Kamati: Kinyesi na Mikojo ya Mifugo ndiyo chanzo cha kufa samaki mto Mara, sio sumu ya maji ya Migodini

Mi sitak mambo ya kitaalam nawaachia wenyewe, aliyesema ng'ombe mmoja anatoa 25kg za kinyesi kwa siku alimaanisha namba hiyo hiyo au alikosea, na lita 21 za mkojo, ng'ombe? Achana na cyanide tuanzie hapa ambapo hapahitaji report wala paper
Hat mimi sijui mzee wangu; jambo la ajabu ni kuwa maeneo hayo yamekuwa na ngombe wengi kwa miaka mingi sana tena sasa hivi idadi ya ngombe inapungua kutokana na kuwapo watu wengi lakini miaka yote hiyo hawakuweza kutoa kinyeshi cha kujaza mto, kwa hiyo ni jambo la ajabu sana. Vile vile ripoti inaonyesha kama vile ngombe wote huenda kujisaidia mtoni mle jambo ambalo siyo la kawaida.

Kuhusu Cyanide, tuwaache wataalamu halisi watakotusaidia kujua ukweli kamili lakini siyo hawa wataalam uchwara wanaotuona kuwa sisi ni mbuzi wa shughuli wanataka kutupelekesha wanavyotaka.
 
 
Naona profesapesa mayele umekuja kuanika ujinga wako humu..umeuza watz wenzako kwa vipande vya pesa..ili kupotosha ukweli.

#MaendeleoHayanaChama
 
Na wewe ndiyo hujui kabisa. Heavy metals huwa hazisababishi vifo vya ghafla bali huleta madhara ya kiafya kama vile magonjwa ya kansa.
Shida unadhani unaelekeza layman humu..toxicology tumeisoma na tunaijua vyema..kuna acute na chronic effect za chemical..kulingana na amount of dose taken..frequency.

Yote yanaweza pelekea madhara ya muda mrefu ama mfupi..ikiwepo kifo hivyo sio kwamba lazima iwe na madhara ya muda mrefu.

#MaendeleoHayanaChama
 
Wakurya wamekula kichuri kwa miaka nenda rudi hawajafa na kichuri kimsingi ni chuzi la mavi ya mnyama....yaani maprof wa Tanzania mnatisha....
 
"Sasa unaingia mkoa wa Mara"

Mikoa miningine yote ni " Karibu mkoa wa..........'

Ila kwa Mkoa wa Mara unapewa tahadhari, unaingia mkoa wa Kanda Maalum.

Kanda hii ni ya waancholi , wanchira na wanchoka ndiyo kanda ambayo ukiingia basi ukae na adabu yako.

Sasa huku kuna profesa kesha sema hata ng'ombe wa Mara wana kinyesi cha sumu!

Ng'ombe wa Kanda Maalum hao.
 
Unajua hapa lazima tuangalia haya mambo kama watu wenye fikra

Huenda sio kweli kwamba kinyesi pekee ndio kimesababisha madhara

Ila chochote kikizidi ni sumu..., Mbolea / kinyesi kikiwa kingi kwenye maji kinapelekea algae growth kubwa ambayo inapunguza oxygen concetration...

Hata wewe hapo maji ingawa ni mazuri ukinywa mengi zaidi unakufa...

Ndio maana ecosystem inahitajiwa kila kitu kwa kiwango.

Everything in moderation ili mambo ya-balance
 
Hakuna lolote ni rushwa tu inasumbua
 
Hakuna lolote ni rushwa tu inasumbua
Kwa yeye kuchukua au kutokuchua Rushwa haimaanishi kwamba concetrated animal farming inayopelekea waste nyingi kuzalishwa katika eneo dogo ni environmental hazard inayoharibu vyanzo vya maji....

Ila hii sio mbaya kwenye free grazing ambapo concentration ya wanyama huwa sio kubwa kama kwenye Concentrated Animal Farming
 
Acha hizoo...!
Hao ng'ombe wameanza leo kufaulisha kinyesi mto Mara?
 
"... rubish rubish ... "alisikika mdau mmoja akikosoa jambo mahali fulani

Input = output (majani walayo yana sumu, hivyo hivyo na kinyesi watoacho kina sumu,.. na nyama yao huenda ikawa na vimelea vya sumu)
 
Nimesoma juujuu heading nikajua ni kamati ya kinyesi na mikojo
 
Pumzika kwa amani Jiwe. Haya yote yangekuwa wazi kwa maslahi ya wanyonge [emoji22] [emoji22] [emoji41] [emoji41]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…