Ingawa naelewa unakotokea lakini kwenye hili natofautiana na wewe. Mimi nadhani kuwa kuna umuhimu wa Chadema kuwepo Bungeni kwa sababu zifuatazo:
1. Ingawa tutaliita kuwa ni Bunge la CCM lakini ukweli ni kuwa ni Bunge la taifa la Tanzania lenye wajumbe wengi kutoka CCM. Kwa sababu hiyo kuna haja ya uwepo wa wajumbe wataowatetea wananchi na kusimamia taifa lao.
2. Kuingia kwenye Bunge sio ishara kuwa wamekubali matokeo ya uchaguzi. Wao wanaweza kusema kuwa wanaingia under protest. Watakapoapa hawataapia CCM au NEC bali wataapia Katiba ya taifa lao la Tanzania.
3. Wakiwa Bungeni watakuwa na nafasi nzuri ya kuwatetea na kuwasemea kwa Mamlaka wale wote ambao kwa namna moja ya nyingine wataona kuwa hawajatendewa haki na serikali.
4. Watapata nafasi ya kuwakumbusha wananchi na serikali kuwa kuna wanachama wao, wafuasi wao na watu wengine ambao wako ndani kwa kesi ambazo hazina mashiko. Wataweza tena kuikumbusha serikali kuwa majibu bado yanahitajika kuhusu wale ambao wamepotea katika mazingira potofu.
5. Wakiwemo watampa ujasiri mbunge mwenzao wa Nkasi ambae kuweza kuwasemea watu wake. Ingawa inabidi wamuangalie vizuri kwa sababu kuna uwezekano wa yeye kuhamia upande wa pili.
6. Wakiwa wabunge wa viti maalum wasio na majimbo watapata fursa kuwasimamia wabunge waliotoka katika maeneo yao na kuwakumbusha wananchi kuhusu ahadi zao. Halima anaweza kumuuliza kila siku Askofu kuhusu maendeleo ya chuo cha uvuvi na safari za kwenda Marekani.
7. Wabunge watakuwa huru zaidi kusimamia masuala ya kitaifa bila kuathirika sana na wao kutokuwepo majimboni mwao.
8. Chadema inahitaji pesa za kujiendesha. Ruzukuwatakayopata itawasaidia sana katika kupunguza gharama za kujiendesha na kujijenga upya. Hawataweza kufanya hivyo kwa kutegemea ada na michango.
Angalizo kubwa ni katika uteuzi wa wabunge wa viti maalum. Kipaumbele kitolewe kwa wale ambao wameonyesha wazi kuwa wana uwezo ws kujenga hoja na wana msimamo usiotetereka. Watu kama Halima Mdee, Esther Bulaya, Esther Matiko, Pendolino Peneza, Salome Makamba, Jesca Kishoka, Suzan Kiwanga na wengine wa calibre hiyo bila kusahau vijana kama yule waliyempora ushindi na kumpa John Mrema, yule aliyegombea Muheza na watu kama Mama Mollel.
Aidha waendelee kuwajenga wapambanaji vijana waliojitokeza kama yule wa Chato. Watu kama Heche, Lema, Msigwa, Sugu, Profesa Lwaitama, Askofu Mwamakula watumike kukijenga chama na kuendelea kuisimamia serikali wakiwa nje ya Bunge.
Waongeze ushirikiano na vyama kama ACT WAZALENDO na CHAUMMA kuendeleo shinikizo la kutaka Katiba Mpya, Tume huru ya uchaguzi na mabadiliko katika utendaji wa vyombo vya dola.
Yote haya yanaweza kufanyika hata wakiwa na wawakilishi ndani ya Bunge.
Wakiamua kususa wajue kuwa Chama Tawala kitaendelea kama walivyofanya Zanzibar na hamna watakachoweza kufanya. Presha kutoka nchi za nje si za kutegemea.
Amandla...