Kamari imeharibu kila kitu kwenye maisha yangu

Ninawanangu wawili hao kazi yao wanajitenga wanakaa peke yao ukiwasogelea utaskia wanatukana nchi za watu utaskia ufaransa wajinga sana, mara Belgium ndo hamna kitu hawa Portugal yaani sitakaa niwaamini tena
 
Chuo ulichosoma ni SUA Morogoro ila ulipohitimu ulirudi mkoani kwako na kufungua biashara Kilombero (Morogoro). Hali sio, unahitaji msaada.
 
Kamari kamari, kuna mama mmoja ni nesi hospitali fulani pale Dom, aliweka hadi rehani gari yake noah na ikaenda, pesa ya semina akiipata yote inaishia kwenye kamari anabakiwa na nauli tu
Mama🤔? Hadi wanawake Wana uraibu wa kamari
 
mchezo wa wenye hela jamani huu, chukua timu zako mbili weka mzigo wa maaana.
sie wengine utaishia minya pumbuz tuu kama mie hapa nimeweka goal goal mechi ya uturki na austria lakini naona dakika zinaenda tuu austria hafungi
Hapana , apo unakuwa umeongeza uwezekano wa kula na sio uhakika wa kula , ata uweke mech Moja uweke mzigo wa maana utaumia tu , kamari n hatari sana , isije kushawishika ukaweka pesa kubwa mana huchez ww
 
Hapana , apo unakuwa umeongeza uwezekano wa kula na sio uhakika wa kula , ata uweke mech Moja uweke mzigo wa maana utaumia tu , kamari n hatari sana , isije kushawishika ukaweka pesa kubwa mana huchez ww
maisha is about probability sasa wewe weka mechi zako mbili tia mpunga, u will win more than lose. hapa nilishapate hela ya supu. GG imetoka mechi ya turkey
 
Degree holder mwandiko wa kingumbaru
 
We baado janja kabisa sema una mbio afu hujui njia,
Sasa unajiona bitch vile life inakufuck.

Kaza tafuta kazi sasa hata ya 10k/day na uridhike na kipatocuha kazi ya mikono yako.

Mimi naamini pesa inatengenezwa na nguvu, muda na akili. Wala sio kuweka tu pesa mahali wewe ukatulia ati utakuta imekua nyingi lazima upigwe siku yako ikikufikia.

Pole, anza upya.
 
ahsant sana mkuu
 
Tatizo vijana wana tamaaa....kamali ni ya wenye hela...ni njia nyingine waliyobuni kukwapua hela toka kwa maskini
 
Tatizo vijana wana tamaaa....kamali ni ya wenye hela...ni njia nyingine waliyobuni kukwapua hela toka kwa maskini
Ni kama mchele wa kuitia jogoo la pasaka.

Ukitaka kula lazima nawe uliwe kidogo - JK.Msoga.

Vipesa wanavyokula kwa bet ndo mchele ila wao wanaobet ndo Majogoo wa pasaka sasa.
 
Pole mkuu ata mim pia ni muhanga wa hii kitu
Nimepteza ela nyingi sana kwa kucheza casino games ila saiz nashkuru sana nimeweza kuacha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…