Kamala Harris: “Mimi ni mwanasheria, Trump ni muhalifu aliyekutwa na hatia mahakamani”

Obama alifanya kosa moja tu...baada ya kupata ushindi mnono na kuchukua both houses aliamini angeweza kuwashawishi Republicans wafanye kazi pamoja, alikosea sana. Ni hapo udhaifu wake ulipoonekana wazi kwani wapinzani wake walikuwa na mipango tofauti, kumkwamisha.

Hakusikiliza ushauri wa watu wake na matokeo yake hakupata mafanikio yaliyotarajiwa na wapiga kura wake. Kosa hilo alilijutia baadaye but then it was too late kwani ilimsababishia kufanya vibaya kwenye mid terms ikiwa ni pamoja na kupata ushindi mdogo na kupoteza house na ndoto yake!

Hata hivyo chini ya Obama mafanikio aliyopata hayawezi kuwa ignored kama alivyobainisha hapo juu Mkuu jmushi1
 
Hilary Clinton alikuwa tishio kwa Trump, tena alikuwa na back up ya Mme wake Rais mstaafu Clinton na Obama, pia alikuwa maarufu kuliko Kamala lakini Trump alimgaragaza.
 
Well said.
 
100% Agreed
 
Unajua Tunatofautiana Kidogo sana, Mimi Namuomgelea Obama kama Obama Bila Kufanya Comparison na Trump..

Kwa sababu Ukimchukua Obama ukafanya Comparison na Trump Utamuona Obama ni Rais Bora sana Kuliko Trump on matter of everything...

Ni sawa Na kumchukua KIKWETE na kumfanyia Comparison Na Magufuli..

Ila ukimchukua Mmoja mmoja Utaona Mapungufu yao bila kufanya Comparison na mwingine..

But so Far Wote tunakubaliana Uongozi wa Trump ulikuwa Mbovu Kuliko wa Obama na wa kibaguzi pia..

Lakini kulingana na Hali ilivyo sasa, Nchi Haihitaji tena Sera za Obamalism.. ambazo Kamala Tunaona ana chembe chembe hizo za Sera hizo...
 
Huwezi kusema ni bora au siyo bora bila kulinganisha na mwingine.

Either ulimlinganishe na marais waliotoka Republican, au na marası kutoka chama chake cha Democratic.

Huwezi kusema siyo bora ama ni bora kwenye uchumi. Zaidi au chini ya nani?

Hapo tayari umeshakosea. Hakuna mantiki.

Lakini mimi nilidhani unazungumzia ubora wa Trump kwenye uchumi na ndiyo maana nikakuletea hizo facts.

Hapa wewe unazungumzia Kikwete na Maghufuli ambao wametokea chama kimoja cha ccm.

Sasa kama unataka tujadili mengine zaidi ya hoja ya uchumi ambayo uliileta hapo awali. Basi ni sawa tu. Lakini malizia moja kwanza then twende kwenye jingine. Mfano hayo unayoyasema kuhusu ubaguzi nk.

Mimi Trump nampenda kwenye issue moja tu ya kuwa kinyume na ushoga nk.

Kwingine ndo napishana naye sana.
 
Huyu mama akipita ushoga na usagaji itakuwa kipaumbele kwenye kila nchi inayoishabikia America
 
Hilary Clinton alikuwa tishio kwa Trump, tena alikuwa na back up ya Mme wake Rais mstaafu Clinton na Obama, pia alikuwa maarufu kuliko Kamala lakini Trump alimgaragaza.
Nawasikitikia sana baadhi ya Watanzania kama wewe mliojiaminisha kuwa mnajua kumbe hamjui kitu. Hujui siasa za Marekani na ni heri mngekaa kimya na kusoma maoni ya wanaojua ili angalau mjifunze.

Ushindi wa Trump mwaka 2016 uliwapa nafasi Wamarekani kumjua a proven and convicted felon. Hakuna namna Trump anaweza kushinda Urais tena kwani ustaarabu huendana na kutorudia kosa la awali.

Kwa Tanzania, mtu kama Trump anaonekana kama shujaa! Kwetu Rais ni mungu asiyegusika na ukimgusa umekufuru. Tunashindwa kuiheshimu na kuitetea hata hiyo Katiba tuliyoapa kuifuata na kuilinda.

Kukaa kimya huficha ujinga kuliko kuropoka hovyo na kujiumbua ulivyo mtupu kichwani, mnatia aibu. Kwa bahati mbaya zaidi idadi ya wajinga inazidi kuongezeka hapa nchini kwa kiwango cha kutisha.
 
Ushindi wa Trump mwaka 2016 uliwapa nafasi Wamarekani kumjua a proven and convicted felon. Hakuna namna Trump anaweza kushinda Urais tena kwani ustaarabu huendana na kutorudia kosa la awali.
Never say never......
 
We
Well said
 
Ok
 
Beberu likimgeukia asianze kulialia maana linatiririka facts tu lile. Further, lina a very clear vision about America he wants to build. Huyo mama zaidi ya zali sidhani kama ana la zaidi.
Umepigilia msuri kwenye kidonda jamaa lipo vyema sana sana hizo siasa uchwara za huyo maza zitamtokea puani maana li mwamba likianza kutema madini dunia yote husikiliza

Yeye (Haris) ajikite kwenye kuuza sera atalifanyia nini taifa akichaguliwa kuliko kutegemea mbeleke maana jamaa halichafukiki

Kama ni lihalifu imeshindikana nini kwenda kunyea debe? ...Ukweli ni kwamba hizo figisu zimeshagonga mwamba na hata raia wameshajua kuna figisu za kipumbavu

Itoshe kusema hakuna wa kumzuia Trump si Marekani yenyewe wala Iran
 
Nimegundua USA hawataki Rais mwanamke. Ni kama huku kwetu,ukweli hata sisi hatumtaki.
 
Hapa nadhani unazungumzia umuhimu wa “Battleground states”

Ziko sita kama sikosei. Mara zote “Battleground states” ndizo ambazo huamuwa mshindi wa urais na siyo popular votes peke yake. Nitaweka uzi wa “battleground states” ili tufuatilie nani anaongoza. Ambapo hadi usawa huu Trump yuko juu ya Harris. Hata hivyo Harris anapunguza “gap” kadri muda unavyokwenda.
 
Uchumi ulianza kushuka kipindi cha Obama?

Weka hapa source ya hiyo taarifa yako.
 
Hilary Clinton alikuwa tishio kwa Trump, tena alikuwa na back up ya Mme wake Rais mstaafu Clinton na Obama, pia alikuwa maarufu kuliko Kamala lakini Trump alimgaragaza.
Situation ya Hillary na Kamala hazifanani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…