Mwenyekiti wa CCM Dr Magufuli amewashukuru wajumbe wa halmashauri kuu ya chama hichi kwa maamuzi mbalimbali waliyoyachukua katika kuleta mabadiliko.
Kwa mfano kamati ya kufuatilia mali za chama iliyoongozwa na Dr Bashiru iligundua ufisadi mkubwa kwenye mali za chama.
Baada ya kamati ya Dr Bashiru kumaliza kazi yake tumefanikiwa kurejesha mali nyingi mikononi mwa chama na kurekebisha baadhi ya mikataba ikiwemo ya Vodacom na jengo la HQ ya UVCCM.
Pia kituo cha habari cha Channel ten kimerejeshwa chamani.
Kwa sasa mapato ya CCM ni zaidi ya sh bilioni 59 kwa mwaka na thamani ya mali zake ni zaidi ya sh bilioni 900
Kadhalika Dr Magufuli amewapongeza wanaccm kwa kuwapokea wabunge na madiwani waliotokea upinzani kwani ujio wao umeiongezea ruzuku CCM kutoka sh bilioni 12 mwaka 2015/16 hadi zaidi ya sh bilioni 13 mwaka 2018/19
Dr. Magufuli anaihutubia NEC ya CCM jijini Mwanza muda huu na tukio liko mubashara Channel ten.
Mzee Pinda amesema japo katiba hairuhusu lakini kutokana na utendaji uliotukuka wa Rais Magufuli anamuomba Rais Magufuli atawale walau kwa miaka 15 badala ya ile 10 ya kikatiba.......japo anaamini kuwa Dr Magufuli hawezi kukubali.
Chanzo: Channel ten
Maendeleo hayana vyama