ufunuo yatatokea, tuna tabu sana!

Amen.

Kuna mambo yameandikwa pia kwenye Mathayo 24 yanatisha anasema mwandishi lingetokea pigo kubwa ole yetu tungetamani tusingezali ila kwa rehema zake huo wakati ulipitilizwa yaani ni kama waliuoforward usitokee.

Pia imeandikwa kwamba ili Yesu kristo arejee sharti injili ihubiriwe ulimwengu mzima, sharti yaani lazima hapo ndio ule mwisho utakuja.
 
Makanisa Saba
Nyota Saba
Vitasa Saba
Mihuri saba
Baragumu Saba
 
Njia na vitabu vya kufanya yote hayo vipo tatizo ni kuwa hatuna uchumi wa kufanya hayo yote.
 
Sasa hawa wanaoisambaza haraka haraka si ndio wanawahisha mwisho wa dunia.

Bora Wachina na wahindi waendelee kugoma
 
Yaliyoandikwa yote yatatokea kamwe Mungu hajawahi na hatosema uwongo. Una heri wewe kwa kusoma na kutafakari maneno haya ya Mungu, kama hujamwamini Yesu basi chukua hatua sasa hivi fanya sala ya toba na endelea kujifunza neno la Mungu, na ishi maisha matakatifu, na hata ukianguka dhambini tubu hapohapo. Iko hivi kuna uamsho wa mwisho mkubwa sana unakuja duniani ambapo watu wengi sana watamwamini Mungu na kutubu pindi ukiona hilo limetokea jua muda wowote Yesu atanyakua walio wake. Na baada ya unyakuo dhiki kuu ya miaka 7 itaanza ambapo mapigo makali sanaaa ya Mungu yatawapata wanadamu, na biblia iko wazi kabisa kuwa kama siku hizo zisingelifupishwa basi asingeokoka mtu yeyote. Ewe ndugu omba sana Mungu unyakuo usikuache maana ukibakia duniani aisee uwezekano wa kumrudia Mungu na kuvumilia mateso ni mdogo sana maana wengi sana watamkubali shetani ili angalau wapate nafuu ya maisha na kwa kukubali huko itakuwa rasmi wamekata tiketi ya kwenda jehanamu.
Barikiwa ndugu!!
 
Hivi vitabu vya dini vinatufundisha namna sahihi yakuishi katika kujaliana kuchukuliana, kusameheana, kupendana, kutokuchukiana,
Pia imetufundisha namna sahihi ya ufanyaji kazi kwa maarifa , uaminifu, ubora , hata kujituma Kwa bidii hizi ni kanuni za Mungu hasa ukitaka kufanikiwa kwenye kazi zako

Hata kuhusu malezi ya watoto Kuna muongozo pia Kwa hiyo hv vitabu vya dini ukisoma Kwa ufahamu utajifunza mengi sana

Ushindwe wewe tuu
 
Vitu kama hivi vipo ndani ya binadamu wala havihitaji vitabu vya mchongo... Mbona kuna nchi hazina hizi dini na maisha yao ni mazuri kuliko huku?
Tena hizi dini ndio zimeharibu utu wetu wa ndani hadi kufikia jamii 1 kujiona bora kuliko nyingine
 
Je akiwemo mmoja Tu Kati Yao aliye mkamilifu utaiangamiza dunia?
Hapana kwa ajili ya huyo mmoja sitaiangamiza🤗🤗🤗🤗🤗
Tunaringa na huo mstari!!
Ibrahim aliuliza hili swali akajibiwa hivyo lakini Kilitokea Nini pale sodoma na gomora.

Wema watakuwa wameshanyakuliwa mawinguni kumlaki Bwana Yesu.Wema watanyakuliwa ghafla bini vuuum.

Na hakutakuwa na janjajanja zikitokea yatatokea ya mke wake Rutu.
 
Vitu kama hivi vipo ndani ya binadamu wala havihitaji vitabu vya mchongo... Mbona kuna nchi hazina hizi dini na maisha yao ni mazuri kuliko huku?
Tena hizi dini ndio zimeharibu utu wetu wa ndani hadi kufikia jamii 1 kujiona bora kuliko nyingine
Nilichozungumzia ni kuwa sioni shida kwenye hivi vitabu labda shida iliyokuwepo namna vile tunavyotafsiri
ndio upelekea jamii Fulani kujiona Bora kuliko wengine hii ni tatizo ni kwetu, 🤔
 
Halafu hiyo adhabu ya milele ni kwamba unachomwa tu moto milele halafu hufi? au unachomwa unateketea? Hebu nielewesheni hapo.
 
Itakuwa balaa,mwenyezi Mungu atuepushie!
 
Barikiwa sana ndugu kwa maelezo mujarabu nashukuru sana kuwa miongoni wa wanaosoma maelezo haya Asante 🙏
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…