Kamanda Muliro kajichanganya kuhusu sakata la Sativa kwenye Kongamano la TLS?

Leo kwenye Kongamano la TLS kuhusu utekaji na kupotea Kwa raia, Kamanda Muliro amejichanganya kwa kuelezea kuhusu suala la Sativa.

1. Kwanza, amekiri kwamba Sativa kabla ya kuhojiwa alikiri kuwa anamjua aliyemteka.

2. Pili, Kamanda Muliro amedai ya kwamba baada ya kauli ya Sativa , alitokea mtu anayejiita whistleblower kwenye mtandao wa x zamani Twitter na kuelezea kuwa aliyemteka Sativa alikuwa ni mtu Fulani.

3. Tatu, Kamanda Muliro kadai ya kwamba walipomhoji Sativa alikiri kwamba akitekwa na washkaji Fulani hivi.

4. Nne, Kamanda Muliro amedai kuwa baada ya mahojiano ameshangaa kusikia stori tofauti ya Sativa kwamba alitekwa na Mafwele.

5. Tano, kamanda Muliro amedai kwamba suala la Sativa linafanyiwa upelelezi na kwamba Kuna wanasheria na wataalamu wanalifuatilia Hilo jambo kwa kina.

6. Mwisho, Kamanda Muliro kadai ya kwamba wao ndio walimuokoa Sativa, Jambo ambalo ukumbi mzima ulipinga kwa mshangao.

Swali linakuja Kamanda Muliro anadai kwamba walimuokoa Sativa, je walimuokoa kutoka wapi na dhidi ya nani. Je nani aliwapa taarifa ya kwenda kumuokoa? Kama waliweza kwenda kumuokoa wanashindwaje kumkamata muhusika. Kwakweli hapa ndipo tatizo lipo. Halafu Cha kusikitisha jeshi la polisi wapo kwenye uchunguzi wa kina huku mtuhumiwa mkuu ndio ZCO wa Dar es Salaam. Huo ni upelelezi au komedi. Ilitakiwa Mafwele apelekwe likizo ya muda kupisha upelelezi na si vingine.

Pia Kamanda Muliro kadai ya kwamba Sativa alidai ya kwamba katekwa na Washkaji na sio mafwele. Sasa ni kwanini jeshi la polisi linatumia nguvu nyingi kudai hajatekwa na Mafwele baadala ya kuwakamata hao washkaji waliotajwa?. Kama jeshi la polisi linaamini alitekwa na washkaji, ni kwanini inakuwa ngumu kuwakamata Hawa washkaji?. Kama washkaji wa mtaani ni ngumu kuwakamata je polisi wataweza kumkamata nani?.

Mwisho, Napenda kumshauri Kamanda Muliro awe Neutral asioneshe upande wake. Leo ni kama alijipanga kuja kupambana na sio kuleta suluhisho au kuleta mpango wa Jeshi la polisi DSM kupambana na utekaji. Pia ni muhimu kukiri mapungufu kwenye jeshi la polisi hasa kwenye utekaji.
Huyu polisi hajui anapaswa kufanya nini.
 
Mnamkumbuka yule mamboyazamani alisema cctv kamera ililifuatilia gari toka Ostabei mpaka Mwenge kisha gari likapotea! Hiyo ni cctv kamera inayotembea barabarani.
 
Ningekuwa Nina mamlaka ningekataza kabisa polisi wangu au vyombo vyangu vya usalama kuhudhuria hii mikutano inayoanzishwa na hawa simbilisi wenye mafungamano na chadema. Kwao hawana jema hawa, Kila kitu watapinga na watajivua ufahamu wote kadiri mbowe au lissu watakavyoamrisha.

Muliro Hana haja ya kumaliza his beautiful time kuwaelekeza chochote hao wanafiki wasiobebeka......atulie kituoni awasubiri katika maandamano awasambaratishe.
 
Afande Muliro ametusaidia kujua sasa tena kwa uhakika kuwa kuna CCM kama chama na kuna CCM nyingine ambayo ni Dola. Kwa upande mwingine ipo Police na PoliCCM. Hizi ni taasisi ambazo zinaonekana kukinzana katika utendaji wake. :AYOOO:
 
Ningekuwa Nina mamlaka ningekataza kabisa polisi wangu au vyombo vyangu vya usalama kuhudhuria hii mikutano inayoanzishwa na hawa simbilisi wenye mafungamano na chadema. Kwao hawana jema hawa, Kila kitu watapinga na watajivua ufahamu wote kadiri mbowe au lissu watakavyoamrisha.

Muliro Hana haja ya kumaliza his beautiful time kuwaelekeza chochote hao wanafiki wasiobebeka......atulie kituoni awasubiri katika maandamano awasambaratishe.
Ndo maana huna hayo mamlaka.Akili zako ni uozo mtupu.
 
Ukimsikiliza vizuri Sativa hajatekwa na Polidi

Polisi hawa wa Tanzania wahangaike na mtu kuanzia Dar wazurure naye karibu nusu ya nchi halafu wakamtupe Katavi

Sidhani polisi wa Tanzania if they mean business wana muda huo

Huyo Sativa Inaonyesha hao watu walikuwa wanajuana na walikuwa na deal zao labda alipewa madawa ya kulevya au madini auze kwa matajiri kisha awape pesa zao wakatofautiana mbele ya safari.

Huo mzunguko kutoka Dar to Arusha then huko kwingine may be aliwazulumu akawa anawadanganya kuwa hayajauzika na mhusika mara yuko Arusha mara sijui yuko mkoa gani baadaye wakaona anawapootezea muda na gharama.Wakashughulika naye.

Hadithi yake ukimsikiliza polisi anawabambikia kesi tu polisi kwa kushawishiwa na wanasiasa tu Lakini anachoongea ukisikiliza kwa makini unaona wazi kuna kitu anaficha
Hapa ndio unaona umetupoteza maboya ile mbaya. Ww lazima utakuwa ni mzee, maana wazee ndio huwa wana story za hivi wakiamini wanaweza kuchanganya watu. Ni hivi, watekaji ni vyombo vya dola kwa maagizo ya rais, na wanapata kinga ya kufanya huo uovu kupitia sheria mpya ya usalama wa taifa.
 
Ningekuwa Nina mamlaka ningekataza kabisa polisi wangu au vyombo vyangu vya usalama kuhudhuria hii mikutano inayoanzishwa na hawa simbilisi wenye mafungamano na chadema. Kwao hawana jema hawa, Kila kitu watapinga na watajivua ufahamu wote kadiri mbowe au lissu watakavyoamrisha.

Muliro Hana haja ya kumaliza his beautiful time kuwaelekeza chochote hao wanafiki wasiobebeka......atulie kituoni awasubiri katika maandamano awasambaratishe.
Uko sahihi, maana hakuna jambo gumu kama kutetea uovu. Leo Muliro amejikuta kwenye wakati mgumu maana alikuwa anajaribu kutetea uovu unaofanywa na vyombo vya dola. Huu ushauri wako ni sahihi maana polisi kushiriki kwenye hii midahalo ni kukubali kuanika uovu wao hadharani.
 
Kakiri kuwa utekaji na upoteaji upo na akatolea mifano mbali mbali kmf papaa Msofe, lakini katetea kwa nguvu zote jeshi la Polisi kutokujihusisha na utekaji.

Maelezo yake yote hakuna popote alipounga mkono serikali kujihusisha na utekaji na kupoteza watu.

Huyu alijipanga kama unavyosema mleta mada, kuja kupangua hoja maudhui ya forum.

Mi husikitishwa sana kuona kiongozi yeyote anayesimama kwenye mimbari na kutetea uongo kwa mambo ambayo yako wazi kabisa katika macho ya jamii.

Hivi angelipotezwa mwanaye wa kuzaa, angelikubali na kuamini upelelezi wa kasi ya kinyonga kwa mambo yaliyo wazi kama ya Sativa?

Inasikitisha Sana mkuu.
 
Upelezi unaendelea kujua kama ni inside Job ndani ya Chadema au Boni yai yuko ndani na Mnyika kajifungia kanisani hataki kwenda polisi kuhojiwa polisi wanamsubiri asaidie upelelezi akitoka huko kanisani alikojifungia

Punguza mizaha kwenye issue serious. Tatizo lako unaiabudu CCM mpaka utu umekuondoka. Unaona raia wengine wasio na vyama sio watanzania.
 
Kwamba Polisi wamtoe Dsm wampeleke Arusha na baadae Katavi, Kwa lipi yaani? Sativa yafaa aseme ukweli nini kilisababisha kukutwa Hifadhini Katavi

Ukweli utapatikana wakikamatwa wahusika
 
Back
Top Bottom