Mkuu Malafyale, Ugonile!
Nakubaliana na maelezo yako,inabidi kwanza tukae kimya ili tuone kwa dhati ukweli wa habari hii,kama inavyoshughulikiwa na vyombo vya sheria na Idara ya Uhamiaji.Hapo awali baadhi ya watu hapa wamekuwa wanashangilia habari hii,labda kwa ushabiki wa vyama vya kisiasa au tabia tu ya kupenda habari mvunjiko (habari mpya).Nimesoma Magazeti mbalimbali ya Leo (Jumanne) na kusikiliza mahojiano ya Hussein Bashe na watu wa BBC na nimeona wazi kuwa kuna habari zinakinzana.
Katika Mahojiano na watu wa BBC,Bwana Bashe amesema wazi kuwa Baba yake Mzazi ni raia wa Somalia aliyehamia hapa muda mrefu,lakini Mama yake mzazi ni mzaliwa wa Tabora, kwa maana hiyo aliweza kupata Uraia wa Tanzania kwa kurithi upande wa Mama yake. Nimejaribu kuipata clip ya Mahojiano yale ili niilete hapa lakini nimeshindwa,kwa wanaotaka kuisikia na kuipata clip hiyo watembelee wavuti.com au wawasiliane na Da' subinukta77.
Kinachonishangaza zaidi Gazeti la Mwananchi na Tanzania Daima wote kwa pamoja wametoa vielelezo vinavyoonyesha Bwana Bashe ana Hati ya Uraia number S/N 312 iliyotolewa tarehe 10/August/2009,Ikumbukwe kuwa kuna Tofauti kati ya Cheti cha kuzaliwa na Hati ya Uraia,kutokana na Gazeti la Mwananchi ina maana si kweli kwamba Mama Mzazi wa Bwana Bashe ni Raia wa kuzaliwa wa Tanzania,ina maana Bashe aliomba Uraia wa Tanzania na ndio maana akakabidhiwa hiyo Hati yenye # S/N 312. Kwa kuwa vitu hivyo vipo kwenye maandishi Ukweli wa habari nzima utajulikana.Lakini kutokana na maelezo ya Bashe kupitia BBC kuna mgongano mkubwa wa maelezo unaotia Utata suala zima la Uraia wake.
Masuala ya Utata wa Uraia sio mageni katika majukwaa ya siasa za Tanzania,itakumbukwa kuwa mwaka 2003 Viongozi wa juu wa kada mbalimbali walivuliwa Uongozi wao kwa sababu Uraia wao ulikuwa na Utata,Miongoni mwa Viongozi hao ni 1);Jenerali Ulimwengu,ambaye aliwahi kuwa mshauri wa Rais,Mkuu wa Wilaya na baadaye Mwenyekiti wa Habari cooperation 2);Moudline Castiko aliyekuwa Njumbe wa CC na Katibu mwenezi wa CCM -Zanzibar 3);Anatory Amani aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoani Kagera.4);Timothy Bandora ambaye alikuwa Balozi na Mwajiriwa wa Wizara ya mambo ya Nje (MOFA).Ni mwaka jana tu pia kumekuwa na Utata wa Uraia wa Catherine Peter Nao,ambaye kama Hussein nae ni mjumbe wa NEC zanzibar.
Tuachie vyombo vya sheria tutaujua ukweli kuhusu Uraia wa Ndugu Bashe.
Mkuu usishtuke salaam yangu ya kinyakyusa,nina mizizi na huko Kyela.Nakumbuka kuwa kamanda wa Vijana CCM kwenye uzinduzi wa Chama hicho 1977.