Kamanda Mambosasa: Ni marufuku kufanya maandamano au Jogging siku za Ibada Jumapili, Jumamosi na Ijumaa!

Kamanda Mambosasa: Ni marufuku kufanya maandamano au Jogging siku za Ibada Jumapili, Jumamosi na Ijumaa!

[emoji849][emoji849][emoji849].
Mnazalisha taifa goi goi Sasa.
Mazoezi ni afya na asaa kipindi hichi Cha coronaa.
 
Hata hio jogging ni ibada kwa raia wengine ndugu polisi, Sababu katiba yetu imetupa uhuru wa kuchagua imani tunayoitaka, Sasa ukikataa kutoa vibali huoni unapingana na katiba ya jamhuri?
 
Safi sana, wanakera sana hawa. Wengine wanatoka Yombo Buza Kwa Mpalange wanaenda kukimbia Masaki, wanaleta usumbufu barabarani
Jamani ni kweli na wanapita kwenye makazi ya watu wanaimba matusi ya nguoni wengine, acha wazuiwe tupumzike maana wanakwaza sana na kelele zao
 
Jamani! Mbona tunaharibu nchi hii.Kama hawa wafanya mazoezi wanaingilia masuala ya ibada, si waongozwe tu namna bora ya kufanya kuliko kuwakataza ikiwemo barabara za kupita.

Wizara ya afya inasisitiza na kuhamasisha watu kufanya mazoezi, mazoezi ni afya. Mbaya zaidi siku za mwisho wa wiki ndipo wengi hupata nafasi. Kuwakataza si uungwana kwakweli. Kama vile waumini wanaona wanaingiliwa,na wanamazoezi pia wanaingiliwa kufanya mambo yao.
 
Hiyo jogging inayokatazwa ni ya vikundi au mtu mmoja mmoja na je hizo siku za ibada kama unakimbia jioni kuna madhara kwa wanaoabudu. Je kama nakimbia peke yangu (jogging) napaswa kuomba kibali?

Mazoezi ni njia ya kujikinga na COVID 19
 
Kamanda Mambosasa kazuia jogging na maandamano barabarani. Hakuzuia michezo. Hizo jogging siyo lazima zifanyike barabarani. Viwanja vya michezo vipo kwanini wasifanyie huko.

Binafsi huwa hizi jogging za barabarani huwa zinakera sana hasa kwenye kupishana magari na pia huwa ni wababe fulani hivi. Wanatanda upande mmoja wa barabara kiasi kuwa magari ya upande wao wanayazuia overtaking hadi upande mwingine uwe wazi. Kiukweli wanasumbua ukizingatia kuwa wakati mwingine unakuwa na haraka kuwahi muda wa ibada.
 
Kamanda wa polisi kanda maalumu ya Dar es salaam mh Mambosasa amesema kuanzia sasa ni marufuku watu kufanya maandamano na mbio za polepole ( jogging) siku za ibada yaani Jumapili, Jumamosi na Ijumaa na kwamba jeshi la polisi halitatoa vibali katika siku hizo....
Waislam tunafanya ibada Kila siku mara tano hivyo hatuna siku maalum ya ibadah. Hivyo hapo hakuna kuandamana kwa aina yoyote wala jogging za aina yoyote kwa siku saba za wiki.

Hatutaki kusikia hata chama twawala wanapewa kibali cha kuandamana kumpongeza fulani sababu wataleta usumbufu kwenye ibadah zetu.
 
Mmmmh naona kama Mambosasa kateleza kwenye hili! Michezo ni Afya na juzi Waziri wa Afya amesisitiza kufanya mazoezi maranyingi kadri tuwezavyo ili mapafu yaweze kutanuka na kuhimili kuwa na hewa ya kuyosha mwilini.

Huyu Kamanda anajitokeza anasiliba anyway naaamin labda habari siyo za kweli hizi
Kachemka saaana basi watengeneze viwanja vya mazoezi# Mitano tenaaa
 
Waislam tunafanya ibada Kila siku mara tano hivyo hatuna siku maalum ya ibadah. Hivyo hapo hakuna kuandamana kwa aina yoyote wala jogging za aina yoyote kwa siku saba za wiki. Hatutaki kusikia hata chama twawala wanapewa kibali cha kuandamana kumpongeza fulani sababu wataleta usumbufu kwenye ibadah zetu.
Swala tano mnaenda na magari?
 
Serikali haina dini..kwanink inataka kujiingiza kwenye dini maana ukisema Ijumaa,J'mosi na J'Pili amewalenga waislam na wakristu peke yake vipi kwa dini zingine?
 
Back
Top Bottom