Kamati Kuu ya CCM yaielekeza Serikali kuchukua hatua kuhusu maoni ya TOZO

Kamati Kuu ya CCM yaielekeza Serikali kuchukua hatua kuhusu maoni ya TOZO

Amesema “Maelezo hayo yamezingatia Ibara ya 20 Kifungu kidogo B ya Ilani ya Uchaguzi 2025, kuongeza upatikanaji wa huduma za kifedha kwa gharama nafuu kwa kupanua wigo wa matumizi ya TEHAMA, kuchochea uwekezaji wa ndani na kukidhi mahitaji halisi ya Wananchi hususani waishio vijijini.”
Kumbe mlidhamiria kabisa kutuua! Dah nyie Watu ni mashetani
 
CCM inayoongozwa na Samia imeitaka Serikali ya Samia kusikiliza kero la tozo linalolalamikiwa na wanachi ili iweze kulitatua.

Kwenu studio.
waliopo Serikalini ndio hao hao Waliopo ccm
Waziri Mwigulu kasema Wananchi Walitaka TOZO
CCM inasema Serikali iwasikilize Wananchi
1662635032269.jpg
1662053772400.jpg
 
Kati ya wajumbe wa kamati kuu yupo Rais ambaye ndiye mwenyekiti wa chama,yupo Makamu wa Rais, Waziri Mkuu na wajumbe wengine wachache ambao hawana ubavu kumlazimisha Rais kufanya chochote, waache kuwafanya Watanzania ni Mazuzu.
 
Asante kwa taarifa
P
Kaka Pascal naomba unisaidie Mwenyekiti wa Kamati kuu ni Nani?
Kiongozi wa serikali iliyoelekezwa na Kamati kuu ni Nani
Mwenyekiti wa BLM iliyoandaa huo muswada wa Sheria ya tozo ni Nani?
Halafu uje unisaidie Nani amemuelekeza Nani!
Ukimya wa watanzania katika mambo yamsingi yanawagusa ni faida kwa viongozi wasiokuwa wabunifu, na wawajibikaji!
Imekua rahisi sana hili la tozo kuzungumzwa kwa sababu kisu kimegusa mifupa mingi!
Nasubiri kamati kuu ieelekeze serikali kupitia upya nauli na gharama za usafiri Baada ya EWURA kutangaza kushuka kwa Bei ya Mafuta ya Petrol!
Ila kwakua wanufaika ni hao hao utaona kimya tu!
 
CCM inayoongozwa na Samia imeitaka Serikali ya Samia kusikiliza kero la tozo linalolalamikiwa na wanachi ili iweze kulitatua.

Kwenu studio.
Kwani hii ni geni kwako

Miaka nenda urudi kwani hujuwi kuwa

Ccm ndiyo serikali

Ccm chama $

Ova
 
Yaani Kamati kuu inayoongozwa na fulani imeilekeza serikali inayoongozwa na huyo huyo fulani. Kwa kifupi kajielekeza.

Serikali inayoongozwa na CCM mbali ya TOZO ingependekeza iwe sikivu ipunguze matumizi ya anasa na ya kifahari mfano utiriri wa magari almaarufu V8, au jambo la wabunge 'kukopeshwa magari', viongozi vigogo wa serikali kununuliwa magari ya anasa V8

Kamati Kuu - CC Central Committee ya CCM suala la kuibana au kuielekeza serikali yake kubana matumizi hilo halina umuhimu?
 
Maisha bhana
Kuna wakati inafika inakuwa HAKUNA mshindi mala mshindwa
Wazee wa Pareto Optimality ndio wanatafuta sasa katikati ni wapi?
Hii ngoma haina bingwa kuna wa itafikia itabidi tuungane tu kukataa jambo fulani
Sasa hii ndio inaitwa 'fact'
 
..Hilo lingewezekana kama Raisi na Amiri Jeshi Mkuu asingekuwa mwenyekiti wa chama.
 
KAMATI KUU YA CCM, muwaase viongozi wenu katika serikali wasiwe wagumu kuhusu matumizi mazuri ya fedha zetu za tozo na kodi, kwani pesa hizi siyo za kwao binafsi hivyo wazitumie kwa kujua fedha hizo wanazo tapanya kwa matumizi ya fujo ya kifahari na anasa ni zetu walipa kodi na hatufurahishwi na mwenendo huo :

Wanasiasa wajifunze kwa mzee Ali Hassan Mwinyi, kuwa usitumie madaraka na mamlaka vibaya hasahasa ukiwa mkubwa kimadaraka. Kumbuka utahukumiwa na historia..

Toka Maktaba :

3 Sept 2016

Alichokizungumza Rais Magufuli kuhusu Maalim Seif kukataa mkono wa Rais Shein

Magufuli amshauri Dr. Mohamed Shein asisaini mafao ya ustaafu ya Maalim Seif Hamad

’Kama mtu anaukataa mkono wako na wewe kataa mkono wako kufanya mambo yake, ajifunze ajue mkono wako una thamani, haiwezekani mbele ya watu unatoa mkono anaukataa halafu unatoka kwenda ofisini unasema unasaini hapa hela ya huyu kwenda kutibiwa’:-JPM
 
Yaani Samia ana uwezo mdogo sana wa kufikiri. Kweli kabisa tozo kwa maskini ni suluhisho endelevu kwa umaskini wa Mtanzania ?Too sad. Sema nini Mwigulu kafanikiwa kuteka ubongo wa Samia.
 
CCM inayoongozwa na Samia imeitaka Serikali ya Samia kusikiliza kero la tozo linalolalamikiwa na wanachi ili iweze kulitatua.

Kwenu studio.
Kujitekenya wajitekenye wenywe na kuche wacheke wenyewe.
Ccm imesha tuona sie ni mazombi
 
Back
Top Bottom