Kama wewe ni mfugaji utakuwa umeelewa ila kamq ni "mtafiti" wa ufugaji, uswahili utakupotoshaAtakua nani kama sio ng'ombe?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kama wewe ni mfugaji utakuwa umeelewa ila kamq ni "mtafiti" wa ufugaji, uswahili utakupotoshaAtakua nani kama sio ng'ombe?
Hat mimi sijui mzee wangu; jambo la ajabu ni kuwa maeneo hayo yamekuwa na ngombe wengi kwa miaka mingi sana tena sasa hivi idadi ya ngombe inapungua kutokana na kuwapo watu wengi lakini miaka yote hiyo hawakuweza kutoa kinyeshi cha kujaza mto, kwa hiyo ni jambo la ajabu sana. Vile vile ripoti inaonyesha kama vile ngombe wote huenda kujisaidia mtoni mle jambo ambalo siyo la kawaida.Mi sitak mambo ya kitaalam nawaachia wenyewe, aliyesema ng'ombe mmoja anatoa 25kg za kinyesi kwa siku alimaanisha namba hiyo hiyo au alikosea, na lita 21 za mkojo, ng'ombe? Achana na cyanide tuanzie hapa ambapo hapahitaji report wala paper
Musoma. Kamati maalum ya kitaifa iliyoundwa na serikali kuchunguza mabadiliko ya maji ndani ya mto Mara, imetoa taarifa ya chanzo cha mabadiliko katika mto huo yaliyosababisha maji kuwa meusi na kutoa harufu, huku samaki wakifa ambapo chanzo kimeelezwa kuwa ni shughuli za binadamu pamoja na nguvu za asili.
Akitoa matokeo ya uchunguzi leo Jumamosi Machi 19, 2022 mjini Musoma, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Profesa Samuel Manyele amesema kuwa hali hiyo imetokana na kuwepo kwa kiwango kikubwa cha kinyesi cha mifugo mtoni pamoja na uozo wa mimea ndani ya mto hasa mimea vamizi kama vile magugu maji na matete.
Amesema kuwa hali hiyo ilisababisha kupungua kwa kiasi kikubwa kiwango cha oksijeni ndani ya mto na hivyo maji kubadilika rangi na kuwa na harufu mbaya huku samaki wakikosa chakula na hivyo kusababisha vifo vyao.
Hata hivyo, amekanusha picha zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii zilizokuwa zikionyesha samaki wakiwa wamekufa kwa wingi, akisema sio kutoka mkoani Mara.
Amesema kuwa kwa mujibu wa uchunguzi waliofanyana walibaini kuwa mabadiliko hayo ni matokeo ya mvua kubwa iliyonyesha ghafla kwa muda mfupi katika kipindi cha mwezi huu hivyo kutibua uchafu uliokuwa umejikusanya chini ya mto kwa muda mrefu.
"Mvua zingeendelea kunyesha hali hii ingeisha kwani uchafu ungetiririshwa lakini kwa vile mvua zimenyesha na kukatika ghafla ina maana uchafu ule unatoka taratibu na hii hali inaweza kudumu kwa zaidi ya miezi mitatu hadi minne endapo mvua hazitanyesha hapa katikakati," amesema.
Profesa Manyele amesema kuwa mto huo umeathiriwa kuanzia katika kijiji cha Marasibora wilayani Rorya na kijiji cha Wegero wilayani Butiama huku akisema kuwa mgodi wa dhahabu wa Barrick North Mara hauhusiki na uchafuzi huo.
"Mgodi upo mbali sana na maeneo yaliyoathirika na hata kama uchafu unaozalishwa mgodini pale ungezidishwa mara ishirini na kumwagwa mtoni maji yasingebadilika rangi wala kuwa katika hali iivyo sasa na maji ya mto kelekea kule mgodini ni masafi na hayana shida yoyote," amesema.
Amesema kuwa wamebaini uwepo wa kinyesi cha ng'ombe zaidi ya tani 1.8 milioni pamoja na mkojo wa ng'ombe lita 1.5 bilioni uchafu uliotokana na kuwepo kwa ng'ombe zaidi ya laki 3 waliokuwepo katika eneo oevu la mto Mara kwa kipindi cha miezi minane mwaka jana wakati wa kiangazi.
"Ng'ombe mmoja ana toa kilo 25 za kinyesi kwa siku moja na mkojo lita 21 kwa siku kwahiyo ukizidisha kwa idadi hiyo ya ng'ombe mara miezi minane utapata kiwango hicho na hapo bado hatujaweka kinyesi na mkojo wa kondoo, mbuzi na punda," amesema.
Akizungumza baada ya kupokea taarifa hiyo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Suleiman Jafo ametoa muda wa siku mbili kwa kamati hiyo kuandaa taarifa kamili yenye mpango kazi juu ya nini kifanyike na muhusika ni nani kisha taarifa hiyo ikabidhiwe kwake kwaajili ya utekelezaji.
"Hii taarifa imenipa faraja baada ya uchunguzi kubaini kuwa hakuna kemikali mtoni maana kama kungekuwa na kemikali hii ingekuwa ni habari mbaya sana lakini taarifa hii inaonyesha kuwa tuna kazi kubwa sana ya kufanya ili mto uweze kuendelea kuwepo na tusipochukua hatua za haraka mto unaweza kupotea," amesema Jafo.
Chanzo: Mwananchi
Pia soma;
1).Vifo vya Samaki Mto Mara: Kamati ya Dharura yaundwa kuchunguza Samaki wanaodaiwa kufa kwa Sumu
2). Madai ya sumu Mto Mara kutoka migodini, wananchi wazuiwa kutumia maji, kula samaki, uvuvi, Serikali yatoa tamko
View attachment 2157025
Au labda mkuu Bams anataka tuamini kuwa huko mto Mara kuna deposit kubwa ya mafuta ambayo hayajachimbwa mpaka yanatiririka yenyewe kuelekea mtoni!Mkuu hebu angalia video clip hii nafikiri inaweza kukusaidia kidogo! Then wasingizie ng'ombe wa wakurya.
View attachment 2158436
Naona profesapesa mayele umekuja kuanika ujinga wako humu..umeuza watz wenzako kwa vipande vya pesa..ili kupotosha ukweli.Siyo porojo ndugu zangu. Shida ya wengi, uelewa hawana, hawafanyi utafiiti hata mdogo kabisa, lakini wanajifanya wanajua kila siku.
Kuna watu, leo hii hata ng'ombe wakifa Mpwapwa, wakaambiwa wamekunywa maji ya sumu yanayotoka mgodi wa dhahabu Geita, watakubali, na kusambaza taarifa hizo kwa nguvu zao zote. Tatizo kubwa ni ujinga katika mambo mengi na kutotambua kuwa ni wajinga.
Shida unadhani unaelekeza layman humu..toxicology tumeisoma na tunaijua vyema..kuna acute na chronic effect za chemical..kulingana na amount of dose taken..frequency.Na wewe ndiyo hujui kabisa. Heavy metals huwa hazisababishi vifo vya ghafla bali huleta madhara ya kiafya kama vile magonjwa ya kansa.
Nimefuga na bibi kwa zaidi ya miaka 3 hizi kilo 25 na mkojo lita 21 ni uongo ukiopitiliza.Ng'mbe mmoja kinyesi 25kg kwa siku + 21 Lita za mkojo???????????? Sijawahi kufuga lakini hapa....Ngumu kumeza
Mbona inakinzana sana naya prof.
Hakuna lolote ni rushwa tu inasumbuaUnajua hapa lazima tuangalia haya mambo kama watu wenye fikra
Huenda sio kweli kwamba kinyesi pekee ndio kimesababisha madhara
Ila chochote kikizidi ni sumu..., Mbolea / kinyesi kikiwa kingi kwenye maji kinapelekea algae growth kubwa ambayo inapunguza oxygen concetration...
Hata wewe hapo maji ingawa ni mazuri ukinywa mengi zaidi unakufa...
Ndio maana ecosystem inahitajiwa kila kitu kwa kiwango
Kwa yeye kuchukua au kutokuchua Rushwa haimaanishi kwamba concetrated animal farming inayopelekea waste nyingi kuzalishwa katika eneo dogo ni environmental hazard inayoharibu vyanzo vya maji....Hakuna lolote ni rushwa tu inasumbua
Acha hizoo...!Unajua hapa lazima tuangalia haya mambo kama watu wenye fikra
Huenda sio kweli kwamba kinyesi pekee ndio kimesababisha madhara
Ila chochote kikizidi ni sumu..., Mbolea / kinyesi kikiwa kingi kwenye maji kinapelekea algae growth kubwa ambayo inapunguza oxygen concetration...
Hata wewe hapo maji ingawa ni mazuri ukinywa mengi zaidi unakufa...
Ndio maana ecosystem inahitajiwa kila kitu kwa kiwango.
Everything in moderation ili mambo ya-balance
Nchi imerudi kwenye rushwaAcha hizoo...!
Hao ng'ombe wameanza leo kufaulisha kinyesi mto Mara?
Pumzika kwa amani Jiwe. Haya yote yangekuwa wazi kwa maslahi ya wanyonge [emoji22] [emoji22] [emoji41] [emoji41]Musoma. Kamati maalum ya kitaifa iliyoundwa na serikali kuchunguza mabadiliko ya maji ndani ya mto Mara, imetoa taarifa ya chanzo cha mabadiliko katika mto huo yaliyosababisha maji kuwa meusi na kutoa harufu, huku samaki wakifa ambapo chanzo kimeelezwa kuwa ni shughuli za binadamu pamoja na nguvu za asili.