Kama yote

Kama yote

Lugha ina sarufi na fasihi sasa hii ni fasihi lugha inapambwa kama yote😋😋
 
Ushamba ni wewe kuona msemo au kitu fulani ni cha kishamba kwasababu wewe binafsi hukipendi. Huo msemo hata mimi nishauliza maana sielewi hio yote,zote kwenye sentensi inaleta maana gani ila siwezi kuwadharau wanaotumia.
Unamaanisha "wingi"..mfano kuna bia kama zote..hapa ni kwamba bia zipo za kumwaga..

Na sijui ni kwa nini watu wanakasirika au wanawaona wanaotumia hii misimu kuwa ni washamba wakati kila mwaka huwa kuna misimu mipya..
 
Ni upumbavu unaoanzishwa na kile kituo pendwa cha vijana,kiukweli hua napatwa na ukakasi juu ya usalama wa marinda ya baadhi yai watangazaji wao...
 
Mkuu yaani ni Yechu yechu tu namalizia bia yangu hapa wala haikatai mzuku ni mwingi fulu kama wote tu.
 
Ukisikia mtu anasema kama zote mkuuu kimbia ni sumu mbaya sana
 
Mimi bado nahangaika kujua maana ya "Kudamshi"
 
misemo mingine bwana " kwakweli sijawahi kujihusisha na misemo kama hiyo " huwa naona niujinga tu
 
Jamaa anatembea mwendo "kama wote" acheni lugha ipate misamiati mipya masuala ya kupangiana misamiati ni wendawazimu... Kilatini kilikufa kwasababu "kama zote" [emoji23][emoji23][emoji23] hizo
[emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Back
Top Bottom