Unavyojibu hoja hapa inaonyesha kuwa unaandika mambo usiyokuwa na uelewa nayo bali umewahi kuambiwa nusu nusu tu. Ni kawaida ya watu wanaojua mambo nusu nsusu kutaka kujionyesha ni wajuzi zaidi ya uwezo wao kwa kujitutumua.
1. Unaponiuliza mimi kama ninajua chemical reaction ya cyanide ni wazi kuwa hata wewe mwenyewe hujui unauliza nini iwapo unashindwa kuelewa kuwa chemical reaction yoyote inatokana na kuwepo kwa reactants mbili au zaidi, na sasa hivi hujasema unataka chemical reaction ya cyanide na reactant gani nyingine unategema nikujibu nini. Matokeo ya ujuaji nusu huo.
2. Cyanide inayotumika kwenye migodi ya dhahabu ni Sodium Cyanide, na hiyo siyo radioctive kabisa kwani inatokana na stable isotope za sodium Na23. Zile isotope mbili ambazo radioactive hazitumiki kwenye cyanide, moja Na22 (halflife approx 2.5 years) inatumika kwenye tomography, na ile nyingine Na24 (halfl ife aprox 1 day) hutumika kutengeza Magnesium. Unapouliza kuelezwa half life ya cynide, ni dalili ama kutokujua unalosema au kulijua nusunusu. Half life inapimwa kwenye radioactive materials tu, sasa unaielataje hapa kwenye mjdala wa cyanide. Ni cyanides chache sanaambazo ni radioactive, mfano Potassium Cyanide lkakini hizo siyo zinazotumika kwenye leacing
3. Kuna watu wameshaweka hapa references mbalimbali kutoka sehemu mbalimbali za dunia zinazoonyesha kuwa byproducts za gold leaching kwa kutumia Sodium cynide ni sumu kwa wanyama na samaki. Haiwezekani wote walioandika report na papers hizo wakawa hawajui ispiokuwa wewe ambaye hujatuonyesha paper yoyote uliyoandika ikatambuliwa duniani kuwa ni salama kutumia sodium cyanide umbali wa km 2.5 kutoka mtoni kwa sababu ya "half-life" (Approximate distance ya kutoka North Mara mgodini hadi mtoni ni kama km 2.5). Kuna mahakama Idaho iluzia mgodi uliokuwa takriban km 5 kutoka mtoni kwa sababu hiyo hiyo.
4. Elewa kuwa watu wanapozungumzia environmental poisoning, siyo kuwa wanasema ukimwaga siku moja tu basi utasababisha vifo hivyo, la hiyo ni cummulative effect ya muda kadhaa; wakati mwingine nusu mwaka na wakati mwingine hata miaka mitano au zaidi. Leo tunapuzungumza global warming kutokana na mafuta ya petroleum, siyo kuwa ilianza leo, ni cumulative kwa muda mrefu.