Kamari imeharibu kila kitu kwenye maisha yangu

Kamari imeharibu kila kitu kwenye maisha yangu

kama ulkuwa unaniona vile kaka me nlikuwa na spin tuu na mara chache chache nacheza aviotor kwa simu nkiwa npo kwa ofisi
Wewe akili huna hapo ulikua haubeti Bali ulikua unaliwa hivi mtu mwenye akili timamu utacheza aviator wabongo akili mnaweka wapi yaani unacheza kitu kinachochezeshwa na kompyuta akili huna mzee hupasi kuonewa huruma
 
Wewe akili huna hapo ulikua haubeti Bali ulikua unaliwa hivi mtu mwenye akili timamu utacheza aviator wabongo akili mnaweka wapi yaani unacheza kitu kinachochezeshwa na kompyuta akili huna mzee hupasi kuonewa huruma
samahani ndugu je kubeti ni kufanyaje yawezekana nkapata chochote kupitia wewe! seems like betting is all about winng right?
 
Anhaa duh Yani mi napendelea sana sports kuliko games, michezo halisia naona kabisa apa man city kakandwa live kabisa dk 90 na nlimpa ashinde au naona kabisa mpka dk ya 90 watu wamegoma kufungana Ngoma 0-0 na nliiweka over 1.5.l, games zile jau sana na apo ndo kampuni za betting zinapiga pesa nyngi sana Yani spin Ile ni bahati kwelkwel kupata na pia nahisi inachezeshwa tu na bookies , aviator nacho nlijaribu nkaona kina flew away kwny 1.00 nkaona ni utapeli tu apa Bora angalau michezo halisi inaenda na uhalisia na uwezekano
 
Kwanza nitangulize salamu zangu kwa wanajamvi wote humu ndani, Tumsifu yesu kristo, Asaalam Aleykum.
Mimi ni kijana wa miaka 26 (me) elimu yangu ya juu ni degree ya tourim managment niliyoipata SUA miaka 2 iliyopita.

Kiufupi Mimi ni muumin mzuri wa biashara hivyo basi baada ya kuhitimu elimu yangu pale SUA mwaka 2022 nilikuwa nmefankiwa kukusanya kiasi fulani cha fedha kwa ajili ya kufanya biashara na kweli nilirudi mkoani kwangu na kufungua biashara ya kuuza vyombo vya ndani katika soko la kilombero, Hivyo kwangu cheti hakikua na maana yoyote ile kwani nia yangu ilikuwa niwe mfanya biashara mkubwa tuu hivyo cheti cha form six na chuo vyote sikuchukua kwani sikua na mpango ata theluthi moja wa kuajiriwa.

Hivyo basi ubongo na akili niliviboost kimapacha ili nikue kibiashara na kweli mambo yalikuwa poa, huku classmate wangu wengne wakitafta ajira. Mpaka kufika mwaka jana mwezi wa 8(august) nikuwa na kiasi cha 4 million.

Basi bhana kuna siku classmate wangu mmoja alniomba tukutane mtaa flani iv na me nkaenda kweli kumskilza ila kwa bahati mbaya alkua kwenye nyumba ya michezo ya bahati na sibu bas bhana tukapiga story na nkamuomba anielekeze namna ya kubeti alooooo hapo ndo nilipo jiloga mwenyewe kwani kwa siku ile nilkula kama elfu 78 kwa dau la 2500 nkasema mbona pesa apa ni chap chap.

WAKUU kuanzia hapo nilkuwa mkamaria mzuri yaan mpaka kuna time nlikua naacha ofisi yenyewe naenda kupambana na betting niwe mkweli betting imeniharibu vibaya mnoo na kunifilisi kila kitu nlichokuwa nacho apa nlipo sina simu wala ata senti moja.

BETTING imeharibu si tu uchumi wangu ata mahusiano na jamii,ndugu,pamoja na marafiki kwan uaminifu tena na mimi hawana PILI betting imenipotezea hisia za mapenzi, hofu ya mungu pamoja na ladha ya chakula kiufupi tyuu saiv akili na ubongo kila kukicha ni kuwaza betting na nimekuwa nikishinda kwenye nyumba za betting kuanzia asubuhi ad wanafunga yaani kula yangu yenyewe ad nipige ukware nikipata buku nile jero na jero nibaahatishe bahati yangu lakini nmeambulia kuwa mtu wa kujilaumu ad kna mda natamani tyuu bora nife coz I am great loser en dis is painful to me always en am lose hope,light en love.

NOW tumain pekee la kwa nini niishi ni namhurumia mwanangu pamoja na mam yake vip wataishi? ni heri nichechemee hivi hivi huku nikifurahia tabasamu la kachanga kangu though sijui now ako na two month nlichomudu kumnunulia ni kofia mbili tyuuu that too bad to how dis fucking aibu inantafuna.
Kwa Nini unaandika Tyu badala YA TU? Angalia usije kuleft group.
 
Zab 27:1
Bwana ni nuru yangu na wakovu wangu
Mithali 1:10
Mwanangu wenye dhambi wakikushawishi, WEWE usikubali
Hos 4:6
Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa
 
Betting inabidi ujifunze ukiwa huna hela nyingi ili unapofanya majaribio ya kujitoa muhanga kwa timu zenye matokeo ya kushangaza usipigwe pakubwa.

Pia utajifunza tabia mbalimbali za matokeo ya ajabu ya betting kama pale unaomba over 1.5, dakika ya 2 tu linaingia goli la 1, na FT goli linabaki hilo hilo.
Au dakika ya 89 timu uliyoipa ushindi inaongoza 2:0.
Unaenda jikoni kuagiza mguu mzima wa kuku, unarudi mezani unakuta matokeo ni 2:2.

Hii itakuponya magonjwa ya moyo, yaani unakuwa moyo wenye uwezo mzito wa kuhimili mashambulizi ya kila aina.
Ndio maana mtu anayebeti huwa haumizwi na mapenzi, anaona hakuna jipya anacheka tu.
Anhaaa nimecheka sana mpaka mgonjwa aliyejifanya kazimia akaletwa hapa amezinduka.
 
Back
Top Bottom