Uchaguzi 2020 Kamati Kuu (Halmashauri Kuu) walikosea sana kumpitisha Askofu Gwajima kugombea Ubunge Kawe

Uchaguzi 2020 Kamati Kuu (Halmashauri Kuu) walikosea sana kumpitisha Askofu Gwajima kugombea Ubunge Kawe

Ccm ikiamua inashinda kibabe tu,ila sasa ndo hivyo tena askofu alishawakera watu wa dini pa kubwa,,,yan apo kawe kila mgombea ni shimo refu la moto majanga matupu si halima wala gwajinongo
 
Nimekuekewa Paskali. Hapo ndio tunaingia kwenye sayansi ya "split personality". Rejea William Shakespeare, Dr. Jekyll and Mr. Hyde. Upande mmoja tunaye Gwaji ambaye ni Mtume Paulo na ule mwingine ni Saul. Hivyo unashauri tumchague Gwaji kama Mt. Paulo na tumwache Gwaji ambaye ni Saul. Tatizo linalojitokeza hapo ni lini utajua kwamba aliyepo leo ni Paulo na si Sauli ili watu waweze kumchagua. Ufumbuzi wake ni kuwaacha wote na si kucheza patapotea.
Mkuu KUTATABHETAKULE , nimeipenda argument yako na especially ule mfano wa Dr. Jekyll and Mr. Hyde ni kazi ya Robert Louis Stevenson na ilikuwa sighted na Dr. Sigmund Freud, kwenye Me and I, na nilipiga madarasa ya Freud humu jf
Psychoanalysis: Superiority Complex ni Dalili ya Inferiority Complex!. Maneno Mafupi Vitendo Virefu.

Baada ya Saulo kugeuka Paulo, he could not return to Saulo, hivyo Gwajima Mbunge ni huyu Gwajima wa sasa na sio Gwajima yule wa zamani!.
p
 
Kamati kuu Wana Akili Sana kumpitisha Gwajima ,nimependa Sana maamuzi yao wamefanya kitu Cha kiakili kumpitisha Mtu mwenye Akili Gwajima
 
Binadamu wote ni viumbe dhaifu, kukosea ni kawaida. Kufuatia ukongwe na uzoefu wa CCM, CCM, haikukosea kumteua Askofu Gwajima, ndiye chaguo sahihi kwa maendeleo ya jimbo la Kawe.

P
Hawakutaki MaCCM,hata ukitembea bila nguo,hupati hata uteuzi wa afisa mtendaji,mbona hujtambui na wewe ni mtu mzima.
 
Heshima sana wanajamvi.

Tukubali tukatae CCM ni chama kikubwa,kikongwe,kina uzoefu katika medani ya siasa za Tanzania na wakati wa Mwl Nyerere kilikuwa na mitazamo iliyovuka mipaka ya Tanzania (Ukombozi wa nchi za kusini mwa Afrika) na pia masuala ya utangamano wa kikanda na hatimaye Afrika nzima.

Kutokana na ukongwe na ukubwa wake unabaki kushangaa ilikuwaje Askofu Gwajima jina lake likapitishwa na vikao vizito vya chama. Kamati kuu ilishindwa kupata ushahidi wa video za Askofu Gwajima akikashifu dini ya KiIslam, Catholic, Lutheran.Eti kwake yeye dini ya maana ni Assemblies of God.

Ipo Video najaribu kuiweka hapa kwa kweli inashangaza kama si kusikitisha.Askofu Gwajima badala ya kuhubiri/mafundisho ya imani yake kajikita zaidi katika kukashfu imani nyingine tena kwa maneno ambayo hata mimi naogopa kuandika hayafai yamekosa ustaarabu wa kiwango cha kutisha.Ni ajabu sana Askofu Gwajima bado anaoujasiri wa kupita mitaani bila aibu wala uoga wa kuomba kura jimbo la Kawe.

CCM imefanya makosa makubwa,tukubali na kujisahihisha mapema.
Kampeni za Gwajima anaruka ruka kama vile karogwa.

Mara azoe taka kwenye mitalo, ma ajipake mavumbi....yaani mradi tu ajifanye kama hamnazo
 
Mimi nadhani CCM hawategemei kupigiwa kura ili kupata ushindi ndio maana wakawa na uthubutu wa kumsimamisha chizi maarifa
 
Nimehudhuria kwenye kampeni katika kata moja ya jimbo la KAWE, aisee nilikua siamini kama wanaccm wenyewe wanaweza kutamka kwa maneno yao midomoni kua Ubunge wanampa mpinzani halafu Urais kwa Magufuli ingawaje nako Urais nasikia wanatamkia mdomoni lakini watampa Tundu Lissu.

Huyu ni mgombea wa pili kukaguliwa live na wananchi katika mkoa wa Dar es Salaam baada ya Bonah Kamoli wa jimbo la Segerea naye kukataliwa hadharani tena yeye akiwepo kwenye mkutano mpaka alifunika macho yake.

Ni kosa sasa kwa kamati kuu ya CCM kupitisha watu ambao hayakua machaguo ya wananchi, tatizo kubwa la Gwajima alikua mshindi wa 3 nyuma ya Angella na Furaha ambao nao walikua na wafuasi wao. Hili limeleta mgawanyiko mkubwa hata kwa CCM wenyewe, wajumbe wanadai hawako tayari kulazimishwa kuchagua mtu ambaye hakua chaguo lao.
 
Gwajima ashapita,kwani ni lazima apite mdee kila chaguzi? This time round it will be messy!!
 
Halima hana ujasiri wa kusalimiana na wananchi kama Gwajima anavyofanya kwa ufupi tu nasubiri anguko la Halima mdee 28 kawe tunakwenda na Gwajima.

IMG-20200928-WA0075.jpg
 
Huwa wanajinadi kuwa watafanya uchakachuaji mkubwa lakini inasemekana Bashite na yeye yupo na furaha wanasaidia kumdhoofisha ingawa Bashite hampendi mdee lakini anamchukia Gwajima zaidi
CCM oyeeeeeee
Gwajima oyeeee kama alikuwa nafasi ya tatu na akateuliwa ujue hata huu ubunge lazima ashinde tu maana n haki yake kabsa haijalishi nani anamchukia au nan anampenda Gwajima kushinda n lazima.
 
CCM ya sasa tumekua viburi sana timepuuza maoni ya wananchi tunaangalia wenye pesa tu
Wananchi wapi CCM imetenda haki kabsa wananchi watatenda haki zaidi tar 28 ndo utajua kwann mkate n Mlaini kwenye chai
Gwajima juuu
 
Back
Top Bottom