Kamari imeharibu kila kitu kwenye maisha yangu

Kamari imeharibu kila kitu kwenye maisha yangu

Pole kijana Mimi pia ni muhanga na hii kitu , ila naeza SEMA angalau Hela nliyoliwa sio pesa yangu ya jasho wala ya wazazi Bali ni pesa ya bumu tu ya matumizi binafsi chuoni mana wengine wanahonga wengine wanailia Bata wengine wanapenda kupendeza ko mwendo wa nguo na viatu ila mm nliiweka kwny betting Kwa kuweka odds 2 natia laki . Katika betting unaweza ona kitu ni uhakika mfano yanga anacheza na majimaji watu wanaekaga ata milion ili wapate laki Kwa vile wanaona yanga anashinda uhakika , ila mipira haitabiriki ndo nlichojifunza ndomana odd 1.01 inachana fresh tu,NB hakuna option kwny kubeti Ina asilimia 💯 kutiki bali inaeza kua na 99%, kama option sio asilimia 💯 uwezekano wa tukio kutokea basi jua pesa Yako IPO hatarini kupotea Yani umeiwekea rehani haijalishi chochote na hakuna tukio lenye uwezekano wa 100% kwny mpira au mchezo wowote ko ni ubahatishaji tu usidanganywe na odds Wala ukubwa wa timu
mkeka me ckuwa naweka ata kidogo me nilikuwa na dili na virtual games na mchezo wangu mkubwa ulkuwa ni spin na wa pili ni aviator
 
kama ulkuwa unaniona vile kaka me nlikuwa na spin tuu na mara chache chache nacheza aviotor kwa simu nkiwa npo kwa ofisi
Ku spin ni hatari mnoo mimi niliwahi jiingiza huko asubuhi tu nishamaliza kunywa chai nazama huko kuondoka ni mpaka niishiwe kiasi nilichoenda nacho au kufungwe, ila nashukuru nilifanikiwa kuchomoka na sitarudi tena
 
Kwanza nitangulize salamu zangu kwa wanajamvi wote humu ndani, Tumsifu yesu kristo, Asaalam Aleykum.
Mimi ni kijana wa miaka 26 (me) elimu yangu ya juu ni degree ya tourim managment niliyoipata SUA miaka 2 iliyopita.

Kiufupi Mimi ni muumin mzuri wa biashara hivyo basi baada ya kuhitimu elimu yangu pale SUA mwaka 2022 nilikuwa nmefankiwa kukusanya kiasi fulani cha fedha kwa ajili ya kufanya biashara na kweli nilirudi mkoani kwangu na kufungua biashara ya kuuza vyombo vya ndani katika soko la kilombero, Hivyo kwangu cheti hakikua na maana yoyote ile kwani nia yangu ilikuwa niwe mfanya biashara mkubwa tuu hivyo cheti cha form six na chuo vyote sikuchukua kwani sikua na mpango ata theluthi moja wa kuajiriwa.

Hivyo basi ubongo na akili niliviboost kimapacha ili nikue kibiashara na kweli mambo yalikuwa poa, huku classmate wangu wengne wakitafta ajira. Mpaka kufika mwaka jana mwezi wa 8(august) nikuwa na kiasi cha 4 million.

Basi bhana kuna siku classmate wangu mmoja alniomba tukutane mtaa flani iv na me nkaenda kweli kumskilza ila kwa bahati mbaya alkua kwenye nyumba ya michezo ya bahati na sibu bas bhana tukapiga story na nkamuomba anielekeze namna ya kubeti alooooo hapo ndo nilipo jiloga mwenyewe kwani kwa siku ile nilkula kama elfu 78 kwa dau la 2500 nkasema mbona pesa apa ni chap chap.

WAKUU kuanzia hapo nilkuwa mkamaria mzuri yaan mpaka kuna time nlikua naacha ofisi yenyewe naenda kupambana na betting niwe mkweli betting imeniharibu vibaya mnoo na kunifilisi kila kitu nlichokuwa nacho apa nlipo sina simu wala ata senti moja.

BETTING imeharibu si tu uchumi wangu ata mahusiano na jamii,ndugu,pamoja na marafiki kwan uaminifu tena na mimi hawana PILI betting imenipotezea hisia za mapenzi, hofu ya mungu pamoja na ladha ya chakula kiufupi tyuu saiv akili na ubongo kila kukicha ni kuwaza betting na nimekuwa nikishinda kwenye nyumba za betting kuanzia asubuhi ad wanafunga yaani kula yangu yenyewe ad nipige ukware nikipata buku nile jero na jero nibaahatishe bahati yangu lakini nmeambulia kuwa mtu wa kujilaumu ad kna mda natamani tyuu bora nife coz I am great loser en dis is painful to me always en am lose hope,light en love.

NOW tumain pekee la kwa nini niishi ni namhurumia mwanangu pamoja na mam yake vip wataishi? ni heri nichechemee hivi hivi huku nikifurahia tabasamu la kachanga kangu though sijui now ako na two month nlichomudu kumnunulia ni kofia mbili tyuuu that too bad to how dis fucking aibu inantafuna.


Pole Sana kaka , shit always is there.

Muda bado upo wa kurekebisha makosa.

Anza na Meditation au tahajud au sala za usiku.

Mkabdhi Mungu kila kitu kuanzia sasa
Unapoamka usiku muombe Sana Mungu akurejeshe on the right way .

Pia jisamehe usijihukumu maana kamali sio wewe tu there's a lot of the people imeua dreams zao so usjione wewe ndo umekumbwa na hilo tatizo peke yako.


Then practice gratitude kila mara kila dakika jizoeze kushukuru Amini utarudi katika Raman I soon as possible.

And finally cherish every single moment

Learn from LS (Mistakes ) but don't dwell on negative thoughts &Past.

Tuna Dakika Sana duniani so blaming is ill.
 
On a serious note, kuacha kamari ni kujikana. Na huez amini, ukifanikiwa ndani ya mwez mmoja kutocheza kamari tayari uko kwenye njia njema.
hii kitu nliambiwa na padre mmoja pale st terresia nlipoenda kutafta msaada wa kiroho. In a nut shell "tatizo la mtu ni mtu mwenyewe so wewe pekee ndo unaweza kuamua kuacha ama lah!!!" but kwangu imekuwa ngumu hii kitu
 
Nilikua nataka nione tu baada ya biashara unayosema uliachana na ajira umeingiza sh ngapi kwa miaka yote hiyo nimechoka nilipoiona milion 4 😄! Wenzio hyo ni posho tu ya mwezi bado misheard mishe! Pole sana.
Kila mtu na kiwango chake
 
Nilikua nataka nione tu baada ya biashara unayosema uliachana na ajira umeingiza sh ngapi kwa miaka yote hiyo nimechoka nilipoiona milion 4 😄! Wenzio hyo ni posho tu ya mwezi bado misheard mishe! Pole sana.
Lakini kwa mfanya biashara hyo 4ml ata kama kaipata kwa miaka 10.....bado ananafasi nzuri ya kuiongeza hyo mara tano yake kwa miaka 2...

Biashara ni kama baiskeli itachukua muda kujifunza ila ukishaweza ndo umeweza...
 
Back
Top Bottom