Kamanda Muliro kajichanganya kuhusu sakata la Sativa kwenye Kongamano la TLS?

Kamanda Muliro kajichanganya kuhusu sakata la Sativa kwenye Kongamano la TLS?

Huwajui polisi wa Tanzania
Kwa mfano
Polisi hawahawa walimuua Mkurugenzi wa zamani wa usalama wa Taifa.

Polisi hawahawa waliwaua wafanyabiashara wa madini kutoka morogoro.

Polisi hawahawa walimuua mfanyabiashara wa Mtwara na kesi ipo mahakamani.
Hata ingekuwa kweli huyo Sativa ana hadhi gani labda ya hadi polisi wakusanye resources zao kutaka kumuua ? Mbona hamna kitu pale
 
Nani yupo sawa Muliro au Sativa. Sativa alisema katekwa na Washkaji na Muliro kadai wao ndio walimuokoa alivyotekwa. Swali linakuja kwanini Sativa kaokolewa na polisi ila washkaji wakaachiwa au hawakukamatwa?.
Read my comment again
 
Hata ingekuwa kweli huyo Sativa ana hadhi gani labda ya hadi polisi wakusanye resources zao kutaka kumuua ? Mbona hamna kitu pale

Hana hadhi kabisa, ila kwanini muhusika hakamatwi Kama polisi ndio walimuokoa?.
 
Haa HaaMakamanda Hao Tangu MO Atekwe
Ona body language ya Mo alipokuwa anampa mkono walipoandaa press ya Mo aipongeze serikali kwa kupatikana kwake.

Ona anavyoogopa kutoa mkono utajua ..
images - 2024-08-19T132010.103.jpeg
 
Mwisho, Napenda kumshauri Kamanda Muliro awe Neutral asioneshe upande wake. Leo ni kama alijipanga kuja kupambana na sio kuleta suluhisho au kuleta mpango wa Jeshi la polisi DSM kupambana na utekaji. Pia ni muhimu kukiri mapungufu kwenye jeshi la polisi hasa kwenye utekaji.
Kuna mtu alishasema polisi wa Tanzania ni empty set huwa hawajui walifanyalo
 
Waongo Sana. Mtu anadai wao ndio waliomwokoa sativa hapo hapo anadai wapo kwenye upelelezi mkali kumkamata muhusika wa utekaji wa Sativa. Yani walishindwa kumkamata wakati wanamwokoa waje wamakamate Sasa hivi? Muongo sana.
Eti hii ndio CCTV footage ya gari iliyotumika kumteka Mo Dewji!

Mchek huyo kamanda machoni.

Mbona ya Area D hawajaileta hadi leo.?
images - 2024-09-12T154504.260.jpeg
 
Leo kwenye Kongamano la TLS kuhusu utekaji na kupotea Kwa raia, Kamanda Muliro amejichanganya kwa kuelezea kuhusu suala la Sativa...
Kakiri kuwa utekaji na upoteaji upo na akatolea mifano mbali mbali kmf papaa Msofe, lakini katetea kwa nguvu zote jeshi la Polisi kutokujihusisha na utekaji.

Maelezo yake yote hakuna popote alipounga mkono serikali kujihusisha na utekaji na kupoteza watu.

Huyu alijipanga kama unavyosema mleta mada, kuja kupangua hoja maudhui ya forum.

Mi husikitishwa sana kuona kiongozi yeyote anayesimama kwenye mimbari na kutetea uongo kwa mambo ambayo yako wazi kabisa katika macho ya jamii.

Hivi angelipotezwa mwanaye wa kuzaa, angelikubali na kuamini upelelezi wa kasi ya kinyonga kwa mambo yaliyo wazi kama ya Sativa?
 
Ukiona amechanganyikiwa hivyo ujue amedhurumu sana haki za watu, lazima ajichanganye na ndio maana polisi wakibanwa mahakamani na mawakili huwa wanaonekana kabisa kuwa sio watu wa haki.
 
Ukimsikiliza vizuri Sativa hajatekwa ba Polidi

Polisi hawa wa Tanzania wahangaike na mtu kuanzia Dar wazurure naye karibu nusu ya nchi halafu wakamtupe Katavi

Sidhani polisi wa Tanzania if they mean business wana muda huo

Huyo Sativa Inaonyesha hao watu walikuwa wanajuana na walikuwa na deal zao labda alipewa madawa ya kulevya au madini auze kwa matajiri kisha awape pesa zao wakatofautiana mbele ya safari.

Huo mzunguko kutoka Dar to Arusha then huko kwingine may be aliwazulumu akawa anawadanganya kuwa hayajauzika na mhusika mara yuko Arusha mara sijui yuko mkoa gani baadaye wakaona anawapootezea muda na gharama.Wakashughulika naye.

Hadithi yake ukimsikiliza polisi anawabambikia kesi tu polisi kwa kushawishiwa na wanasiasa tu Lakini anachoongea ukisikiliza kwa makini unaona wazi kuna kitu anaficha
Mkuu na Mzee kibao naye wanasingiziwa? Je, analysis yako inasemaje kuhusu kina soka au dogo wa Tanga???
 
Mkuu na Mzee kibao naye wanasingiziwa? Je, analysis yako inasemaje kuhusu kina soka au dogo wa Tanga???
Upelezi unaendelea kujua kama ni inside Job ndani ya Chadema au Boni yai yuko ndani na Mnyika kajifungia kanisani hataki kwenda polisi kuhojiwa polisi wanamsubiri asaidie upelelezi akitoka huko kanisani alikojifungia
 
Leo kwenye Kongamano la TLS kuhusu utekaji na kupotea Kwa raia, Kamanda Muliro amejichanganya kwa kuelezea kuhusu suala la Sativa.

1. Kwanza, amekiri kwamba Sativa kabla ya kuhojiwa alikiri kuwa anamjua aliyemteka.

2. Pili, Kamanda Muliro amedai ya kwamba baada ya kauli ya Sativa , alitokea mtu anayejiita whistleblower kwenye mtandao wa x zamani Twitter na kuelezea kuwa aliyemteka Sativa alikuwa ni mtu Fulani.

3. Tatu, Kamanda Muliro kadai ya kwamba walipomhoji Sativa alikiri kwamba akitekwa na washkaji Fulani hivi.

4. Nne, Kamanda Muliro amedai kuwa baada ya mahojiano ameshangaa kusikia stori tofauti ya Sativa kwamba alitekwa na Mafwele.

5. Tano, kamanda Muliro amedai kwamba suala la Sativa linafanyiwa upelelezi na kwamba Kuna wanasheria na wataalamu wanalifuatilia Hilo jambo kwa kina.

6. Mwisho, Kamanda Muliro kadai ya kwamba wao ndio walimuokoa Sativa, Jambo ambalo ukumbi mzima ulipinga kwa mshangao.

Swali linakuja Kamanda Muliro anadai kwamba walimuokoa Sativa, je walimuokoa kutoka wapi na dhidi ya nani. Je nani aliwapa taarifa ya kwenda kumuokoa? Kama waliweza kwenda kumuokoa wanashindwaje kumkamata muhusika. Kwakweli hapa ndipo tatizo lipo. Halafu Cha kusikitisha jeshi la polisi wapo kwenye uchunguzi wa kina huku mtuhumiwa mkuu ndio ZCO wa Dar es Salaam. Huo ni upelelezi au komedi. Ilitakiwa Mafwele apelekwe likizo ya muda kupisha upelelezi na si vingine.

Pia Kamanda Muliro kadai ya kwamba Sativa alidai ya kwamba katekwa na Washkaji na sio mafwele. Sasa ni kwanini jeshi la polisi linatumia nguvu nyingi kudai hajatekwa na Mafwele baadala ya kuwakamata hao washkaji waliotajwa?. Kama jeshi la polisi linaamini alitekwa na washkaji, ni kwanini inakuwa ngumu kuwakamata Hawa washkaji?. Kama washkaji wa mtaani ni ngumu kuwakamata je polisi wataweza kumkamata nani?.

Mwisho, Napenda kumshauri Kamanda Muliro awe Neutral asioneshe upande wake. Leo ni kama alijipanga kuja kupambana na sio kuleta suluhisho au kuleta mpango wa Jeshi la polisi DSM kupambana na utekaji. Pia ni muhimu kukiri mapungufu kwenye jeshi la polisi hasa kwenye utekaji.
Kavideo kapo? 🐼
 
muliro ni debe tupu ubongo wa mbele na nyuma hazisomani
 
Kwamba Polisi wamtoe Dsm wampeleke Arusha na baadae Katavi, Kwa lipi yaani? Sativa yafaa aseme ukweli nini kilisababisha kukutwa Hifadhini Katavi
 
Kwa kweli kuna binadamu wenzetu wameshajivua ubinadamu na kuuvaa unyama.......yaani wao furaha yao ni kuona binadamu wenzao wanateseka na kufariki ikiwa tu vyeo na madaraka vitaingiliwa.......

Wao wanajiona wataishi milele......wao wamejipa mamlaka za kutesa na kunyakua roho za binadamu wenzao kana kwamba wao wana ushirika na muumba.....

Matendo yao machafu yaliyokithiri yamepofusha mioyo yao mpaka imekuwa ngumu kwao kuurejea ubinadamu............

Nawakumbusha kuwa kama ambavyo waliapa kwa vitabu vya dini kuwakilisha kuwa yupo aliye juu na mwenye mamlaka.....

Iko siku watalipia kila ubaya wa tendo lao......na siku hakutakuwa na jeshi la polisi wala magari ya kuwasha....bali ni wao na mola wao mlezi.......

MUNGU YUPO......
Amen 🙏
 
Back
Top Bottom