Hahaha sasa Lisu anataka kujenga chama gani? Chama chenye uwazi siyo chadema, tayarai mmesha sema Mbowe ndiye muhasibu, na ndiye kila kitu.
Chadema ina baraza la wazee, ina kamati kuu na ngazi nyingi tu ambazo hayo yanaweza kuulizwa.
Chadema inakaguliwa kila mwaka na CAG, msajiri anapewa copy. Chadema inapokea Ruzuku hivyo msajiri anaifahamu account ya chama.
Wewe na Lisu mnaifahamu account ya chama, lakini manataka siasa za kuchafuana. Mnaweza kujenga hoja kujitoa chadema, maana imeshaacha misingi yake, Mnasubiri nini Mkono wa kwaheri?
Ile ni taasis, inahitaji siri na hekima , wewe na Lisu mnataka kuanika account hadharani ili kukidharirisha chama kwa faida yenu. Yeye anataka kupayuka kila kitu hadharani, kujipa ujuaji wa kila kitu.
Account za chadema zipo na zinajulikana, na hzina shida hizo mnazotaka ziwe nazo.
Lisu ni mwanasheria na wakili msomi, chadema siyo baba wala mama yake, chadema imeshaacha misingi iliyokuwa ikiisimamia, Lisu anasubiri nini kuondoka?