Kamati kuu CCM yamtosa Hussein Bashe, adaiwa si raia wa Tanzania

Mwenye kujua SHERIA naomba anijuze: Mfano nimezaliwa Tanzania maisha yangu yote ni hapo hapo TZ kuanzia kielimu hadi kikazi nikaowa TZ na mwenzi wangu ni mtu wa TZ nikizaa watoto watakuwa ni raia wa wapi? nami ni raia wa wapi ikiwa baba yangu ni MGHANA mama yangu ni Mtanzania??
Nitafuata uraia wa kuzaliwa au wa Baba au wa Mama??

KWA SAababu Tanzania Hakuna mtu anyehakiki kumbukumbu kama hizo, basi wewe unaweza kukaa na kupata haki zako zote kama Mtanzania na wala kutakuwa hakuna mtu atakekusumbua, lakini utakapo ingia kwenye mambo ya siasa basi ndio kumbukumbu zako zivutwa ba kuwekwa mezani
PAMOJA NA HAYO YOTE, NIKIJIBU SWALI LAKO LA HAPO KWENYE ZAMBARAU NI KUWA, KAMA UKO KWENYE SITUATION ULIYOITAJA BASI SHERIA INAKUPASA UNAPOFIKISHA UMRI WA MIAKA KUMI NA NANE (18), UENDE KUUKANA URAIA MMOJA KATI YA HIZO TATU ULIZONAZO, MAANA KAMA BABA NI MGHANA NA SAY MAMA NI MZAMBIA NA WEWE UMEZALIWA TANZANIA, SHERIA YA TANZANIA INAKUTAMBUA KUWA UNA HAKI YA KUWA RAIA KATIKA NCHI ZOTE HIZO TATU, KWA HIYO UKIFIKA 18 INAKUBIDI UIAMBIE SERIKALI KUWA KATIKA RAIA ZOTE HIZO TATU WEWE UTAKUWA RAIA WA....
 
Kuna habari kuwa Hussein Bashe ataongea na waandishi leo..! Je kasema nini...? Vilevile mliopo kwenye press conference hiyo mnaweza kumuuliza kuhusu ripoti hizi mbili zinazotatanisha..

1. Akihojiwa na BBC swahili alisema kuwa yeye ni raia kwakua mama yake ni mtanzania (si msomali) na baba yake ndie msomali kwahivyo amerithi uraia wa mzazi mmoja wapo (mama yake) ambaye ni mtanzania na hana haja ya kuukana uraia wa baba.

2. Gazeti la leo la Mwananchi linadai alishaukana uraia wa Somalia kwenye mahakama ya kivukoni.

Lipi kweli kati ya haya mawili?

Mawazo Matatu;

Naungana na wewe,kwa maskio yangu nimesikia Bashe akisema anashangaa kuambiwa sio raia kwa sababu Mama yake ni mzaliwa Tabora na kisheria akasema kama mmoja wa wazazi wako ni raia wa TZ hupaswi kuomba uraia ukifikisha miaka 18 kwani unakuwa unarithi moja moja uraia wa TZ kutoka kwa mmoja wa wazazi wako!

Lkn jana hiyo hiyo akaongea na waandishi wa habari na kuonyesha hata viapo vyake alivyo apa mahakamani Dar kuukana uraiawa Somalia;kisheria ina maana ni kweli kuwa wazazi wake wote 2 hawakuwa Raia wa TZ bali Wasomali alipokuwa anazaliwa Bashe na ndiyo maana aliapa kuukana uraia wa wazazi wake!

Ni kauli 2 tata tena tofauti toka kwa mtu huyu Bashe;hii naanza kuunga mkono kauli ya Makamba kuwa kijana huyu ni"vuvuzela"wa uraia;iweje uende kuapa mahakamani na kuukana usomalia kama wewe mmoja wa wazazi wako ni raia kipindi kile unazaliwa?Kama wewe ni Riai wa TZ why ukaape ili kuukana U-somalia na kuupata U-TZ wakati wewe ni raia tayari wa KUZALIWA wa TZ uliye urithi toka kwa mama yako aliyekuwa RAIA wakati Bashe anazaliwa?

Uhamiaji mchunguzeni kijana huyu Bashe;anajichanganya sana kwenye habari zake!
 
Mkuu Malafyale, Ugonile!
Nakubaliana na maelezo yako,inabidi kwanza tukae kimya ili tuone kwa dhati ukweli wa habari hii,kama inavyoshughulikiwa na vyombo vya sheria na Idara ya Uhamiaji.Hapo awali baadhi ya watu hapa wamekuwa wanashangilia habari hii,labda kwa ushabiki wa vyama vya kisiasa au tabia tu ya kupenda habari mvunjiko (habari mpya).Nimesoma Magazeti mbalimbali ya Leo (Jumanne) na kusikiliza mahojiano ya Hussein Bashe na watu wa BBC na nimeona wazi kuwa kuna habari zinakinzana.

Katika Mahojiano na watu wa BBC,Bwana Bashe amesema wazi kuwa Baba yake Mzazi ni raia wa Somalia aliyehamia hapa muda mrefu,lakini Mama yake mzazi ni mzaliwa wa Tabora,kwa maana hiyo aliweza kupata Uraia wa Tanzania kwa kurithi upande wa Mama yake.Nimejaribu kuipata clip ya Mahojiano yale ili niilete hapa lakini nimeshindwa,kwa wanaotaka kuisikia na kuipata clip hiyo watembelee wavuti.com au wawasiliane na Da' subinukta77.

Kinachonishangaza zaidi Gazeti la Mwananchi na Tanzania Daima wote kwa pamoja wametoa vielelezo vinavyoonyesha Bwana Bashe ana Hati ya Uraia number S/N 312 iliyotolewa tarehe 10/August/2009,Ikumbukwe kuwa kuna Tofauti kati ya Cheti cha kuzaliwa na Hati ya Uraia,kutokana na Gazeti la Mwananchi ina maana si kweli kwamba Mama Mzazi wa Bwana Bashe ni Raia wa kuzaliwa wa Tanzania,ina maana Bashe aliomba Uraia wa Tanzania na ndio maana akakabidhiwa hiyo Hati yenye # S/N 312. Kwa kuwa vitu hivyo vipo kwenye maandishi Ukweli wa habari nzima utajulikana.Lakini kutokana na maelezo ya Bashe kupitia BBC kuna mgongano mkubwa wa maelezo unaotia Utata suala zima la Uraia wake.
Masuala ya Utata wa Uraia sio mageni katika majukwaa ya siasa za Tanzania,itakumbukwa kuwa mwaka 2003 Viongozi wa juu wa kada mbalimbali walivuliwa Uongozi wao kwa sababu Uraia wao ulikuwa na Utata,Miongoni mwa Viongozi hao ni 1);Jenerali Ulimwengu,ambaye aliwahi kuwa mshauri wa Rais,Mkuu wa Wilaya na baadaye Mwenyekiti wa Habari cooperation 2);Moudline Castiko aliyekuwa Njumbe wa CC na Katibu mwenezi wa CCM -Zanzibar 3);Anatory Amani aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoani Kagera.4);Timothy Bandora ambaye alikuwa Balozi na Mwajiriwa wa Wizara ya mambo ya Nje (MOFA).Ni mwaka jana tu pia kumekuwa na Utata wa Uraia wa Catherine Peter Nao,ambaye kama Hussein nae ni mjumbe wa NEC zanzibar.

Tuachie vyombo vya sheria tutaujua ukweli kuhusu Uraia wa Ndugu Bashe.
Mkuu usishtuke salaam yangu ya kinyakyusa,nina mizizi na huko Kyela.Nakumbuka kuwa kamanda wa Vijana CCM kwenye uzinduzi wa Chama hicho 1977.
 
Nawashangaa nyote kwa kutobaini kitu gani hasa kilitokea. Hzi hati zote ni fake -- kwa maana kwamba zilitolewa hivi karibuni tu na kuwa -back-dated -- kwa malipo (rushwa) of course -- ili Bashe atimize azma yake ya kupanda katika medani za kisiasa za nchi hii. Na unaweza ku-guess nani yuko behind all this -- RA of course.

Mambo haya yako sana katika upatikanaji wa passport lakini huwa hayajulikani hadi issue kama ya Bashe izuke ndiyo suala huwekwa chini ya microscope kali. Maafisa wa uhamiaji, hata yule hakimu aliyesimamia kiapo itabidi watoe maelezo. Hata huyo RA kama serikali ikitaka, au kama ina ubavu wa kuuweka uraia wake under microscope kali, tutayaona madudu ya ajabu tu yalioyafanywa na maafisa husika wa wa serikali.
 
ukweli ni kwamba serikali ikiamua inweza, ila bahati mbaya tu ni kwamba inaamua mara chache sana!!!
 
Nawashangaa nyote kwa kutobaini kitu gani hasa kilitokea. Hzi hati zote ni fake -- kwa maana kwamba zilitolewa hivi karibuni tu na kuwa -back-dated -- kwa malipo (rushwa) of course -- ili Bashe atimize azma yake ya kupanda katika medani za kisiasa za nchi hii. Na unaweza ku-guess nani yuko behind all this -- RA of course.

Mambo haya yako sana katika upatikanaji wa passport lakini huwa hayajulikani hadi issue kama ya Bashe izuke ndiyo suala huwekwa chini ya microscope kali. Maafisa wa uhamiaji, hata yule hakimu aliyesimamia kiapo itabidi watoe maelezo. Hata huyo RA kama serikali ikitaka, au kama ina ubavu wa kuuweka uraia wake under microscope kali, tutayaona madudu ya ajabu tu yalioyafanywa na maafisa husika wa wa serikali.

Mkuu usimung'unye maneno sema tu madudu anayofanya Jakaya Kikwete.
 
Mkuu Malafyale, Ugonile!
Nakubaliana na maelezo yako,inabidi kwanza tukae kimya ili tuone kwa dhati ukweli wa habari hii,kama inavyoshughulikiwa na vyombo vya sheria na Idara ya Uhamiaji.Hapo awali baadhi ya watu hapa wamekuwa wanashangilia habari hii,labda kwa ushabiki wa vyama vya kisiasa au tabia tu ya kupenda habari mvunjiko (habari mpya).Nimesoma Magazeti mbalimbali ya Leo (Jumanne) na kusikiliza mahojiano ya Hussein Bashe na watu wa BBC na nimeona wazi kuwa kuna habari zinakinzana.

Katika Mahojiano na watu wa BBC,Bwana Bashe amesema wazi kuwa Baba yake Mzazi ni raia wa Somalia aliyehamia hapa muda mrefu,lakini Mama yake mzazi ni mzaliwa wa Tabora, kwa maana hiyo aliweza kupata Uraia wa Tanzania kwa kurithi upande wa Mama yake. Nimejaribu kuipata clip ya Mahojiano yale ili niilete hapa lakini nimeshindwa,kwa wanaotaka kuisikia na kuipata clip hiyo watembelee wavuti.com au wawasiliane na Da' subinukta77.

Kinachonishangaza zaidi Gazeti la Mwananchi na Tanzania Daima wote kwa pamoja wametoa vielelezo vinavyoonyesha Bwana Bashe ana Hati ya Uraia number S/N 312 iliyotolewa tarehe 10/August/2009,Ikumbukwe kuwa kuna Tofauti kati ya Cheti cha kuzaliwa na Hati ya Uraia,kutokana na Gazeti la Mwananchi ina maana si kweli kwamba Mama Mzazi wa Bwana Bashe ni Raia wa kuzaliwa wa Tanzania,ina maana Bashe aliomba Uraia wa Tanzania na ndio maana akakabidhiwa hiyo Hati yenye # S/N 312. Kwa kuwa vitu hivyo vipo kwenye maandishi Ukweli wa habari nzima utajulikana.Lakini kutokana na maelezo ya Bashe kupitia BBC kuna mgongano mkubwa wa maelezo unaotia Utata suala zima la Uraia wake.
Masuala ya Utata wa Uraia sio mageni katika majukwaa ya siasa za Tanzania,itakumbukwa kuwa mwaka 2003 Viongozi wa juu wa kada mbalimbali walivuliwa Uongozi wao kwa sababu Uraia wao ulikuwa na Utata,Miongoni mwa Viongozi hao ni 1);Jenerali Ulimwengu,ambaye aliwahi kuwa mshauri wa Rais,Mkuu wa Wilaya na baadaye Mwenyekiti wa Habari cooperation 2);Moudline Castiko aliyekuwa Njumbe wa CC na Katibu mwenezi wa CCM -Zanzibar 3);Anatory Amani aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoani Kagera.4);Timothy Bandora ambaye alikuwa Balozi na Mwajiriwa wa Wizara ya mambo ya Nje (MOFA).Ni mwaka jana tu pia kumekuwa na Utata wa Uraia wa Catherine Peter Nao,ambaye kama Hussein nae ni mjumbe wa NEC zanzibar.

Tuachie vyombo vya sheria tutaujua ukweli kuhusu Uraia wa Ndugu Bashe.
Mkuu usishtuke salaam yangu ya kinyakyusa,nina mizizi na huko Kyela.Nakumbuka kuwa kamanda wa Vijana CCM kwenye uzinduzi wa Chama hicho 1977.

Sorry hapo kwenye rangi sheria haisemi hivyo. Kama baba angekuwa Mtanzania inakuwa automatic mama No. Angalia sheria tena inasemaje kama ulifuatilia ule mlolongo wa Dual citizenship hilo liliwekwa bayana kule tulilijadali and beside naifahamu hiyo sheria vizuri tuliiridhi kutoka kwa Waingereza ingawa wao wanaweza kuwa wameibadili..
 
Mimi huwa napenda kufuatilia issue, sio mtu.
Je kuna system maalum ya kucheki wagombea wao wote, uraia, kumbukumbu ya kesi nk ili vitumike wakati wa kuhakiki majina?
Au atakae pata bahati mbaya ndio atakaehusika?
Je tunaweza sasa kuwa wagombea wote waliobaki ni raia (kwa uhakika wa sheria zilizopo) na hawana kesi zinazokatazwa?
Hivi inakuwaje kama hizi issue zingekuwa zinawekwa wazi kabla ya kuchukua fomu ili kupunguza fujo? hii itasababisha watu wafunguliwe kesi za jinai kwa kudanganya na foji, na sio upuuzi wa aina hii.
 
Mawazo Matatu;

Naungana na wewe,kwa maskio yangu nimesikia Bashe akisema anashangaa kuambiwa sio raia kwa sababu Mama yake ni mzaliwa Tabora na kisheria akasema kama mmoja wa wazazi wako ni raia wa TZ hupaswi kuomba uraia ukifikisha miaka 18 kwani unakuwa unarithi moja moja uraia wa TZ kutoka kwa mmoja wa wazazi wako!

Lkn jana hiyo hiyo akaongea na waandishi wa habari na kuonyesha hata viapo vyake alivyo apa mahakamani Dar kuukana uraiawa Somalia;kisheria ina maana ni kweli kuwa wazazi wake wote 2 hawakuwa Raia wa TZ bali Wasomali alipokuwa anazaliwa Bashe na ndiyo maana aliapa kuukana uraia wa wazazi wake!

Ni kauli 2 tata tena tofauti toka kwa mtu huyu Bashe;hii naanza kuunga mkono kauli ya Makamba kuwa kijana huyu ni"vuvuzela"wa uraia;iweje uende kuapa mahakamani na kuukana usomalia kama wewe mmoja wa wazazi wako ni raia kipindi kile unazaliwa?Kama wewe ni Riai wa TZ why ukaape ili kuukana U-somalia na kuupata U-TZ wakati wewe ni raia tayari wa KUZALIWA wa TZ uliye urithi toka kwa mama yako aliyekuwa RAIA wakati Bashe anazaliwa?

Uhamiaji mchunguzeni kijana huyu Bashe;anajichanganya sana kwenye habari zake!

Hi
Sheria ya Uraia Tanzania ina hitaji mtu yeyote aliyezaliwa na mzazi aiye Mtanzania anatakiwa kuukana uraia wa mzazi wake akifikia umri wa miaka kumi na nane. Katika mfano wa Hussein bashe, mama yake alizaliwa katika mkoa wa tabora, lakini na mzazi ambaye alikuwa ni raia wa Somalia. Mama wa Hussein alipofika umri wa 18 years haukukana uraia wa Somalia that means she still was SOMALI at the time Hussein was born.

Wazazi wake waliomba uraia wa tanzania mika kumi baada ya Bashe kuzaliwa, kwa hiyo yeye alikuwa bado ni msomali kwa sababu alzaliwa na wazazi waliokuwa wasomali.

Now Hussein, kwa sababu alikwenda shule sio kucheza ila kusoma alielewa kwamba siku moja atatakiwa awe raia wa tanzania to fulfill his dream of becoming a leader in the country he loves. Akaenda Kivukoni Magistrates and denounce his Mother's status"somali" , so alipewa uraia wa Tanzania August 2009.

Hakuna kauli zenye utata amefuata sheria ilivyokuwa inatakiwa. Suali ni kwamba? Je kama hawa viongozi waliokuwa kwenye mkutano dodoma nyuma ya closed doors, wamefanya very stupid and childish mistakes watafuata njia sahihi na wajiuzulu kwa kuwajibishwa?

By the way, nimeandika hii post because myself have been there and done that so. Hakuna mtu atakaye niambia sheria inasema hivi na vile. I know the sheria cos i had to deal with it.

The only issue here is, Hussein somewhere touched the president's inner cycle and he is
paying for it because watanzania bado mmelala...President should not be allowed to run the country like royal family...period!

all the best
 
@counterpunch, did you want to be know as counterattack!!lol

Kwa nini unaongea kama unaishi 18th century..hi ni 21st century na hakuna mtu anayeweza kufeki mambo kama hayo, kama unaona huyu kijana anasaidiwa na Rostam Azizi, kwa nini unakuwa kipofu kuona kwamba huyu anatoswa na kikwete, mke wake an mtoto wake?
Kaa ufikiri kabla haujatamka kwa sababu usidhani haya mambo yanayofanywa na viongozi yatakuwa yanamuwinda mtu mmoja au rangi tofauti na yako..Ila kila mtu ni sawa leo kwa hussein bashe kesho itakuwa kwako..Jiandaeni au pigieni haki zenu watanzania
 
what a ridiculousl assertion, are you crazy you are using an example that is absolutely BS..I cant believe this..I swear to god Tanzania is doomed..the onle solution is "NEOCOLONIALISM"
 
WIZARA ya Mambo ya Ndani imemwandikia barua kada wa CCM, Hussein Bashe kuthibitisha kuwa ni raia wa Tanzania baada ya suala hilo kusababisha anyimwe nafasi ya kuwania ubunge wa Nzega kwa tiketi ya CCM.

Bashe alishinda kwenye kura za maoni za CCM kwenye jimbo hilo la Nzega baada ya kupata kura zaidi ya 14,000, lakini akaenguliwa baada ya ukakasi kuibuka kwenye uraia wake.

Baadaye katibu mkuu wa CCM, Yusuf Makamba na katibu wa idara ya itikadi na uenezi ya chama hicho, John Chiligati waliwaambia waandishi kuwa Bashe si raia na kwamba ametakiwa aanze upya taratibu za kupata uraia wa Tanzania.

Alipoulizwa kuhusu suala la Bashe jana, Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha alisema: "Kwa mujibu wa sheria, mimi ndiye wa mwisho kuzungumzia suala hili. Jibu langu lipo pale pale na siwezi kubadili. Bashe ni raia halali wa Tanzania."

Masha, ambaye alishawahi kusema kuwa uraia wa Bashe hauna tatizo, aliongeza kusema: “Nani kasema Bashe si raia? Kama waziri mwenye dhamana nasema, Bashe ni raia halali na hakuna atakayebadilisha msimamo wangu huu.’’

Taarifa ambazo Mwananchi inazo zinasema kuwa barua hiyo ya serikali kwenda kwa Bashe imeandikwa na waziri huyo ambaye pia anasimamia Idara ya Uhamiaji, lakini alipoulizwa na Mwananchi kuhusu barua hiyo hakutaka kueleza chochote zaidi ya kusisitiza kuwa mgombea huyo wa zamani wa ubunge wa Nzega ni raia halali.

Barua ambayo Mwananchi imeiona kutoka kwa mmoja wa maofisa waandamizi wa wizara hiyo inaonyesha kuwa mbali na kumthibitishia Bashe kuwa ni raia, pia imemfafanulia tatizo lililojitokesza kwenye nyaraka za awali kuhusu kabila.

Barua hiyo imeeleza kuwa kwa mujibu wa kifungu Na.5 (1) au 7 (8) cha Sheria Namba 7 ya Uraia ya mwaka 1995, Bashe ni raia wa Tanzania kwa kuzaliwa. Barua hiyo iliyoandikwa Septemba 3 ambayo inakwenda kwa Bashe, ina kichwa cha habari kisemacho "Upotoshwaji juu ya Uraia wako" ambayo inaonekana kuwa ni majibu ya barua kutoka kwa kada huyo wa CCM akitaka ufafanuzi wa suala lake.

Barua hiyo ya Masha inaeleza kuwa utata kuhusu uraia wa Bashe ulitokana na kada huyo kuwasilisha hati ya kiapo inayoonyesha kuwa ni Mnyamwezi badala ya Mtanzania mwenye asili ya Somalia. "Utata huo haukuondolei haki yako ya kuwa Mtanzania. Hata hivyo utata huo umeondolewa kwa kiapo kingine ambacho kimerekebisha kile cha awali," anaeleza Masha katika barua hiyo. "Kwa msingi huo, kwa barua hii ninathibitisha kuwa Hussein Mohamed Bashe Ibrahim ni raia wa Tanzania kwa kuzaliwa kwa mujibu wa Sheria ya Uraia Na.7 ya mwaka 1995 kifungu Na. 5(1) au 7(8)."

Barua hiyo imepelekwa kwa Bashe na kwa katibu mkuu wa CCM, Yusuf Makamba.
Ufafanuzi wa jana wa Masha umetolewa takriban wiki tatu tangu halmashauri kuu ya CCM imuondoe kwenye kinyang'anyiro cha jimbo hilo ambalo lilikuwa linashikiliwa na Lucas Selelii ambaye alishika nafasi ya pili kwa kupata kura zisizidi 3,000 lakini pia akatemwa.
Tiketi ya CCM ya jimbo hilo ilikwenda kwa Dk Khamis Kigwangala ambaye pia alikumbwa na tatizo la uraia baada ya kuhojiwa na Idara ya Uhamiaji na baadaye kuwekewa pingamizi ambalo lilitupwa.

Mbali na kuenguliwa kwenye kugombea ubunge, halmashauri kuu iliagiza mwanasiasa huyo kijana avuliwe uanachama na vyeo vyake vyote ndani ya CCM, ikiwa ni pamoja na ujumbe wa baraza kuu la umoja wa vijana.

Alipotafutwa kuzungumzia suala hilo la Bashe, katibu mkuu wa CCM, Yusuf Makamba alisema asingeweza kulizungumzia kwa kuwa yuko mapumzikoni. "Nipo nyumbani kwa mapumziko,'' alisema Makamba na kukata simu.

Naye makamu mwenyekiti wa CCM Bara, Pius Msekwa hakutaka kuzungumzia suala hilo na badala yake alisema: "Mimi nipo Mwanza Vijijini, siyajui ya Dar es Salaam.
Waulize ambao wako huko (Dar es Salaam).''

Baada ya kikao hicho cha halmashauri kuu ya CCM kilichofanyika Dodoma, Chiligati aliwaambia waandishi wa habari akisema: “Wazazi wa Bashe walikuja nchini wakitokea Somalia na baba yake alipata uraia miaka kumi baadaye.

Kwa kuwa Bashe alizaliwa kabla ya wazazi wake kupata uraia, kisheria yeye si raia na kwamba alikuwa akiishi kwa mazoea na matatizo kama haya yamewakumba watu wengi kwa mfano Jenerali Ulimwengu.”

SOURCE: Gazeti la Mwananchi

My Question: Kwa nini Masha hakuyafutilia mbali maamuzi ya Makamba na CCM yake siku ile ile walipoyatoa??
 
Serikali yathibitisha uraia wa Bashe Send to a friend
Thursday, 09 September 2010 22:41

Hussein Bashe

Sadick Mtulya
WIZARA ya Mambo ya Ndani imemwandikia barua kada wa CCM, Hussein Bashe kuthibitisha kuwa ni raia wa Tanzania baada ya suala hilo kusababisha anyimwe nafasi ya kuwania ubunge wa Nzega kwa tiketi ya CCM.

Bashe alishinda kwenye kura za maoni za CCM kwenye jimbo hilo la Nzega baada ya kupata kura zaidi ya 14,000, lakini akaenguliwa baada ya ukakasi kuibuka kwenye uraia wake.

Baadaye katibu mkuu wa CCM, Yusuf Makamba na katibu wa idara ya itikadi na uenezi ya chama hicho, John Chiligati waliwaambia waandishi kuwa Bashe si raia na kwamba ametakiwa aanze upya taratibu za kupata uraia wa Tanzania.

Alipoulizwa kuhusu suala la Bashe jana, Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha alisema: "Kwa mujibu wa sheria, mimi ndiye wa mwisho kuzungumzia suala hili. Jibu langu lipo pale pale na siwezi kubadili. Bashe ni raia halali wa Tanzania."
Masha, ambaye alishawahi kusema kuwa uraia wa Bashe hauna tatizo, aliongeza kusema: “Nani kasema Bashe si raia? Kama waziri mwenye dhamana nasema, Bashe ni raia halali na hakuna atakayebadilisha msimamo wangu huu.’’

Taarifa ambazo Mwananchi inazo zinasema kuwa barua hiyo ya serikali kwenda kwa Bashe imeandikwa na waziri huyo ambaye pia anasimamia Idara ya Uhamiaji, lakini alipoulizwa na Mwananchi kuhusu barua hiyo hakutaka kueleza chochote zaidi ya kusisitiza kuwa mgombea huyo wa zamani wa ubunge wa Nzega ni raia halali.

Barua ambayo Mwananchi imeiona kutoka kwa mmoja wa maofisa waandamizi wa wizara hiyo inaonyesha kuwa mbali na kumthibitishia Bashe kuwa ni raia, pia imemfafanulia tatizo lililojitokesza kwenye nyaraka za awali kuhusu kabila.

Barua hiyo imeeleza kuwa kwa mujibu wa kifungu Na.5 (1) au 7 (8) cha Sheria Namba 7 ya Uraia ya mwaka 1995, Bashe ni raia wa Tanzania kwa kuzaliwa.

Barua hiyo iliyoandikwa Septemba 3 ambayo inakwenda kwa Bashe, ina kichwa cha habari kisemacho "Upotoshwaji juu ya Uraia wako" ambayo inaonekana kuwa ni majibu ya barua kutoka kwa kada huyo wa CCM akitaka ufafanuzi wa suala lake.

Barua hiyo ya Masha inaeleza kuwa utata kuhusu uraia wa Bashe ulitokana na kada huyo kuwasilisha hati ya kiapo inayoonyesha kuwa ni Mnyamwezi badala ya Mtanzania mwenye asili ya Somalia.

"Utata huo haukuondolei haki yako ya kuwa Mtanzania. Hata hivyo utata huo umeondolewa kwa kiapo kingine ambacho kimerekebisha kile cha awali," anaeleza Masha katika barua hiyo.

"Kwa msingi huo, kwa barua hii ninathibitisha kuwa Hussein Mohamed Bashe Ibrahim ni raia wa Tanzania kwa kuzaliwa kwa mujibu wa Sheria ya Uraia Na.7 ya mwaka 1995 kifungu Na. 5(1) au 7(8)."
Barua hiyo imepelekwa kwa Bashe na kwa katibu mkuu wa CCM, Yusuf Makamba.

Ufafanuzi wa jana wa Masha umetolewa takriban wiki tatu tangu halmashauri kuu ya CCM imuondoe kwenye kinyang'anyiro cha jimbo hilo ambalo lilikuwa linashikiliwa na Lucas Selelii ambaye alishika nafasi ya pili kwa kupata kura zisizidi 3,000 lakini pia akatemwa.

Tiketi ya CCM ya jimbo hilo ilikwenda kwa Dk Khamis Kigwangala ambaye pia alikumbwa na tatizo la uraia baada ya kuhojiwa na Idara ya Uhamiaji na baadaye kuwekewa pingamizi ambalo lilitupwa.

Mbali na kuenguliwa kwenye kugombea ubunge, halmashauri kuu iliagiza mwanasiasa huyo kijana avuliwe uanachama na vyeo vyake vyote ndani ya CCM, ikiwa ni pamoja na ujumbe wa baraza kuu la umoja wa vijana.
Alipotafutwa kuzungumzia suala hilo la Bashe, katibu mkuu wa CCM, Yusuf Makamba alisema asingeweza kulizungumzia kwa kuwa yuko mapumzikoni.

"Nipo nyumbani kwa mapumziko,'' alisema Makamba na kukata simu.
Naye makamu mwenyekiti wa CCM Bara, Pius Msekwa hakutaka kuzungumzia suala hilo na badala yake alisema: "Mimi nipo Mwanza Vijijini, siyajui ya Dar es Salaam.

Waulize ambao wako huko (Dar es Salaam).''
Baada ya kikao hicho cha halmashauri kuu ya CCM kilichofanyika Dodoma, Chiligati aliwaambia waandishi wa habari akisema: “Wazazi wa Bashe walikuja nchini wakitokea Somalia na baba yake alipata uraia miaka kumi baadaye. Kwa kuwa Bashe alizaliwa kabla ya wazazi wake kupata uraia, kisheria yeye si raia na kwamba alikuwa akiishi kwa mazoea na matatizo kama haya yamewakumba watu wengi kwa mfano Jenerali Ulimwengu.”
 
Mazingaombwe na usanii wa CCM kunawakati yanatia kichefuchefu kama huyu jamaa Bashe aliondolewa ktk kinyanganyiro cha ubunge kwa sababu ya urai na sasa imethibitishwa kwamba ni raia wa Tanzania kama hakuondolewa kwa mizengwe iliku ni mategemeo yangu kua CCM ingelimuomba msamaha na kumrejesha katika kinyang'anyiro cha ubunge vininevyo tunashindwa kuiilewa CCM hiki ndicho chama tunachotegemea kituoongoze MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
Mkuu Wakili,

Kumrejesha kwenye kinyang'anyiro it is too late, deadlines za kuchukua na kurejesha fomu Tume ya Uchaguzi zimeishapita, so hata wakisema wamrejeshe NEC (Tume) hawawezi kumruhusu. Atarejeshewa nafasi zake za uongozi ndani ya CCM na UVCCM. Kwenye Ubunge ndo imetoka, labda asubiri 2015.

Kama waliomfanyizia walitaka asigombee Ubunge, lengo limetimia. Anatakiwa atulize kichwa na kuanza kutafakari ya huko mbeleni. Hiyo ndio CCM Bwana, maana unashangaa JK alikuwa na data full mpaka akasema hata hati za viapo ni fake (kulingana na magazeti yaliyonukuu maneno ya JK wakati akijenga hoja ya kumkata jina). Sasa sijui JK anajisikiaje na iwapo ni kweli alisema maneno hayo?

Kuna vitu vingine maamuzi yake yanahitaji umakini mkubwa ili kuepuka kurudia matapishi. Ni aibu kubwa kwa viongozi wa juu wa CCM ambao walitamka hadharani kwamba jamaa si raia, na ndio maana kila mmoja anakwepa kuongelea hilo swala. Yaonekana ama walijua ni nini kilikuwa kinaendelea au wanaona aibu baada ya kuumbuliwa.
 
Mambo bado... tuna zaidi ya siku 50 nyingine

Mkuu ninasaka sana habari za uchaguzi Mkoa wa Tabora, kwa bahati mbaya hazipatikani au kama zinapatikana basi uandishi wake uko nusu nusu. Ina maana mkoa wangu hauna wawakilishi/waandishi wa magazeti?
 
Back
Top Bottom