Kamati: Kinyesi na Mikojo ya Mifugo ndiyo chanzo cha kufa samaki mto Mara, sio sumu ya maji ya Migodini

Acha hizoo...!
Hao ng'ombe wameanza leo kufaulisha kinyesi mto Mara?
Tunaongelea mambo mengi sana kwa wakati mmoja..

Kama kinyesi / mbolea inaweza kupelekea vifo vya viumbe hai kwenye maji haimaanishi kwamba ndicho kilichotokea Mara..., Na kama sicho kilichotokea Mara haimaanishi kwamba wingi wa mbolea / samadi kwenye vyanzo vya maji hakuwezi kuleta madhara...

Tuongelee vitu katika utenganisho ama sivyo tunaweza kujikuta tunakataa theory fulani sababu haikutokea sehemu fulani wakati hio theory ina ukweli (inaweza kutokea)
 
Kwamba ng'ombe mara wanakula sumu ndiyo maana kinyesi kina sumu?
Sumu ni nini ?

Mbolea kwenye mimea ni chakula, mbolea kwenye maji pia ni chakula cha algae ambacho baadhi ya samaki mfano Tilapia wanakula..., sasa mbolea ikizidi algae wakazidi wakati hakuna jua la kutosha (photosynthesis) ili algae watengeneze oxygen dissolved oxygen kwenye maji inapungua..., Oxygen ikipungua nadhani you know what will happen
 
Mimi pia nimeshangaa sana kusoma ripoti hii ya ajabu ya Profesa

Na mimi kiasili natoka jamii ya wafugaji kanda ya ziwa

Ila hili la ng'ombe kunya kilo 25 na kukojoa mkojo lita 21 kwa siku HAKIKA NI UONGO wa mchana kweupe!

Hakuna ng'ombe wa kunya kilo 25 na mkojo lita 21 kwa siku huku kanda ya ziwa. Huyu profesa ni mwongo. Kuna kitu hakiko sawa, wanaficha jambo hawa!!

Hawa ng'ombe wamekuwa ni tembo wanye mavi ya namna hiyo kwa siku?

Na ina maana profesa huyu anataka kutuambia kubwa hawa ng'ombe walikuwa wananyea mavi na kukojolea mkojo huo ndani ya mto kila siku?

Na hizo mvua ndo zimeanza kunyesha mwaka huu huko Mara? Miaka mingine hakujawahi kuwa na mvua? Kwanini hakukutokea maafa ya namna hii?

Na hao ng'ombe 300,000 tu ndiyo wameanza kufugwa mwaka huu huko Mara?

Ni kweli kabisa hii ripoti ni ya uongo. Ni ya kupika na kuuficha ukweli halisi ambao wameuona.

Kuna mawili kuihusu kamati hii;

AIDHA
Hawana utaalamu wa kuchunguza jambo hili

AU

Kwa sababu aidha kuhongwa na wahalifu hao, wameamua kuuficha ukweli wa jambo hili kwa maslahi yao na ya wahalifu hao wa mazingira!
 
Labda uniambie Huwaga watu wanabeba malori ya kinyesi cha ngombe na mikojo kwenda kumwaga kwenye ule mto ila kinyesi cha ng'ombe wa malisho wa kawaida hawa wawe wengi vipi kamwe hakiwezi kuleta shida... maji yanamove muda wote accumulation ya kinyesi mpaka kuleta hio athari inatokea wapi??? Ni upuuzi wa hali ya juu wazri kupokea na kukubali ripoti ile
 
Sijibu issue iliyotokea mto Mara, najibu watu wanaosema Kinyesi hakiwezi kuleta madhara..., Ndio maana nikasema kuanzia mwanzo huyu Bwana apingwe specifically kulingana na sehemu aliyofanya hio Kazi ila sio kupinga uwezekano wa jambo kama hilo kutokea.... Na hapa nilikuwa najibu Uzi kwamba Kinyesi cha Mifugo ya Mara kina Sumu....
 
Watanzania kweli watawala wanatuona wasenge na mazoba hivi kweli
 
Kwa hiyo ni kwa ajili ya Mara pekee?
 
Wananchi hapo wangemnywesha kwanza hayo maji kama kweli hayana sumu,na kiongozi wa nchi hana habari ...........................
 
Kwa hiyo ni kwa ajili ya Mara pekee?
Again siongelei kilichotokea Mara naongelea kama jambo kama hilo linaweza kutokea..., In short animal waste ni moja ya chanzo kikubwa sana katika uharibu wa vyanzo vya maji duniani (ingawa hii inaletelezwa sana na concentrated animal farming) kwenye free grazing hili sio tatizo kubwa as kinyesi kinakuwa absorbed kama mbolea hata kabla ya kufikia water bodies
 
Sawa mkuu
 
Ni up.umbavu wa hali juu kufikiria kuwa eti kuna sumu za mgodini zingesababisha samaki kufa mto Mara. Ni fikra za kijinga kabisa kutoka kwa wajinga wasiojua chochote kuhusiana na shughuli za mineral processing...
Comment ya mchongo.
 
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema, mtu akikuambia mambo ya ovyo, na wewe unajua ni ya ovyo, na yeye anajua amakumbia ya ovyo, basi mtu huyo amekudharau sana.
 
Umekazana ni "Matusi kwa Rais,"

Mimi nakwambia hayo ni Matusi kwa wananchi ambao wanategemea mto huo kwenye maisha yao ya kila siku.

Rais wako ategemei chochote kutoka kwenye huo Mto.


Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa mkuu wananchi hata wakionewa hawana cha kufanya kamati imetoa majibu ya kipuuzi wakiamini Rais ni wa kumtania na kumchukulia poaa...!! Na kweli ametaniwa na kuchukulia poa amebaki anashangaa tuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…