Kamari imeharibu kila kitu kwenye maisha yangu

Ndio maana yake betting sio ajira ya Kila mtu Bali ni ya watu wachache tunaojielewa ukiona mtu anasema betting mbaya ujue sio kazi yake atafute kazi nyingine
Hakuna mtu ambaye hatetei chake unahaki ya kutetea chako
 
Cheza fx cryptocurrency trading za maana acha betng hazna maana
 
Dogo watu tupo kwenye industry toka 2011 nyie mnao firisika yawezekana hua mnarogwa
 
Sijui ila nadhani ungepaswa kutoa ushauri... betting ni tatizo Kwa vijana wengi si huyo tu. Cha msingi apambne kuondkan na hyo hali
Tatizo lolote kwa mtu au jamii linaanzia ktk akili yake.
Tunawezakubali kwamba ni tatizo,lakini mitaani anakoishi kijana mwenzake akashinda milion 10,huyu mtu tutamsaidiaje kwa hicho atakachokuwa amekiona hapo mtaani kwake??

Ngono kwa vijana ni tatizo,lakini lazima tuwaambie kama ni lazima wafanye basi wahakikishe wafate kanuni za kiafya ili kuepuka madhara yake ya moja kwa moja
tukiwa tunafoka tu ngono hivi,ngono vile wakati tunalala chumba kimoja wanaona wanatuona sisi wachawi.

Betting kama ilivyo kilevi chochote ni kibaya kama utakiendekeza,lazima uwe na nidhamu ktk kiasi cha matumizi,ambayo utaitumia hata ktk maisha mengine ya kila siku,
Mimi nachoweza kumwambia asiache betting,aache upumbavu.
 
Wakati unakula efu 78 yangu kwa hiyo buku mbilj yako ulijiona nani?
 
Njia Zipo nyingi ila mojawapo ni kuchukua maaamuzi magumu.Si lazima ashirikiane sana na wacheza kamali wenzake lakini ajaribu kushirikiana zaidi na watu wasiopenda kamali. Hii hitachochea kubadirisha fikira zake ndani ya muda mfupi na baadae atajikuta anachukia kucheza kamali.Ingawa sio rahisi kuchukuwa maaamuzi hayo lakini inabidii.

Mbili,hamtangulize mungu, kwa Mungu hakuna kinachoshindikana na maisha bila kamali inawezekana.Kamali ni adui wa maendeleo.
 
Alfu bado Kuna mtu anasema kubet sio tatizo..ety tatizo n mtu mwenyw sijui imekaa vp hyo?
πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚
Kila kitu fanya kwa kiasi. Roho iliniuma kama wiki mbili nilikuwa nataka kama 30K nikaweka mechi ya England sijui na Slovenia. Zipatikane goal mbili tu. Nikatia 100,000. Alafu timu mbili tu. Huwezi amini dk ya 13 Jude Bellingham katia goli nikajua hapa tayari. Mpira ukaisha likabaki goal lile. Laki yote ikaenda.
Nikajiambia shikamoo Kanji πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Kwaiyo unataka nini au Umekuja Kulia Jf
Hapana ndugu sikuja kulia humu mimi, apa nilipo toka tarehe 23 jana ad leo naishi maisha ya ajabu mno nalala popote then nakula chochote nachopata njiani. UNAWEZA jiuliza kwa nini imekuwa hivyo ad naishi maisha haya? ukweli ni kwamba siku hiyo nilipatiwa nauli ya kwenda mkoa x, pamoja na fedha ya mahitaji nikiwa uko lakini still bado nilipitiwa kwa betting na nkalose yote so kurudi home siwez wala nini natanga tanga apa natafuta lift za mkoa huo ili nisepe zangu lakini mambo bado magumu mpaka najuta kwa nini mimi?
 
samahani ni mwez jana tarehe 23
 
Betting ni utapeli indirect, utashinda sana tu lakini amini utarudisha na fidia juu!
 
Nilikua nataka nione tu baada ya biashara unayosema uliachana na ajira umeingiza sh ngapi kwa miaka yote hiyo nimechoka nilipoiona milion 4 πŸ˜„! Wenzio hyo ni posho tu ya mwezi bado misheard mishe! Pole sana.
Mimi hiyo nahonga demu na kumuomba msamaha kwakuwa ni ndogo sana.
 
Jinga kabisa eti umemudu kununua vikofia viwili tuh Kwa mwanao hadi sasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…