Kamati: Kinyesi na Mikojo ya Mifugo ndiyo chanzo cha kufa samaki mto Mara, sio sumu ya maji ya Migodini

Kamati: Kinyesi na Mikojo ya Mifugo ndiyo chanzo cha kufa samaki mto Mara, sio sumu ya maji ya Migodini

Musoma. Kamati maalum ya kitaifa iliyoundwa na serikali kuchunguza mabadiliko ya maji ndani ya mto Mara, imetoa taarifa ya chanzo cha mabadiliko katika mto huo yaliyosababisha maji kuwa meusi na kutoa harufu, huku samaki wakifa ambapo chanzo kimeelezwa kuwa ni shughuli za binadamu pamoja na nguvu za asili.

Akitoa matokeo ya uchunguzi leo Jumamosi Machi 19, 2022 mjini Musoma, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Profesa Samuel Manyele amesema kuwa hali hiyo imetokana na kuwepo kwa kiwango kikubwa cha kinyesi cha mifugo mtoni pamoja na uozo wa mimea ndani ya mto hasa mimea vamizi kama vile magugu maji na matete.

Amesema kuwa hali hiyo ilisababisha kupungua kwa kiasi kikubwa kiwango cha oksijeni ndani ya mto na hivyo maji kubadilika rangi na kuwa na harufu mbaya huku samaki wakikosa chakula na hivyo kusababisha vifo vyao.

Hata hivyo, amekanusha picha zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii zilizokuwa zikionyesha samaki wakiwa wamekufa kwa wingi, akisema sio kutoka mkoani Mara.

Amesema kuwa kwa mujibu wa uchunguzi waliofanyana walibaini kuwa mabadiliko hayo ni matokeo ya mvua kubwa iliyonyesha ghafla kwa muda mfupi katika kipindi cha mwezi huu hivyo kutibua uchafu uliokuwa umejikusanya chini ya mto kwa muda mrefu.

"Mvua zingeendelea kunyesha hali hii ingeisha kwani uchafu ungetiririshwa lakini kwa vile mvua zimenyesha na kukatika ghafla ina maana uchafu ule unatoka taratibu na hii hali inaweza kudumu kwa zaidi ya miezi mitatu hadi minne endapo mvua hazitanyesha hapa katikakati," amesema.

Profesa Manyele amesema kuwa mto huo umeathiriwa kuanzia katika kijiji cha Marasibora wilayani Rorya na kijiji cha Wegero wilayani Butiama huku akisema kuwa mgodi wa dhahabu wa Barrick North Mara hauhusiki na uchafuzi huo.

"Mgodi upo mbali sana na maeneo yaliyoathirika na hata kama uchafu unaozalishwa mgodini pale ungezidishwa mara ishirini na kumwagwa mtoni maji yasingebadilika rangi wala kuwa katika hali iivyo sasa na maji ya mto kelekea kule mgodini ni masafi na hayana shida yoyote," amesema.

Amesema kuwa wamebaini uwepo wa kinyesi cha ng'ombe zaidi ya tani 1.8 milioni pamoja na mkojo wa ng'ombe lita 1.5 bilioni uchafu uliotokana na kuwepo kwa ng'ombe zaidi ya laki 3 waliokuwepo katika eneo oevu la mto Mara kwa kipindi cha miezi minane mwaka jana wakati wa kiangazi.

"Ng'ombe mmoja ana toa kilo 25 za kinyesi kwa siku moja na mkojo lita 21 kwa siku kwahiyo ukizidisha kwa idadi hiyo ya ng'ombe mara miezi minane utapata kiwango hicho na hapo bado hatujaweka kinyesi na mkojo wa kondoo, mbuzi na punda," amesema.

Akizungumza baada ya kupokea taarifa hiyo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Suleiman Jafo ametoa muda wa siku mbili kwa kamati hiyo kuandaa taarifa kamili yenye mpango kazi juu ya nini kifanyike na muhusika ni nani kisha taarifa hiyo ikabidhiwe kwake kwaajili ya utekelezaji.

"Hii taarifa imenipa faraja baada ya uchunguzi kubaini kuwa hakuna kemikali mtoni maana kama kungekuwa na kemikali hii ingekuwa ni habari mbaya sana lakini taarifa hii inaonyesha kuwa tuna kazi kubwa sana ya kufanya ili mto uweze kuendelea kuwepo na tusipochukua hatua za haraka mto unaweza kupotea," amesema Jafo.

Chanzo: Mwananchi

Pia soma;

1).Vifo vya Samaki Mto Mara: Kamati ya Dharura yaundwa kuchunguza Samaki wanaodaiwa kufa kwa Sumu

2). Madai ya sumu Mto Mara kutoka migodini, wananchi wazuiwa kutumia maji, kula samaki, uvuvi, Serikali yatoa tamko
View attachment 2157025
1. Walipima wapi, lini na ngombe wangapi ili kujua kila ngombe moja ktk hao malaki anakunya mv uzito wa nusu ya mfuko wa cement?

2. Lita hizo za mkojo na mv zilitoka wapi kama muda husika ulikuwa kiangazi hakuna mvua?

3. Miaka yote kabla ya tukio hili la ghafla kulikuwa hakuna ngombe?

4. Kama walikuwepo kwanini ngombe waanze ghafla kunya na kukojoa kiasi hicho muda wa kiangazi tu na sio masika? Waliugua kipindupindu?
 
Wewe Ndio Mdau ambao JF wanenileta kukusoma huku?
 
Kisayansi tunaelewa kinyesi ni moja ya chakula cha samaki.

Pia kinyesi kikioza ndani ya maji huzalisha wadudu ambao huliwa na samaki.

Sasa hii ya kinyesi kuchafua maji na kuua samaki imekua ni mpya.
Ndugu yangu kwanza watu watofautishe mto na bwawa pale mto mara maji yanatiririka sasa hiyo kinyesi kina resistance gani kuweza kutuama na kuweza kutengeneza sumu. Hii haiwezekani mimi sikubaliani na hii ripoti
 
Kisayansi tunaelewa kinyesi ni moja ya chakula cha samaki.

Pia kinyesi kikioza ndani ya maji huzalisha wadudu ambao huliwa na samaki.

Sasa hii ya kinyesi kuchafua maji na kuua samaki imekua ni mpya.

Serikali nzima haiwezi kujitenga na hii kadhia.

Hakuna kisingio hapa.

Taarifa iliyotolewa haiingii akilini.
 
Vibaka kazini👇😁😁😁
AA-cq1.jpg
AEm_LX.jpg
 
Hao watu wa mara vinyesi vyao vipimwe tu
Maana kama majibu ya tume ndiyo Haya
Basi kinyesi toka mara unaweza zalishia bomu la nyuklia

Ova
 
SERIKALI yetu inapenda utani sana..
Kanda ya Ziwa.. ugonjwa wa CANCER umeongezeka sana.. ikumbukwe maji kwenye kwenye mito na hata pembezoni mwa ziwa Victoria hutumika majumbani kama usafi na hata kupikia chakula..
Mwezi wa Nne nitakuwepo Msoma, nitatufuta kifaa kisafi nitaosha na distilled water nitachota maji mtoni na ziwani nitapeleka kiwanda flani (siri) wanayo analyser.. Na tutacheki..
pH kwenye maji
Colour
Sulfur conc
Mercury ipo kiasi gani
Cynide level
Bila hivyo watu watakuja kufa ovyo kwa kutumia chemical za ajabu kwenye maji.
Kinyesi hakiwezi kuwa sumu.. Hata sikumoja.. Ni biological products ambayo kwanza inarutuba.. Ndio maana inatumika kama mbolea
 
cha juu mkuuu na huko kanda ya ziwa kuna kansa kwa kwenda mbele hata ocean road wagonjwa wengi ni wa kanda ya ziwa ,anyway kamati imekula kwa urefu wa kamba yake bana
Aliyeiunda tuma nae kayakubali majibu ya tume?

KILA M1 ALE KWA UREFU WA KAMBA YAKE
 
Yaani ningekuwa Madarakani mimi wangenikoma!! Mjue sasa watanzania hili ndo tatizo la kuingia Madarakani kwa uchawi uchawi!!...Wooote hawa waliokubali utoporo huu hawajasoma vizuri hawa madarasa yakawakaaa!!

Ila waliingia madarakani kwa uchawi!!!.. hawa dini waliweka pembeni ........na mchawi wenu mkubwa aliye waroga mpaka mkalala fofofofofofo ni Dini za yesu mzungu baaaasi!....Naema hamchomokimtake msitake labda mfuate yangu haya!
 
Sasa Rasmi nimeamini Magufuli amefarikii...!!! Yani mpaka waziri anakubali kupokea rpoti ya kimakuuuu hiii...shwain sanaa

Kama ile stori ya maji ya kufulia umeme na matumiz ya makazi kukaushwa na ng’ombe kwa kunywa maji liter 450kwa siku
 
Back
Top Bottom