Kamati: Kinyesi na Mikojo ya Mifugo ndiyo chanzo cha kufa samaki mto Mara, sio sumu ya maji ya Migodini

Hii ni taarifa mchongo.
 
Muafrika hata afike level gani ya elimu, atabaki kuwa mpumbavu tu.

Wewe fikiria hapa Tz unamtofautishaje Kishimba au Msukuma na Chenge au Lipumba?? Kwa kipi yani??
Vyeti vya kitaaluma na urefu wa C.V zao.
 
Za kuambiwa changanya na zako!!

Kuna maslahi ya umma na maslahi ya watu wachache.

Ni ngumu wakati mwingine kung'amua umma ndio akina nani!!
 
Kwa muktadha huo, ina maana ng'ombe wote wa Mkoa wa Mara wamefunzwa kuwa sehemu pekee ya kujisaidia ni mtoni tu.

Hivyo wakiwa machungani huko huwa wanatunza vinyesi mikojo yao hadi wafike mtoni!

What a joke!
 
Ukitaka kujua uwezo wao uwapime kwa kuwaangalia propesa Lipumba, Mruma na Ossoro...

Mwafrika hata asome vipi huwezi mtofautisha na mshenzi.
Nafuta kauli.

Sema siasa na wanasiasa ktk bara letu la Africa ni kansa na virusi hatari ustawi ya jamii yetu ya kiafrika
 
Hii ni decomposition formula. Vipi kuhusu quantity?.... weka namba ya simu tukutafutie uteuzi
Ha ha ha aaaaa! Namba tena?
Binafsi nilihitaji prof ashushe madini rahisi tunayoweza kuelewa kwa urahisi.

Kutumikia wananchi ni jambo muhimu, lakini jambo hilo liambatane na baraq za Allah.
 
Kinachotafutwa hapa siyo uchafu wa maji ya mto Mara ila ni sababu ya kuondoa wafugaji na mifugo bonde la mto mara tu
 
Kwahiyo kinyesi cha Ng'ombe ndiyo kimesababisha maji kubadilika rangi na kuua samaki mtoni ?
 
Sitaki tena kusoma ikiwa nikisoma kufikia level ya uprofessor ninapoteza Uzalendo na utu kama huyu.
Kifupi tunaomba tume huru iundwe kuchunguza jambo hili na kuchunguza tume hii pia
 
Hapo Kwenye Tani 1.8 za kinyesi Cha Ng'ombe patamu
 
Mtu na pesa zake eeh
Anaweza kuhamisha mito milima na mabonde
Lakini akumbuke Mungu hapokei rushwa
Ujinga kama huu usingetokea kama Baba Yetu wa kisiasa Dkt Magufuli angekuwepo. Ila basi ndiyo hivyo, wananchi wataendelea kufa huku chanzo hatukijui.
 
Alichoficha mwenyekiti wa ripoti na hii timu yake ni kuwa chanzo cha hayo mavi ya ng’ombe kuwa contaminated ni nini???

“The study by Jadavpur University's School of Environmental Studies says the region's groundwater is contaminated with the cancer-causing chemical which gets into paddy through contaminated water. Cattle that feed on contaminated paddy husk and water produce dung that is likely to contain arsenic.”

Inaonekana chemical ambazo ni hatari kutoka migodini zinaingia kwenye mifumo ya maisha ya maeneo husika kama kwenye nyasi na hizo nyasi zikiliwa na hao ng’ombe hatimaye wanazitoa kupitia kinyesi ambacho kinaenda kwenye maji. Ila watoa reporti wamehongwa hela waseme tu uhusika ule wa mwisho. Kumbukeni pia tofauti na Dkt Magufuli aliyekuwa anahakikisha haki za watanzania zinalindwa, Mama yeye anahakikisha haki za muwekezaji zinalindwa kwanza hata kama watanzania itabidi wafe. Hiyo ripoti imetengenezwa kulinda muwekezaji.
 
Najiuliza tu kama huo mto Mara unamwaga maji mahali ambapo ni muhimu sio tu kwa uchumi wa nchi yetu bali hata jirani zetu, je tume haikuona kuwa majibu fulani yanaweza kudraw public attention na hata watu/soko letu kutilia shaka kuwa kuna kitu kinafichwa?

Au tume haikufuata taratibu na kukimbilia kutoa report kwa wanasiasa!!
 
Kumbe 2m ndio imefanya awauze watanzania wenzake..insikitisha sana.

#MaendeleoHayanaChama
 
Uko sawa..ila tambua huo ni mto sio bwawa..manake flow ya maji mapya kila mda so hilo la samadi haliwezi kuwa tatizo..inshu hapo inawezekana ni utando wa mafuta juu ya maji ama kemikali.

Ila kuhusu samadi inayo decompose hapo tumepigwa na kitu kizito.


#MaendeleoHayanaChama
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…