Kamati kuu ya CCM yakutana Mwanza: Yampongeza Rais Magufuli, Walio hama vyama vya Upinzani waongeza Ruzuku ya chama hadi Bil 13

Kamati kuu ya CCM yakutana Mwanza: Yampongeza Rais Magufuli, Walio hama vyama vya Upinzani waongeza Ruzuku ya chama hadi Bil 13

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Kamati kuu ya CCM imekutana jijini Mwanza na kuongozwa na Mwenyekiti wake Dr Magufuli.

Kamati kuu imempongeza Rais Magufuli na serikali yake kwa ujenzi wa miradi mikubwa inayoendelea nchini.

Katibu mkuu wa CCM Dr Bashiru amesema kwa sasa hakuna kikwazo chochote kinachoweza kupunguza kasi ya chama na serikali yake katika kuwaletea maendeleo wananchi.

Dr Bashiru amewataka watanzania kuendelea kuwa na umoja huu tulionao sasa kwani umoja na amani iliyopo ndio vimewezesha kupatikana kwa haya maendeleo makubwa tunayoyashuhudia.

CCM.jpg

Mwenyekiti wa CCM Dr Magufuli amewashukuru wajumbe wa halmashauri kuu ya chama hichi kwa maamuzi mbalimbali waliyoyachukua katika kuleta mabadiliko.

Kwa mfano kamati ya kufuatilia mali za chama iliyoongozwa na Dr Bashiru iligundua ufisadi mkubwa kwenye mali za chama.

Baada ya kamati ya Dr Bashiru kumaliza kazi yake tumefanikiwa kurejesha mali nyingi mikononi mwa chama na kurekebisha baadhi ya mikataba ikiwemo ya Vodacom na jengo la HQ ya UVCCM.

Pia kituo cha habari cha Channel ten kimerejeshwa chamani.

Kwa sasa mapato ya CCM ni zaidi ya sh bilioni 59 kwa mwaka na thamani ya mali zake ni zaidi ya sh bilioni 900

Kadhalika Dr Magufuli amewapongeza wanaccm kwa kuwapokea wabunge na madiwani waliotokea upinzani kwani ujio wao umeiongezea ruzuku CCM kutoka sh bilioni 12 mwaka 2015/16 hadi zaidi ya sh bilioni 13 mwaka 2018/19

Mzee Pinda amesema japo katiba hairuhusu lakini kutokana na utendaji uliotukuka wa Rais Magufuli anamuomba Rais Magufuli atawale walau kwa miaka 15 badala ya ile 10 ya kikatiba.......japo anaamini kuwa Dr Magufuli hawezi kukubali.
 
NAKWEDE,
Hahahaaaa........ Kuna wakati aliweka uzi hapa akiwananga CCM kwamba wasimtanie.

Kumbe alishabadili gia angani?!!!!
 
Duh mbowe kiporo na kwenye dustbin ,kama namuona yale majicho

State agent

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe dada bhana...hivi macho ya Mbowe unayosema kila siku unamzidi nini mfano?
Labda ujinga tu ndo unamzidi..Kwenye familia yenu hamna National au International figure kumfikia Mh.Mbowe ila kila macho ya Mbowe .
Old s.l.u.t

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahahaaaa........ Kuna wakati aliweka uzi hapa akiwananga CCM kwamba wasimtanie.

Kumbe alishabadili gia angani?!!!!
Wakati ule alikuwa anajiuza, ikawa wanapishana na CCM kwenye bei ndo maana alitoa hiyo onyo😃😃😃😃😃
 
Rais Magufuli anahitaji pongezi na sio kwa CCM tu, hata wapinzani, na Watanzania wote hata wasioukua na mlengo wowote kichama.
Kwa sasa anapongezwa Afrika yote, ametenda, anatenda na atatenda, tunamuombea kwa Mungu ampe nguvu na uwezo maana kazi iliyo mbele yake inamuhitaji kwa sana, leo hii akiamua kuachia madaraka, sitegemei kama kunaye atakuja mwenye utashi wa kutekeleza haya ya leo.
 
Hahahaaaa........ Kuna wakati aliweka uzi hapa akiwananga CCM kwamba wasimtanie.

Kumbe alishabadili gia angani?!!!!
Wakati ule alikuwa anajiuza, ikawa wanapishana na CCM kwenye bei ndo maana alitoa hiyo onyo😃😃😃😃😃
 
Lazima kumpongeza na ni lazima kumshukuru.
,Rais dokta muweza wa yote na asieshindwa kwa lolote.” TEAM KUABUDU/KUSUJUDIA
 
Back
Top Bottom