Kamanda Mambosasa: Upelelezi wa kesi ya wafuasi 27 wa CHADEMA wakiwemo viongozi wanaodaiwa kufanya fujo gereza la Segerea umekamilika

Huenda itakuwa anawajengea hoja ya kesi nyingine, kwanza ilitoka taarifa huko Dodoma, pili ilitoka taarifa Dar na hii sasa ni ya tatu! Wanausongo na Chadema.

Wafungwa wako nchini ya magereza siyo polisi ambao jukumu lao liliisha siku ya hukumu.
Chadema ni sikio la kufa Mdee kusema kweli simpendi, kwanza tabia yake ya kutotafuta mwanaume akaolewa alafu atake tumchukulie kama kingozi shupavu inanikera.

Mdee si mfano bora kwa watoto wetu hasa wa kike na wamama wote kwa nchii.

Mwisho narudia Mbowe hatoshi kuongoza chadema anafanya siasa za kipuuzi sana muda wa kutumia akili yeye ni nguvu bila maarifa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkiambiwa ninyi ni POLICCM huwa hamkubali.

Hivi...kwani Mbowe hakutolewa kwa kulipiwa faini??

Kama faini ililipwa inawezekanaje watu wakamtoe Mbowe gerezani kwa nguvu??

Huyu kamanda bado hajatuambia aliyemteka Mo ni nani, anatoa longo longo tu.

Tukisema yeye anamjua aliyemteka Mo na kwamba ndiye aliyetoa amri ya kuwapiga wafuasi wa CDM na kwamba ndiye anayemuamuru kuutangazia uma ujinga huu atakataa???

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwanza atuambie alifikaje fikaje nyumbani kwa kina MO asubuhi asubuhi kufakamia chai.
 
Wakati mwingine ni ngumu sana kuuaminisha umma mtu aliyeenda kumpokea mtu kufanya fujo na kumchania polisi shati wakati siku chache zilizopita polepole aliyeenda magereza hiyohiyo tena na kuwaalika hadi na waandishi wa habari yeye hakuchana mashati ya polisi hao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndiyo maana hata mataifa makubwa yanatuambia sisi tupo vizuri mno kubumba maneno kuliko matendo....urongo urongo mwingii

Mzee kaamua kudanganya umma mchana kweupee
 
‪LIVE: Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya DSM Lazaro Mambosasa anazungumza kuhusu kilichotokea juzi Segerea wakati Freeman Mbowe akisubiriwa kutoka gerezani

=====

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI
JESHI LA POLISI TANZANIA

TAARIFA KWA UMMA.
KUKAMATWA KWA WAFUASI WA CHADEMA 27 KWA TUHUMA ZA KUFANYA FUJO KATIKA GEREZA LA MAHABUSU SEGEREA.

Mnamo tarehe 13.03.2020 majira ya saa 07:00 mchana Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam lilipokea taarifa kutoka kwa maofisa wa Gereza la Mahabusu Segerea kuwa kuna kundi la wafuasi wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) likiongozwa na wabumbe wawili ambao ni Halima James Mdee, Ester Amos Bulaya na Meya wa Ubungo Boniface Jacob limekusanyika katika geti la kuingilia gerezani hapo huku likiandamana na kufanya fujo kutaka kuingia kwa nguvu ndani ya gereza kwa lengo la kwenda kumtoa mwenyekiti wa chama chao Mhe.Freeman Mbowe.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum baada ya kupokea taarifa hizo lilituma askari wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) na askari wa kituo cha Polisi Stakishari na ambapo walipofika eneo hilo waliwakuta askari magereza wakiwa wanaendelea kuwadhibiti wanachama hao na ndipo Polisi walipowakamata watuhumiwa 27.

Baada ya watuhumiwa hao kukamatwa askari wa Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na askari wa Jeshi la magereza waliwachukua na kuwapeleka kituo cha Polisi Stakishari kwa mahojiano na baada ya mahojiano watuhumiwa wote 27 walidhaminiwa kwa mujibu wa sheria na watafikishwa mahakamani hivi karibuni kwani upelelezi wa shauri hili umeishakamilika.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linatoa onyo kali kwa kikundi chochote cha siasa,dini,au mtu yeyote kuacha kabisa kuchezea maeneo nyeti kama magereza,makambi ya Majeshi yote au maeneo yoyote ambayo ni nyeti kwa taifa.

Hivyo atakayejaribu kufanya hivyo atachukuliwa hatua kali za kisheria.

WATU 03 WAPOTEZA MAISHA KWA AJARI YA BARABARANI.

Mnamo tarehe 15.03.2020 majira ya 04:30 alfajiri huko barabara ya kawawa mataa ya veta gari namba T 530 DNW aina ya EICHER daladala linalofanya safari za Mbangara- Makumbusho likitokea Mbagala kuelekea Makumbusho liligongana na gari la kubebea nyama lenye namba T 744 DET lililokuwa likitokea Tazara kuelekea katikati ya Jiji na kusababisha vifo vya watu watatu ambao ni wanaume wawili na mwanamke moja na kusababisha majeruhi ya watu nane.

Chanzo cha ajari ni daladala kutaka kuwahi kupita kwenye taa nyekundu.

LAZARO MAMBOSAS– SACP
KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAM.
15/03/2020

CCM asilia amkeni, mtoseni Magufuli anazidi kuiharibu nchi ya mwemyeheri Nyerere
 
Mahakamani kuna taratibu zake, na magereza kuna taratibu zake. Eneo la Magereza siyo public toilet kwamba unaingia tu unavyojisikia wewe.
Jamani tuwe siriasi na kile tunachojaribu kukitetea walioumizwa nao ni binadamu siyo wanyama, kwa akili za kawaida tu,watu washindwe kwenda kumtoa Mbowe kabla faini haijalipwa mpaka waende kumtoa kwa nguvu baada ya faini kutolewa na hati ya kumtoa gerezani imeshatolewa wakati wanajua kuwa hiyo ndiyo hatima ya mwisho kwa Mbowe kuwepo gerezani, pasipo kukata rufaa wala kutumia nguvu ya kumtoa gerezani.
 
Huyu mambo sasa alivyo mjinga anadhani watanzania ni wajinga kiasi cha kuwaongopea hivyo???

Mtu kalipa faini, hati ya kumtoa gerezani anayo, anawezaje kwenda kutumia nguvu ili kumtoa Mbowe gerezani??

Basi mambosasa umefika wakati wa kutumia nguvu alizo nazo kwenda kwao kulima kuliko kutumia nguvu hizo kuunda hoja za kijinga hivyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizi ndio zile kesi za kubambikizwa anazo zikataa Mh. Rais. Hivi kwa uelewa wangu mdogo!! Wafungwa huwa wamezungushiwa tuu ukuta au hufungiwa ndani? Maana huyu Rpc ana taka kutumasnisha kwamba kama hawa waheshimiwa wange fanikiwa kuingia pale getini basi wafungwa wange toroka. Kwanini polisi hamjengi hoja za kweli?

Sent using Jamii Forums mobile app
Uwezo waa kujenga hoja watoe wapi? Hawana na hawatakuwa nao!
 
Hapa Tanzania hakuna kikosi cha polisi kinachopiga watu vibaya kama KMGM wamekosea sana kuwa provoke hao jamaa walitakiwa wajipange kidogo
 
Ukishaona ndani ya inchi uongo unatumika kwa watu waliopewa dhamana ya kutuongoza na imegeuka kuwa kitu cha kawaida basi jua kwamba kupambazuka kuko kalibu, sababu haiwezekani kwa mtu Mwenye akili timamu akubaliane na hayo yanayoongelewa na polisi
 
‪LIVE: Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya DSM Lazaro Mambosasa anazungumza kuhusu kilichotokea juzi Segerea wakati Freeman Mbowe akisubiriwa kutoka gerezani

=====

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI
JESHI LA POLISI TANZANIA

TAARIFA KWA UMMA.
KUKAMATWA KWA WAFUASI WA CHADEMA 27 KWA TUHUMA ZA KUFANYA FUJO KATIKA GEREZA LA MAHABUSU SEGEREA.

Mnamo tarehe 13.03.2020 majira ya saa 07:00 mchana Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam lilipokea taarifa kutoka kwa maofisa wa Gereza la Mahabusu Segerea kuwa kuna kundi la wafuasi wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) likiongozwa na wabumbe wawili ambao ni Halima James Mdee, Ester Amos Bulaya na Meya wa Ubungo Boniface Jacob limekusanyika katika geti la kuingilia gerezani hapo huku likiandamana na kufanya fujo kutaka kuingia kwa nguvu ndani ya gereza kwa lengo la kwenda kumtoa mwenyekiti wa chama chao Mhe.Freeman Mbowe.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum baada ya kupokea taarifa hizo lilituma askari wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) na askari wa kituo cha Polisi Stakishari na ambapo walipofika eneo hilo waliwakuta askari magereza wakiwa wanaendelea kuwadhibiti wanachama hao na ndipo Polisi walipowakamata watuhumiwa 27.

Baada ya watuhumiwa hao kukamatwa askari wa Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na askari wa Jeshi la magereza waliwachukua na kuwapeleka kituo cha Polisi Stakishari kwa mahojiano na baada ya mahojiano watuhumiwa wote 27 walidhaminiwa kwa mujibu wa sheria na watafikishwa mahakamani hivi karibuni kwani upelelezi wa shauri hili umeishakamilika.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linatoa onyo kali kwa kikundi chochote cha siasa,dini,au mtu yeyote kuacha kabisa kuchezea maeneo nyeti kama magereza,makambi ya Majeshi yote au maeneo yoyote ambayo ni nyeti kwa taifa.

Hivyo atakayejaribu kufanya hivyo atachukuliwa hatua kali za kisheria.

WATU 03 WAPOTEZA MAISHA KWA AJARI YA BARABARANI.

Mnamo tarehe 15.03.2020 majira ya 04:30 alfajiri huko barabara ya kawawa mataa ya veta gari namba T 530 DNW aina ya EICHER daladala linalofanya safari za Mbangara- Makumbusho likitokea Mbagala kuelekea Makumbusho liligongana na gari la kubebea nyama lenye namba T 744 DET lililokuwa likitokea Tazara kuelekea katikati ya Jiji na kusababisha vifo vya watu watatu ambao ni wanaume wawili na mwanamke moja na kusababisha majeruhi ya watu nane.

Chanzo cha ajari ni daladala kutaka kuwahi kupita kwenye taa nyekundu.

LAZARO MAMBOSAS– SACP
KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAM.
15/03/2020

Jamaa wanawapa kiki wapinzani enzi za Lyatonga Mrema mwalimu Nyerere alisema mwacheni asukumwe kwenye gari wakichoka wataacha leo mzee wa kilalacha yupo wapi? Mpaka serikali za mitaa kapigwa
 
Back
Top Bottom